MAMBO MATANO YA KUSHUKURU
Siku zote maisha
si rahisi. Siku zingine mambo yote huenda ovyo na unahisi kwamba haiwezi kuwa
mbaya Zaidi. Nyakati nyingine mambo huenda vyema na maisha unayahisi kuwa
mazuri. Lakini wewe unaeishi kwa ajili ya Mungu, unaweza kuwa na shukrani kila
wakati – bila kujali unavyohisi.
“Shukuruni kwa kila jambo; maana hayo
ni mapenzi ya Mungu kwenu katika kristo.” 1 Wathesalonike 5:18
Mawazo yenye
shukrani yana athari kubwa maalumu kwetu sisi. Ukosoaji, kulalamika na mawazo
ya giza hukimbia unapochagua kuwa mwenye shukrani hata katika hali mbaya Zaidi.
Je! Hii si silaha yenye kutumika ambayo unapaswa kuwa nayo maishani mwako?
Kila mara
una jambo la kushukuru, bila kujalisha mahali ulipo wala unavyohisi.
1. Umeapokea uzima!
Kwamba u
mzima si tu kwa sababu ya nafasi. Mungu amekupangia uzaliwe na uishi duniani
kwa muda mfupi, na anataka uishi maisha ya furaha. Wale wanaoishi maisha yao
kwa kufuata mapenzi ya Mungu, wataona kwamba hivi ndivyo ilivyo kabisa!
Si tu kwamba
anakupa uzima, lakini pia hukupatia ushauri mzuri wa namna ya kuishi. Hupaswi
kutilia shaka hili. Unachopaswa kufanya ni kufungua biblia kutafuta sheria za
Mungu, na zote ni za kweli kwa 100%. “ Anayebariki wengine hubarikiwa sana .” Mithali 11:25. “Kwa maana, atakayependa
maisha, na kuona siku njema, auzuie ulimi wake usinene mabaya, na midomo yake
isiseme hila.” 1Petro 3:10.
Fikiria
kwamba Mungu anakupenda sana kwamba alikupa uzima, eneo zuri la kuishi (Dunia)
na sheria zake kamili kuishi ndani yake. Hili ni jambo la kushukuru sana!
2.
Kamwe hauko peke yako
Watu wengi
wapo katika hatua moja katika maisha yao huhisi kwamba hakuna mtu anaewaelewa,
hakuna mtu anayewafahamu, hakuna mtu anayejali. Lakini unapaswa kujua kwamba
kila wakati una rafiki, mtu ambaye hukusaidia na una baba ambaye yu pamoja
nawe. Bila kujali unapoishi, unapoenda na unachofanya, Mungu yupo hapo. Yupo
kwa ajili yako. Daudi anaandika juu ya hili;
“Wewe
wajua kuketi kwangu na kuondoka kwangu; umelifahamu wazo langu tokea mbali.
Umepepeta kwenda kwangu na kulala kwangu, umeelewa na njia zangu zote.” Zaburi 139:2-3.
Mungu
hukutazama, hukusaidia. Anakupenda hivyo hawezi kukuacha uwe mpweke. Ni salama
kuwa karibu nae. Hili ni jambo la kushukuru.
3. Unaweza kujawa na furaha wakati wa
majaribu
Hakuna mtu
anaishi bila kupitia mateso. Hali ngumu majaribu yanapokuja, unaweza kujaribiwa
kutilia shaka kwamba Mungu anajua lililo jema kwako, kwa kuwa ameacha mambo
haya yatokee. Lakini Mungu anajua kilicho bora kwako, kwa sababu anataka
kukufundisha kwa kupitia majaribu haya, ili mwishoni uweze kushiriki katika
asili ya utauwa. (Yakobo 1:12; 2Petro
1:4.)
Mungu anajua
hali gani unapaswa kuwa nayo kujiandaa kwa ajili ya mbingu. Kama unaamini hili,
unaweza kujawa na furaha hata unapokuwa katika ugumu ya kibinadamu.
Wanachohofia wengine, makwazo na kuwa na uchungu, inaweza kuwa kitu chanya
kwako.
Katika
majaribu unaona maumivu yako, hasira, tuhuma, wivu, mapenzi yako mwenyewe n.k.,
na kwa kutokujitoa kwa dhambi hizi, taratibu utamalizana na dhambi hizi katika
asili yako. Ndipo utapata tunda la roho maishani mwako! Hivyo kuna sababu kubwa
kujawa na furaha wakati wa majaribu – kwa kuwa hukuleta karibu na mbingu.
“Ndugu
zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali;
mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa Imani yenu huleta subira. Subira na iwe na
kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa na neno.” Yakobo 1:2-4.
Fikiria
kwamba una sababu ya kuwa na furaha juu ya mambo ambayo wengine huyaona kama
mzigo! Mungu anajua unachohitaji na hukusaidia kwa njia yote! Hili ni jambo la
kushukuru.
4. Mungu anakupenda sana
“Kwa maana
jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe wa pekee, ili kila
mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.” Yohana 3:16.
Kifungu hiki
ni kwa ajili yako: “Mungu alikupenda hata akamtoa mwanawe wa pekee, ili wewe
umwaminiye usife bali uwe na uzima wa milele.” Mungu aliwaza juu yako
alipomtuma Yesu, mwanawe mpendwa duniani kuwa mwanadamu ili uokolewe. Kupitia
Yesu unaweza kupata msamaha wa dhambi zote ulizotenda na kuanza upya. Unapata
nafasi ya kuishi kama Yesu mwenyewe, huru kutoka katika dhambi zote! (Warumi 6:22) Mungu anatafuta kuwa na
ndugu kama yeye – wale wanaomfuata na kutafuta mapenzi ya Mungu katika mambo
yote.
Mungu
anatupenda sana kiasi kwamba alimtoa mwanawe sadaka, Yesu, aliyefanya iwezekane
kwamba tusitende dhambi tena. Hilo ni jambo la kushukuru.
5. Una baadae yenye tumaini
Unaweza
kuitazamia baadae! Unapokuwa umemkabidhi Mungu maisha yako yote na mapenzi yako
yote una baadae yenye tumaini, katika maisha na katika uzima wa milele.
Siku moja
utakutana na Yesu tena. Na utakutana na wengine walioishi maisha ya kiuanafunzi
kama ambavyo unayoishi, na mtajawa na furaha pamoja nao! Baada ya hapo unaweza
kuwa katika dunia mpya ambapo roho wa Mungu mwenyewe atatawala na hapatakuwa na
dhambi tena. Kila jambo katika dunia mpya hutokea kwa Imani, tumaini na upendo.
(Ufunuo wa Yohana 21:1-3; 1Wakorintho
13:13.)
Ikiwa
umeishi kwa ajili ya Mungu hapa duniani, unaweza kuitazamia siku ambayo utakuwa
na Yesu. Fikiria kuhusu kuchaguliwa kwa ajili ya jambo kama hili! Ni tumaini
kiasi gani! Hili ni jambo la kushukuru sana!
Ayubu 14:7
“Kwa maana
lipo tumaini kwa mti; kama ukikatwa utachipuka tena, nayo machipukizi yake
mapya hayatakoma.
MAOMBI NA MAOMBEZI
WASILIANA NA MCHUNGAJI LAURENT MPOMA
0763652896
WHATSAP: 0762756542
0 Comments