Follow us

SOMO: MUNGU ANAHITAJI UMPE NAFASI ILI ATENDE KWENYE MAISHA YAKO

Tangazo

 

SOMO: MUNGU ANAHITAJI UMPE  NAFASI ILI ATENDE KWENYE MAISHA YAKO

Shalom watu wa Mungu leo nimeona niwashirikishe somo hili kwa nia ya kufaidiana kuhusiana na suala zima la kumpa Mungu nafasi katika maisha yetu, kwasababu kwa wewe uliyeamini maisha yako bila Mungu ni sawa na bure kabisa. lakini pale tutakajitambua na kumpa Mungu nafasi ya kwanza ndipo tutakapo Muona Mungu kwa viwango vya juu zaidi, kwani atachukuwa nafasi kubwa na kujidhihirisha kuwa Yeye ndiye Mungu aliye juu ya miungu na kwamba hakuna aliye kama Yeye. lakini watu wengi hatumuoni Mungu katika ukuu wake kwasababu ya kutokumpa Mungu nafasi ya kwanza kwenye maisha yetu, lakini ukisoma Biblia unaweza kuona vile wengetu walivyotendewa katika maisha ya kila siku. karibu ujifunze hakika ninaamini kuna kitu utakachojifunza.

MIFANO KUPITIA IBIBLIA

1. YEHOSHAFATI NA UFALME WA YUDA WALIMPA MUNGU NAFASI, MUNGU AKASEMA NAO. 2Nya20:3-15.

Mpendwa wangu unayesoma ujumbe huu napenda kukushirikisha kitu nilichojifunza kwa Yehoshafati pamoja na watu wake ni kwamba hawa watu walitoa nafasi kwa Mungu kuhusika katika shida yao waliokuwa wanaipitia na Mungu alipoona amepewa nafasi akasema nao. kumbe kama hauna moyo wa kumpa Mungu nafasi kuna uwezekano mkubwa wa kutoisikia sauti ya Mungu au Mungu kusema nawewe, siku za leo ni watu wachache wanaosikia sauti ya MUNGU lakini kitu nilichojifunza katika kisa hiki cha kibiblia ni vile walivyotoa nafasi kwa Mungu, na huu ni ukweli usiopingika kiwango cha watu wengi katika kutoa nafasi kwa Mungu kipo chini sana, watu wengi wanasema wanasikia sauti ya Mungu au Mungu kasema nao lakini kumbe ni waongo. lakini sababu kubwa ni kutokumpa Mungu nafasi katika yale yanayotuhusu. unataka kuisika sauti ya Mungu toa nafasi kwa Mungu, ubize uliona bila Mungu ni kuupiga ngumi upepo. mtafute Mungu (Yesu) mpe nafasi ya kwanza katika mambo yako yote.

2.UFALME WA YUDA WALIPOTOA NAFISI, MUNGU ALIWAPA MAELEZO 2Nya20:13-19.

Uwezi kupewa maelekezo na Mungu kama wewe unajifanya mjuaji na haumpi Mungu nafasi, watu wengi wamekwama kwenye mambo yao kwasababu ya kutokumpa Mungu nafasi ya kuhusika katika mambo wanayoyafanya. sasa mambo yakisha kwama ndio wanarudi kwa Mungu na kuomba msaada, wakati awali walijifanyia wanavyojua. ukweli ni kwamba ni vizuri kumpa Mungu nafasi maana Yeye anajua yote yaliyopita na hata yajayo kama akiona kuna tatizo mbele katika kile unachotaka kukifanya atakupa maelekezo ili upate msaada usije kujikuta kwenye matatizo mabaya na ya kukuzidi uwezo, lakini usipomshirikisha katika mambo yako ni laisi kuingia kwemye ndoa mbaya, biashara mbaya, kazi mbaya, kutokufanikiwa, kufirisika, kuhaibika, mikwamo na kurudi nyumba kimaendeleo. maana mafanikio imara ni yale yanayotokana na  Bwana Yesu na hayo yanaweza kupatikana kwa maelekezo ya Mungu. mpendwa msomaji wangu achana na maisha ya kujiendea bila utaratibu aua maelekezo ya Mungu. kwani kuchagua maisha hayo ni asara kubwa maishani. wengi wapo kwenye mikwamo kwa sababu ya kujifanyia mambo bila ya kumshirikisha Mungu.

3. UFALME WA YUDA WALIPOTOA NAFASI, MUNGU ALIPIGANA VITA BADALA YAO: 2Nya20:20.

Mpenzi msomaji wangu hapa kuna kitu cha kujifunza, yaani hata kama upo kwenye vita katika maisha yako, lakini kama utamshirikisha Mungu au kutoa nafasi kwa Mungu, Mungu atapigana badala yako, lakini kwakuwa watu wengi tunatumia akili zetu kujipigania na kupambana kwa ajili ya maisha yetu inafika mahali tunashindwa kabisa na kujikuta katika hali ya kukata tamaa na kuvunjika moyo kabisa. ndugu yangu nakushauri kabla yakupigana vita elewa kama wewe umeokoka asilimi kubwa vita vinavyoinuka vinatokana na imani tuliyonayo. kwahiyo kama wewe umeokoka unapaswa kuelewa kuwa vita ni vya Bwana sio vya kwetu.

4. UFALME WA YUDA WALIPOTOA NAFASI, MUNGU ALIWASHINDIA VITA YAO. 2Nya20:22-28.

Sasa unaweza kuona kwa wazi vile Mungu anavyoweza kuhusika na vita vyetu na kutushindia katika vita vinavyojiinua katika maisha yetu. kwahiyo kama wewe upo kwenye vita na ukiangalia hauoni msaada upande wowote kumbuka Bwana wa mabwana yupo, anachoitaji ni wewe kumpa nafasi.

5. KUMPA MUNGU NAFASI KUNA TUPA UWEZO ZAIDI KATIKA KUYAKABILI YANAYOTUKABILI. 2Nya20:3-4, 15-17

Unapotoa nafasi kwa Mungu Mungu anakupa nafasi ya nguvu na uwezo wa kuyakabili yanayokukabili katika maisha yako.



KANISA LA  NCHI YA UKOMBIZI MINISTRY.

(NENO, MAOMBI NA MAOMBEZI)

 

SOMA: 2 MAMBO YA NYAKATI 1:1-13. Utagundua iko faida kubwa sana unayoipata unapomtumikia Mungu kwa njia ya matoleo. Naomba nikushirikishe hizi Baraka maana Mungu anakubariki sana, Anakwenda kufungua Milango yako ya Uchumi, Elimu, Nyota, Mashamba, Ndoa, Watoto wako na mengineyo mengi...Utabadilishwa kama sulemani alivyo ongea na Mungu moja kwa moja (Live) usiku wa manmane  . Na Wewe uko tayari kuwa kama Sulemeni?..Mguse Mungu ili na yeye akuguse.

 TUNAUNUNUZI WA VIFAA HIVI KWA AJILI YA MKUTANO WA INJILI.

 1. SPEAKER.......1....TSHS, 950,000/=

 2. VITAA VYA MADHABAHU..........TSHS, 50,000/=

 3. MAIKI .......WIRELESS......2.....TSHS, 100,000/=

 4. VITI........10......TSHS, 160,000/=

 5. MAIKI 2 ….WIRE…..TSHS, 50,000/=

6. MIXER..1……………..TSHS, 500,000/=

7. TRUBAI  4…………….TSHS,  120,000/=

 

UKIGUSWA KUMTOLEA MUNGU.

 WASILIANA NA MCHUNGAJI

 TUMIA:

 0762756542....M-PESA.......JINA: LAURENT MPOMA

 0714890889.....TIGO PESA....JINA: LAURENT MPOMA

 0782859946.....AIRTEL MONEY......JINA: LAURENT MPOMA.

 

KUTAKUWA NA MAOMBI KWA KILA MTU ATAKAYE MTOLEA MUNGU.

 MUNGU AKUBARIKI SANA

 MAOMBI NA MAOMBEZI

 PIGA : 0762756542, 0782859942, 0714890889

 WATSAP: 0762756542.

                   0714890889

 

Post a Comment

2 Comments