MAMBO SABA(7) YANAYOWEZA KULITAFUNA
KANISA.
UTANGULIZI
Kanisa ni watu walioitwa na kutengwa
na mambo ya dhambi.
1 Kor 6:17-18 '' Kwa hiyo, Tokeni
kati yao, Mkatengwe nao, asema BWANA, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami
nitawakaribisha. Nitakuwa BABA kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na
wa kike,''
Maandiko hayo ni sehemu tu ndogo ya
maandiko yanayolitambulisha Kanisa la KRISTO duniani.
Kanisa hai wametengwa na uovu wa
dhambi na wametengwa na mambo ya kidunia
yaliyo machukizo(Machafu).
Ndio maana huwezi kumuona Askofu
akiwa disko akicheza.
Huwezi kumuona Mkristo aliyeokoka
akiwa kwa mganga wa kienyeji.
Huwezi kumuona Mchungaji anatoa talaka.
Huwezi kumuona Mteule wa MUNGU akivuta
sigara wala bangi na tena huwezi kumuona mteule wa KRISTO akitumia madawa ya
kulevya.
Huwezi kuona kanisa wakichukua mapanga na mikuki
wakienda kulipiza kisasi kwa maadui zao.
Kanisa ndilo pekee linalosababisha
amani Duniani.
Kanisa ni la muhimu sana duniani.
Siku Kanisa la MUNGU likiondolewa
duniani ndipo neema itatoweka.
Kibiblia katika migao saba ya nyakati
huu ni wakati wa Kanisa au wakati wa Neema.
Kanisa la KRISTO ndilo pekee
linalomwabudu MUNGU aliye hai na wa kweli
1.Dhambi kwa viongozi wa kanisa.
Hosea 4:6 ''
Watu wangu wanaangam Madhara makubwa zaidi yanayoweza kuliathiri kanisa ni
dhambi kwa viongozi wa kanisa. Watu wa kanisani wanaweza wakaangamizwa sawasawa
na watu wa mataifa kwa sababu ya viongozi wa kanisa. Kiongozi wa kanisa
akiisahau sheria(Neno la MUNGU lote) anaweza kusababisha matatizo makubwa ya
kiroho kwa kanisa.
Kiongozi
akiwa mdhambi itakuwa vigumu sana yeye kukemea dhambi katika kanisa na kwa njia
hiyo watu wa MUNGU watakuwa wanaangamiza kwa kukosa maarifa.
Kama
mchungaji ni mzinzi ni vigumu sana yeye kukemea uzinzi.
Kama
Mchungaji ni mwizi ni vigumu sana kukemea wizi.
Kama Askofu
ni muongo ni vigumu sana kukemea uongo kanisani.izwa kwa kukosa maarifa; kwa
kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu
mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto
wako.''
2.Viongozi wa kanisa kutendea kazi kila neno wanaloambiwa na waumini au jirani
wa waumini.
1 Timotheo 5:19-22 ''Usikubali mashitaka juu ya mzee,
ila kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu. Wale wadumuo kutenda dhambi
uwakemee mbele ya wote, ili na wengine waogope. Nakuagiza mbele za Mungu, na
mbele za Kristo Yesu, na mbele za malaika wateule, uyatende hayo pasipo
kuhukumu kwa haraka; usifanye neno lo lote kwa upendeleo. Usimwekee mtu mikono
kwa haraka, wala usizishiriki dhambi za watu wengine. Ujilinde nafsi yako uwe
safi.''
Katika maandiko
haya tunaweza kujifunza mambo mengi sana lakini kulingana na somo langu katika
kipengele hiki cha pili, kunahitajika umakini sana kwa viongozi wa kanisa
katika vile wanavyoambiwa na waumini au majirani wa baadhi ya waumini.
Kwanza
kiongozi anapoambiwa jambo na mmoja wa waumini wake ambalo linamweka hatiani
mtu mwingine haitakiwi kiongozi huyo kumwita haraka haraka tu mtuhumiwa na
kumuonya au kumtenga, mambo hayo yanalitafuna sana kanisa leo.
Haina maana
kwamba usifanyie kazi unayoambiwa na waumini wako au majirani wa waumini wako
lakini hakikisha unafanya uchunguzi wa
kina wewe mwenyewe ili pasitokee uonevu. Kama kuna mtu umemuonea wewe mchungaji
hakika mtu huyo hata kama atakuwa anakuja kanisani lakini hatakusikiliza na
hatazingatia Neno la MUNGU unalomfundisha, hadi uweke mambo sawa.
Mara
nyingine watu wenye makosa ndio huwa wa kwanza kukimbilia kwa Mchungaji ili
kuwasema wengine kama njia ya kujisafisha na kuonekana wema.
Inawezekama
mmoja wa wana kanisa anatuhumiwa na mtu mwingine wa kanisani kwamba ni mzinzi
kwa sababu tu alionekana akitembea barabarani saa saba usiku. Mchungaji kama
atamwita mtuhumiwa haraka tu na kumfukuza kanisani au kumsema hadharani
kanisani, na kama jambo hilo amesingiziwa hakika hapo kanisa litakuwa
limetafunwa sana maana huyo naye anaweza akaanza kuitafuta haki yake kwa nguvu,
anaweza akaacha kwenda kanisani na kujiangamiza kabisa, anaweza akarudi nyuma
kiroho.
Kama
amekosea inabidi kiongozi ajilidhishe kwanza ndipo atoe hukumu. Namna nzuri ya
kujilidhisha ni kupata ushahidi kutoka kwa watu wawili au watatu ndivyo Biblia
inashauri hapo juu.
Dhambi
lazima zikemewe kanisani lakini iwe ni kweli dhambi imetendeka, sio
kusingiziwa.
Biblia
inakushauri kiongozi wa kanisa kwamba usihukumu kwa haraka ila thibitisha
kwanza. Usipendee mtu, lakini kama utaamua haraka haraka tu mambo yanayowahusu
waumini hakika unaweza kujikuta umependelea pasipo sababu.
3.Kuwepo wakala wa shetani katikati
ya kanisa.
1 Yohana 4:1-3 ''Wapenzi, msiiamini kila roho, bali
zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na MUNGU; kwa sababu manabii wa uongo
wengi wametokea duniani. Katika hili mwamjua ROHO wa MUNGU; kila roho ikiriyo
kwamba YESU KRISTO amekuja katika mwili
yatokana na MUNGU. Na kila roho isiyomkiri YESU haitokani na MUNGU. Na hii
ndiyo roho ya mpinga Kristo ambayo mmesikia kwamba yaja; na sasa imekwisha
kuwako duniani.''
Shetani
hutaka sana kuingia kanisani ili aharibu utakatifu wa kanisa.
Kanisa ni
lazima lisimame katika kweli ya Neno la MUNGU.
Viongozi wa
kanisa ni lazima sana walisimamie kusudi la MUNGU kwa kulitii sana Neno la
MUNGU.
Kwa tamaa za
pesa le kuna baadhi ya watumishi hutunga vitu vya uongo ili tu kujipatia
waumini au kupata pesa.
Sio kila
miujiza ni ya MUNGU na sio kila anyehubiri watu ni anataka watu hao waende
uzima wa milele. Kila mtu anaweza kuwa mchungaji akiamua lakini kama huyo
hamtii KRISTO hakika huyo ni wakala wa shetani kanisani.
roho ya
mpinga Kristo ipo na kazi yake ni kuaondoa watu kwa KRISTO.
Hatuhitaji
kumwabudu MUNGU kupitia sanamu au maji ya baraka, hatutakiwi kumwabudu MUNGU
kupitia watu wanaojiita MUNGU.
Tunatakiwa
kumwabudu MUNGU kupitia YESU KRISTO na sio vinginevyo.
4. Kanisa kuacha maombi.
1 Thesalonike 5:17 '' ombeni bila kukoma; ''
Maombi ni
maisha hivyo hayatakiwi kuwa ya msimu tu bali ya siku zote.
Kanisa
likisahau maombi kuna madhara yatatokea maana kuona rohoni kutapungua, hamu ya
kuendelea na wokovu itapungua.
Kanisa
lisipokuwa na maombi ni rahisi shetani kupanda magugu ndani ya kanisa na
kuyang'oa magugu hayo ikawa ni vigumu.
Kanisa
halitakuwa kuwa na maombi tu bali pia ni lazima kanisa liwe na maombi ya
kufunga kila mara.
Kanisa kama
mtu binafsi wa kanisani lazima afundishwa kuomba na kufunga na awe anafunga ili
kunoa makali yake ya kiroho na ili aweze kujibiwa mahitaji yake anayakayo.
Kuna mengine
hayawezi kuondoka katika kanisa hadi kanisa lifunge na kuomba.
Mathayo 17:21 ''Lakini namna hii haitoki ila
kwa kusali na kufunga.''
5. Kanisa kutembea katika maono ya
uongo yanayoambatana na ujanja ujanja wa watumishi.
Mathayo 15:8-9 ''Watu hawa huniheshimu kwa midomo; Ila
mioyo yao iko mbali nami. Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo
maagizo ya wanadamu.''
Kama kanisa
litamwacha KRISTO na Neno lake hakika shetani atachukua nafasi tu na jambo hilo
kupelekea uongo kuanza kuliendesha kanisa.
shetani
akitawala kanisa ni lazima waumini wawekewe mipaka na kufundishwa kujiona
kwamba wao tu ndio kanisa na kwingine kote ni kwa shetani. Biblia ndio
inatakiwa iwe ushahidi na sio watumishi kuwadanganya watu.
Sio kila
mchungaji au Askofu ameitwa na MUNGU, Wengine wamejita na wengine wameitwa na
shetani.
Shetani ni
baba wa uongo hivyo na watumishi wake lazima wabuni vitu vya uongo na lazima
kanisa litembee katika maono ya uongo, mambo haya yanalitafuna kanisa sana.
Leo kuna
wachungaji hawamhubiri KRISTO tena bali wanajihubiri wenyewe na kudanganya
watu. Kanuni ya Biblia pia inatafasiriwa vibaya na baadhi ya watu. Ngoja
nikuambie; Japokuwa Ibrahimu Ni Baba Wa Imani Lakini Hiyo Haina Maana Kwamba
Sara Ni Mama Wa Imani. . Mambo Ya Kiroho Huwa Tofauti Na Mambo Ya Kibinadamu.
Tukiruhusu Kanisa Liifuate Dunia Basi Ipo Siku Tutasikia Kwamba Stephano Au
Ayubu Ni Babu Wa Imani. Dunia Leo Imeingia Kanisani Ndio Maana Kuna Mawakala Wa
shetani Hujipachika Katika Baadhi Ya Maandiko Na Kudai Maandiko Hayo
Yaliwatabiri Wao. Kuna Watu Hudai Wao Ni Eliya Amerudi Duniani, Kuna Watu
Hujiita Kristo, Kuna Watu Hujiita Henoko Aliyerudi Duniani, Wengine Hudhani
Kuna Mtu Anaitwa Mama Wa Mungu leo. Kuna Watu Hujiita Mungu Muumbaji Aliyekuja
Kuishi Na Wanadamu Na Kuna Waongo Original Hudai Biblia Iliondolewa Zamani Na
Kuja Kitabu Kingine. Kanuni Ya Biblia Iko Tofauti Sana Na Kanuni Za Kibinadamu
Au Kanuni Za Kimwili. Ukitaka Biblia Ikufuate Utaishia Pabaya. Wewe Mwanadamu
Ndio Unatakiwa Uifuate Biblia. Biblia Haiwezi Kubadilishwa Na Mazingira Wala
Haiwezi Kubadilishwa Na Wanadamu. Kataa Kuokoka Harafu Utarajie Mbingu, hakika
hakuna mbingu kwa wanaokataa kuokolewa na BWANA YESU(Yohana 3:16-21). Mkatae
YESU Ukidhani Utafika Mbinguni, hakika huwezi kufika(Matendo 4:12)
6.
Kanisa kukosa upendo.
1 Petro
1:22-23 ''Mkiisha kujitakasa roho zenu kwa kuitii kweli, hata kuufikilia
upendano wa ndugu usio na unafiki, basi jitahidini kupendana kwa moyo. Kwa kuwa
mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika;
kwa neno la Mungu lenye uzima, lidumulo hata milele. ''
Upendo wa KiMUNGU ni hali ya kumpenda mtu bila
kujali mtu huyo alivyo au ana sifa gani.
Lazima
kanisa liwe na upendo. Kanisa lazima limpende mchungaji wao na sio kumsema
vibaya. Kumbuka kuwa mkimsema vibaya mchungaji wenu hakuna atakayemsema vizuri
huko nje, hakuna atakayekuja kuokoka maana atadhani kanisa halifai kumbe ni
kukosekana kwa upendo.
Lazima
kanisa wapendane wote bila kujali cheo cha mtu au hadhi ya mtu. Ukikosekana
upendo wa kiMUNGU kanisani hakika jambo hilo litalitafuna sana kanisa na kanisa
halitastawi kamwe.
''Upendo huvumilia, hufadhili; upendo
hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni; haukosi kuwa na adabu; hautafuti
mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya; haufurahii udhalimu, bali
hufurahi pamoja na kweli; huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote;
hustahimili yote.-1 Kor 13:4-7 ''
7.
Kutokubali kukosolewa au kusahihishwa.
1 Kor
8:2 ''Mtu akidhani ya kuwa anajua neno,
hajui neno lo lote bado, kama impasavyo kujua.''
Hakuna
mwanadamu anayejua yote na hakuna mwanadamu anayeweza yote.
Katika
kanisa wote tunategemeana. Hata Mchungaji kuna baadhi ya mambo hajui na anahitaji
kusaidiwa, Hata mama mchungaji sio kwamba anajua yote kuliko wanawake wote
kanisani. Sio kwamba wazee wa kanisa hawana la kusaidiwa bali yapo tena mengi.
Sio kwamba
matumizi ya kanisa yakienda vibaya basi wanaotaka kushauri wafukuzwe kanisani.
Vitu vya kanisa
ni vya kanisa na sio mali ya kiongozi wa kanisa hivyo kuna wengine akitaka
kusaidiwa tu kwa upole anaanza kuhubiri kwamba roho ya uasi na kukosa heshima
imeingia kanisani.
Kama
Mchungaji angekuwa anajua yote ana anaweza yote basi kusingekuwepo kiongozi wa
ibada kanisani, kusingekuwepo mashemasi kanisani, kusingekuwepo wapiga vyombo
na kusingekuwepo waimbaji. Lakini kwa sababu kila mtu kanisani ni muhimu basi
ni muhimu sana kusaidiana ili kuondoa lawama zisizokuwa na sababu.
Asante kama
umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
MUNGU WA
MBINGUNI AKUBARIKI SANA.
WAKO KATIKA
UTUMISHI WA MUNGU ALIYE HAI
BISHOP
LAURENT MPOMA
HUDUMA: NCHI
YA UKOMBOZI MINISTRY
MWAJA KITOPE
– SINGIDA MJINI
USHAURI NA
MAOMBEZI
0714890889
WHATSAP:
+255762756542

0 Comments