Follow us

WANAOHUSIKA NA KUFUNGUA MALANGO YAKO YA BARAKA

Tangazo


1.    1.   MUNGU.

Kwa maombi yako na kukaa kwenye utakatifu na kuliishi kusudi la MUNGU na kumtolea MUNGU zaka na sadaka kwa usahihi na upendo, MUNGU atafungua milango ya baraka kwako. Kumb 28:8 ''BWANA ataiamuru baraka ije juu yako katika ghala zako, na mambo yote utakayotia mkono wako; naye atakubarikia katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako.'' MUNGU anapoiamuru baraka fulani ije kwako hufungua mlango wa baraka hiyo kuja kwako. Ona Mfano hapa ambapo MUNGU aliamuru baraka ya chakula cha mbinguni ishuke kwa wana wa Israeli. Biblia inasema Zaburi 78:23-25 '' Lakini aliyaamuru mawingu juu; Akaifungua milango ya mbinguni; Akawanyeshea mana ili wale; Akawapa nafaka ya mbinguni. Mwanadamu akala chakula cha mashujaa; Aliwapelekea chakula cha kuwashibisha.''  

2. Wewe mwenyewe.

 Kujitambua kiroho, kuomba, kuzijua haki zako kwa MUNGU, maisha matakatifu na ya haki na kubaki katika Eneo ambalo MUNGU amekufungulia mlango wa baraka yako.  Mwanzo 22:17-18 '' katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao; na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia; kwa sababu umetii sauti yangu.'' Ibrahimu kama mwanadamu alipomtii MUNGU alibarikiwa, kwa sababu milango ya baraka ilifunguliwa kwake. Milango ya baraka ambayo adui walikuwa wameikalia MUNGU alisema uzao wa Ibrahimu utaimiliki hiyo milango ambayo adui walikuwa wameichukua. Hata wewe adui zako wanaweza kuifunga milango yako ya baraka, adui zako wanaweza kuichukua milango yako ya baraka. Kazi yako ni kumtii MUNGU sasa na kumcha yeye pekee, Kuishi maisha matakatifu ya Wokovu na kuomba katika KRISTO YESU ili uimiliki tena hiyo Milango ambayo adui zako waliichukua.

2.      Wazazi wako.

Wazazi wako wanaweza kukufungulia mlango wako wa baraka kwa malezi yao, kukusomesha na kukufundisha jinsi ya kumtegemea MUNGU.

 4.Watumishi wa MUNGU.

 Watumishi wa MUNGU wanaweza kukufungulia mlango wako wa baraka kwa kukufundisha Neno la MUNGU na kukufunulia kanuni za MUNGU za kukufanya mlango wako wa baraka ufunguke na Kukuombea.

Mithali 18:20-21 ''Tumbo la mtu litajazwa matunda ya kinywa chake; Atashiba mazao ya midomo yake. Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake.'' 

Mungu akubariki sana

Maombi na maombezi

Mchungaji Laurent Mpoma

(NCHI YA UKOMBOZI MINISTRY TZ)

Piga 0762756542

 

Post a Comment

0 Comments