Follow us

SOMO: JINSI NGUVU ZA GIZA ZINAVYOINGIA NDANI YA MTU AU KUITESA FAMILIA BILA MTU KUJUA AU FAMILIA KUJUA

Tangazo

 

MCHUNGAJI LAURENT MPOMA
HUDUMA YA NCHI YA UKOMBOZI
(HEMA LA MAOMBI NA MAOMBEZI)
mchunga

JINSI NGUVU ZA GIZA ZINAVYOINGIA NDANI YA MTU AU KUITESA FAMILIA BILA MTU KUJUA AU FAMILIA KUJUA

MUNGU alivyoumuumba Mwanadamu Kusudi na Lengo lake kuu lilikuwa sio tu kumpa Dunia hii aitawale; Bali Lengo lilikuwa ni KUABUDIWA.

Shetani (Lucifer au Joka) Aliyekuwa Mbinguni kama Malaika Mkuu wa Sifa;Alikitamani Kiti Cha Enzi cha MUNGU BABA,akatupwa Chini yeye na Malaika(Ambao leo ndio Majini na Mapepo) waliomuunga mkono kwenye Kampeni zake za Uasi dhidi ya MUNGU. (Ufunuo 12:7-)

Unatakiwa kujua kitu kimoja Muhimu:

MUNGU hana damu na Nyama,[Kama mimi na wewe] YEYE NI ROHO.(Yohana 4:24)

Mathayo 10:28 isema Msiwaogope wauao mwili wasiweze kuiua roho; afadhali mwogopeni yule awezaye kuangamiza mwili na roho na pia katika jehanamu.

 Sasa Ibilisi Shetani na Mapepo,Majini pia Roho.Hawafanani na MUNGU moja kwa moja ila wana sifa moja iko kama MUNGU; nao hawana mwili wa damu na Nyama.

 Kuna jambo moja la ajabu sana ambalo wanadamu wengi hawalijui na pia Ibilisi hataki walitambue.

MUNGU katika kitu anakiheshimu na huwa haendi kinyume nacho "NI NENO LAKE" na huwa hageuzi.

Alipowapa malaka wanadamu kwa kusema "WAKATAWALE" katika (Mwanzo 1:28) alimaanisha kabisa kwa Kumpa mwanadamu Milki yote ya Dunia hii.Yaani kama vile Yeye anavyotawala Mbinguni, ndivyo alitaka mwanadamu atawale hapa dunia kwa asilimia 100.( Zaburi 115:16)

Kwanini Mwanadamu alipewa Kumiliki hii dunia ?!

 1.Aliundwa (Designed) au kuumbwa kutokana na Mavumbi (Kitu ambacho roho haina)

 2.Sababu nyingine ni Kumzuia Shetani asitawale hapa dunia.Kwasababu mahali pake ni kuzimu 3.Sababu ya Tatu ilikuwa ni Mapenzi yake yatimize hapa duniani(Kupitia Mwanadamu) kama kule Mbinguni.

Sasa katika kitu ambacho Wanadamu wengi wamefungwa fahamu kutokukijua;Ni kwamba MUNGU pamoja na UUNGU wake hawezi kumtawala Mwanadamu kwa Nguvu (Pamoja na kwamba amemuumba yeye) Hawezi bila ruhusa ya Mwanadamu mwenyewe kukubali Kutawaliwa naye.

Sababu Kuu ya kwanza, ni Kwasababu Mungu ALIMUUMBA MWANADAMU NA UTASHI (Maamuzi ya Kufanya au Kuamua Jambo)

Sababu ya pili.

MUNGU anaheshimu Mamlaka sana.

Sababu ya tatu;

MUNGU ni ROHO.

Roho haziwezi kuishi hapa duniani kwasababu kuu mbili

1.Ili uishi hapa duniani lazima uwe Damu na Nyama.

2. Roho haziwezi kuishi hapa kwasababu hazitengenezwa au kuumbwa kuhimili hali ya hewa na mazingira ya hapa duniani.

Kwahiyo ili MUNGU atawale hapa duniani ni lazima "AVAE MWILI" (Yaani Aingie ndani ya Mwanadamu)

Vivyo hivyo Shetani ili atawale hapa duniani ni lazima auingie mwili wa mwanadamu ili afanikishe malengo yake.

NJIA  AMBAZO  MASHETANI  HUTUMIA  KUMWINGIA  MWANADAMU.

1.Madhabahu na Kafara za koo.

2.Ibada za sanamu(Kuabudu miungu na wafu)

3.Uchawi wa kurithi au kununua

4.Kutokuwa na Ulinzi wa Nguvu za MUNGU ndani ya Mtu.

5.Kuwaza kupitiliza na kuruhusu Moyo ujae Uchungu.

6.Kutokumpa YESU Maisha Ayatawale

7.Tamaa ya Mali (Kuwa na Fedha Cheo nk)

8.Vyakula (Vya kishetani kulishwa kwenye ndoto au kutegewa)

9.Manukato (Pepo linaweza likakuingia kupitia harufu flani ya perfumu,Spray ambazo zina roho za kishetani ndani yake.

Kwa mfano kuna Perfurme unaweza kuisikia kwa mtu(Mwanaume au mwanamke) na ghafla ukaanza kupata hisia za kingono.

(Takasa manukato kila unapoyanunua kabla hujayatumia)

10.Mifugo (Pepo linaweza kuingia kupitia Nyama( Kwasababu yanaweza kuishi ndani yake) (Mathayo 8:31)

11.Yanaweza yakaiingia Familia yako kupitia wasaidizi wa ndani.(Mdada wa Kazi au Shamba boi)

12.Ngono (Kukutana kimwili na mtu yeyote asiye sahihi katika maisha yako,ni moja ya njia kuu ya mapepo,Yenye nuksi,magonjwa na mabalaa kukuingia mwanadamu.

13.Aina fulani ya Musiki wenye maneno ya kuhamasisha Mambo ya kishetani (Ngono,Pombe,Uvutaji wa Bangi,sigara shisha,Madawa ya kulevya nk)

Nikipata Wakati nitakufundisha Jinsi ya Kujilinda Kupambana na haya Madudu(Madhabahu za Kishetani na Jinsi ya kujichomoa huko na Matumizi ya Damu ya Yesu; pamoja na Jinsi ya kuwatumia au kufanya kazi na Malaika wa Vita.(Zaburi 91:11) (Waebrania 12:22)

UBARIKIWE SANA

MAOMBI NA MAOMBEZI

WASILIANA NA MCHUNGAJI LAURENT MPOMA

+255714890889

WHATSAP: +255762756542

Post a Comment

0 Comments