NJIA SABA ZA KUKUSAIDIA KUIACHA DHAMBI INAYOKUSUMBUA.
Warumi 6:12 '' Basi, dhambi isitawale ndani ya miili yenu ipatikanayo na mauti, hata mkazitii tamaa zake;''mKama kuna kitu cha kwanza ambacho mwanadamu anatakiwa kushughulika nacho basi ni kuacha dhambi ili kuishi maisha matakatifu.
Mithali 15:3 ''Macho ya BWANA yako kila mahali; Yakimchunguza mbaya na mwema.'' Kwa MUNGU matendo yetu yote yako wazi mbele zake.
Obadia 1:15 ''Kwa maana hiyo siku ya BWANA i karibu juu ya mataifa yote; kama ulivyotenda, ndivyo utakavyotendwa; malipo yako yatakurudia juu ya kichwa chako mwenyewe.''
1Timotheo 1:15 ''Ni neno la kuaminiwa, tena lastahili kukubalika kabisa, ya kwamba KRISTO YESU alikuja ulimwenguni awaokoe wenye dhambi; ambao wa kwanza wao ni mimi.'' Kumbuka kuwa ukimpokea YESU na ukatubu kwake hakika dhambi zako zote zitafuta na MUNGU hatazikumbuka tena. Lakini usipotubu na kuokoka hakika uovu wako utadumu hadi siku unaondoka duniani maana hukutubu na kuacha uovu huo. Kuna watu hudhani kwamba hawawezi kuacha dhambi lakini ukweli ni kwamba huo ni uongo tu wa shetani kuhakikisha mwanadamu huyo haendi uzima wa milele. Kama kuna dhambi inakutesa na hujui jinsi ya kuiacha nakuomba jifunze ujumbe huu na uuhamishie katika matendo utashinda.
NJIA SABA ZA
KUKUSAIDIA KUIACHA DHAMBI INAYOKUSUMBUA.
1. Kumtii MUNGU
kupitia Neno lake Biblia.
Yakobo 4:7-10 '' Basi
mtiini MUNGU. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia. Mkaribieni MUNGU,naye
atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha
mioyo yenu, enyi wenye nia mbili. Huzunikeni na kuomboleza na kulia. Kucheka
kwenu na kugeuzwe kuwa kuomboleza, na furaha yenu kuwa hamu. Jidhilini mbele za
BWANA, naye atawakuza. ''
· Njia muhimu za kumtii MUNGU ni kumpinga
shetani.
· Ni kujitenga na kila jambo la
kishetani.
· Kumtii MUNGU ni kumwabudu katika Roho
na kweli.
2. Kuishi maisha
matakatifu.
1 Petro 1:15 '' bali
kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika
mwenendo wenu wote;'' Mtakatifu kinyume chake ni mtenda dhambi. Kama unataka
kushinda dhambi basi acha dhambi na kuanza kutenda mema, huo ndio utakatifu.
Anza tu kuipenda mbingu kwa kuamua kuishi maisha matakatifu. Jitenge na kila
vishawishi vilivyokufanya uingie dhambini. Jitenge na marafiki wabaya wote.
Acha tabia zako zote ambazo ni za dhambi. Acha ulevi, uzinzi, uongo na kila
dhambi. Amua tu kumpendeza MUNGU kwa kuanza kuishi maisha matakatifu kila siku.
3. Kuokoka.
Yohana 3:16-21 ''Kwa
maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila
mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana MUNGU hakumtuma
Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye
yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina
la Mwana pekee wa MUNGU. Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni,
na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu. Maana
kila mtu atendaye mabaya huichukia nuru, wala haji kwenye nuru, matendo yake
yasije yakakemewa. Bali yeye aitendaye kweli huja kwenye nuru, ili matendo yake
yaonekane wazi ya kuwa yametendwa katika MUNGU. '' Kuokoka ni jambo la muhimu
sana kama unataka kuzishinda dhambi. Kuokoka ndio mwanzo wa mwanadamu kumwabudu
MUNGU katika Roho na kweli. Kuokoka ni kumpokea BWANA YESU kama Mwokozi wako.
Hakuja jambo zuri na muhimu kwa kila mwanadamu kama kumpokea YESU na kuanza
kuishi maisha matakatifu.
4. Kujitenga na
dhambi.
Warumi 6:23 '' Kwa
maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele
katika Kristo Yesu Bwana wetu.'' Biblia iko wazi sana ikisema kwamba dhambi ina
matokeo mabaya sana. Dhambi ina mshahara na huo mshahara unaitwa mauti yaani
kutengwa na MUNGU. Na mauti hiyo kama Mwanadamu huyo hatatubu maana yake mauti
hiyo ya dhambi itazaa jehanamu. Kama unataka kushinda dhambi hakikisha
unajitenga na kila dhambi. Kila kisababishi cha dhambi hakikisha unakaa mbali
nacho.
5. Kuutumia muda wako
wote vizuri na kwa malengo mema.
Waefeso 5:15-17
''Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali
kama watu wenye hekima; mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu. Kwa
sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya BWANA.''
Biblia inakushauri kuukomboa wakati maana nyakati hizi ni nyakati za maovu
mengi. Muda ambao unautumia disko ungeutumia kwa MUNGU ungeziepuka dhambi.
6. Kufunga na kuomba.
Mathayo 17:21
''Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.'' Kazi mojawapo ya maombi
ni kuutiisha mwili ili tamaa mbaya zisiinuke. Kazi mojawapo ya maombi ya
kufunga ni kuifanya roho yako iutawale mwili na sio mwili kuitawala roho. Kama
huwa huwezi kupata muda wa kuomba ni ngumu kushinda ya dunia. Kama huwa huwezi
kupata muda wa kufunga na kuomba ni ngumu kushinda dhambi. Nakushauri kuanzia
leo uwe na muda wa kuomba na kufunga itakusaidia.
Ø Tafuta ushindi wako
katika maombi.
Ø Ita utakatifu
kupitia maombi yako.
Ø Ita nguvu za
kuishinda dhambi kupitia maombi.
Ø Utiishe mwili wako
kupitia maombi na kufunga.
7. Kuenenda kwa ROHO
MTAKATIFU.
Wagalatia 5:16 ''Basi
nasema, Enendeni kwa ROHO, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.'' Kazi
mojawapo ya ROHO wa MUNGU ndani yetu ni kutusaidia kushinda mambo yote ya
ulimwengu. Changamoto ya wanadamu ni jinsi ya kumpata huyo ROHO MTAKATIFU maana
yeye hachangamani na uovu, yeye ni mtakatifu na akiingia ndani yako atakusaidia
kuishi maisha matakatifu ila kama tu ukimtii. Mambo mengi yanayokuja mbele yako
ni mapando ya giza ili kukufanya utende dhambi, lakini akiwapo ROHO wa MUNGU
atakusaidia jinsi ya kuepuka dhambi. Unaweza kukuta Binti unaitwa na rafiki yako,
yule rafiki yako anakuwa amepanga akupe madawa ya kulevya kisha atembee na
wewe, Kama una ROHO wa MUNGU ni lazima tu atakukataza kwenda maana yeye anajua
jambo kabla hata halijatokea. ukimtii ROHO wa MUNGU utashinda.


0 Comments