SOMO: MUNGU ANAHITAJI UMPE NAFASI ILI ATENDE KWENYE MAISHA YAKO
Shalom watu wa Mungu leo nimeona niwashirikishe somo hili
kwa nia ya kufaidiana kuhusiana na suala zima la kumpa Mungu nafasi katika
maisha yetu, kwasababu kwa wewe uliyeamini maisha yako bila Mungu ni sawa na
bure kabisa. lakini pale tutakajitambua na kumpa Mungu nafasi ya kwanza ndipo
tutakapo Muona Mungu kwa viwango vya juu zaidi, kwani atachukuwa nafasi kubwa
na kujidhihirisha kuwa Yeye ndiye Mungu aliye juu ya miungu na kwamba hakuna
aliye kama Yeye. lakini watu wengi hatumuoni Mungu katika ukuu wake kwasababu
ya kutokumpa Mungu nafasi ya kwanza kwenye maisha yetu, lakini ukisoma Biblia
unaweza kuona vile wengetu walivyotendewa katika maisha ya kila siku. karibu
ujifunze hakika ninaamini kuna kitu utakachojifunza.
MIFANO
KUPITIA IBIBLIA
1.
YEHOSHAFATI NA UFALME WA YUDA WALIMPA MUNGU NAFASI, MUNGU AKASEMA NAO.
2Nya20:3-15.
Mpendwa wangu unayesoma ujumbe huu napenda kukushirikisha
kitu nilichojifunza kwa Yehoshafati pamoja na watu wake ni kwamba hawa watu
walitoa nafasi kwa Mungu kuhusika katika shida yao waliokuwa wanaipitia na
Mungu alipoona amepewa nafasi akasema nao. kumbe kama hauna moyo wa kumpa Mungu
nafasi kuna uwezekano mkubwa wa kutoisikia sauti ya Mungu au Mungu kusema
nawewe, siku za leo ni watu wachache wanaosikia sauti ya MUNGU lakini kitu nilichojifunza
katika kisa hiki cha kibiblia ni vile walivyotoa nafasi kwa Mungu, na huu ni
ukweli usiopingika kiwango cha watu wengi katika kutoa nafasi kwa Mungu kipo
chini sana, watu wengi wanasema wanasikia sauti ya Mungu au Mungu kasema nao
lakini kumbe ni waongo. lakini sababu kubwa ni kutokumpa Mungu nafasi katika
yale yanayotuhusu. unataka kuisika sauti ya Mungu toa nafasi kwa Mungu, ubize
uliona bila Mungu ni kuupiga ngumi upepo. mtafute Mungu (Yesu) mpe nafasi ya
kwanza katika mambo yako yote.
2.UFALME
WA YUDA WALIPOTOA NAFISI, MUNGU ALIWAPA MAELEZO 2Nya20:13-19.
Uwezi kupewa maelekezo na Mungu kama wewe unajifanya
mjuaji na haumpi Mungu nafasi, watu wengi wamekwama kwenye mambo yao kwasababu
ya kutokumpa Mungu nafasi ya kuhusika katika mambo wanayoyafanya. sasa mambo
yakisha kwama ndio wanarudi kwa Mungu na kuomba msaada, wakati awali
walijifanyia wanavyojua. ukweli ni kwamba ni vizuri kumpa Mungu nafasi maana
Yeye anajua yote yaliyopita na hata yajayo kama akiona kuna tatizo mbele katika
kile unachotaka kukifanya atakupa maelekezo ili upate msaada usije kujikuta
kwenye matatizo mabaya na ya kukuzidi uwezo, lakini usipomshirikisha katika
mambo yako ni laisi kuingia kwemye ndoa mbaya, biashara mbaya, kazi mbaya,
kutokufanikiwa, kufirisika, kuhaibika, mikwamo na kurudi nyumba kimaendeleo.
maana mafanikio imara ni yale yanayotokana na Bwana Yesu na hayo yanaweza kupatikana kwa
maelekezo ya Mungu. mpendwa msomaji wangu achana na maisha ya kujiendea bila
utaratibu aua maelekezo ya Mungu. kwani kuchagua maisha hayo ni asara kubwa
maishani. wengi wapo kwenye mikwamo kwa sababu ya kujifanyia mambo bila ya
kumshirikisha Mungu.
3.
UFALME WA YUDA WALIPOTOA NAFASI, MUNGU ALIPIGANA VITA BADALA YAO: 2Nya20:20.
Mpenzi msomaji wangu hapa kuna kitu cha kujifunza, yaani
hata kama upo kwenye vita katika maisha yako, lakini kama utamshirikisha Mungu
au kutoa nafasi kwa Mungu, Mungu atapigana badala yako, lakini kwakuwa watu
wengi tunatumia akili zetu kujipigania na kupambana kwa ajili ya maisha yetu
inafika mahali tunashindwa kabisa na kujikuta katika hali ya kukata tamaa na
kuvunjika moyo kabisa. ndugu yangu nakushauri kabla yakupigana vita elewa kama
wewe umeokoka asilimi kubwa vita vinavyoinuka vinatokana na imani tuliyonayo.
kwahiyo kama wewe umeokoka unapaswa kuelewa kuwa vita ni vya Bwana sio vya
kwetu.
4.
UFALME WA YUDA WALIPOTOA NAFASI, MUNGU ALIWASHINDIA VITA YAO. 2Nya20:22-28.
Sasa unaweza kuona kwa wazi vile Mungu anavyoweza
kuhusika na vita vyetu na kutushindia katika vita vinavyojiinua katika maisha
yetu. kwahiyo kama wewe upo kwenye vita na ukiangalia hauoni msaada upande
wowote kumbuka Bwana wa mabwana yupo, anachoitaji ni wewe kumpa nafasi.
5.
KUMPA MUNGU NAFASI KUNA TUPA UWEZO ZAIDI KATIKA KUYAKABILI YANAYOTUKABILI.
2Nya20:3-4, 15-17
Unapotoa nafasi kwa Mungu Mungu anakupa nafasi ya nguvu
na uwezo wa kuyakabili yanayokukabili katika maisha yako.
KANISA LA NCHI YA UKOMBIZI MINISTRY.
(NENO, MAOMBI NA MAOMBEZI)
SOMA: 2 MAMBO YA NYAKATI
1:1-13. Utagundua iko
faida kubwa sana unayoipata unapomtumikia Mungu kwa njia ya matoleo. Naomba
nikushirikishe hizi Baraka maana Mungu anakubariki sana, Anakwenda kufungua
Milango yako ya Uchumi, Elimu, Nyota, Mashamba, Ndoa, Watoto wako na mengineyo
mengi...Utabadilishwa kama sulemani alivyo ongea na Mungu moja kwa moja (Live)
usiku wa manmane . Na Wewe uko tayari kuwa kama Sulemeni?..Mguse
Mungu ili na yeye akuguse.
TUNAUNUNUZI
WA VIFAA HIVI KWA AJILI YA MKUTANO WA INJILI.
1.
SPEAKER.......1....TSHS, 950,000/=
2. VITAA VYA
MADHABAHU..........TSHS, 50,000/=
3. MAIKI
.......WIRELESS......2.....TSHS, 100,000/=
4.
VITI........10......TSHS, 160,000/=
5. MAIKI 2
….WIRE…..TSHS, 50,000/=
6. MIXER..1……………..TSHS,
500,000/=
7. TRUBAI 4…………….TSHS,
120,000/=
UKIGUSWA KUMTOLEA MUNGU.
WASILIANA NA
MCHUNGAJI
TUMIA:
0762756542....M-PESA.......JINA:
LAURENT MPOMA
0714890889.....TIGO
PESA....JINA: LAURENT MPOMA
0782859946.....AIRTEL
MONEY......JINA: LAURENT MPOMA.
KUTAKUWA NA MAOMBI KWA KILA MTU ATAKAYE MTOLEA MUNGU.
MUNGU AKUBARIKI
SANA
MAOMBI NA
MAOMBEZI
PIGA : 0762756542,
0782859942, 0714890889
WATSAP: 0762756542.
0714890889
2 Comments
Aminaaaa
ReplyDeleteAmina Mungu akubariki sana kwa kujifunza maneno ya Mungu
ReplyDelete