KANUNI ZAKUFANYA ILI MAOMBI YAKO YAJIBIWE NA MUNGU
1 Muombajisharti usiwe mwenye dhambi.
"Tunajua
kwamba Mungu HAWASIKILIZI watu wenye Dhambi, ila humsikiliza yeyote mwenye
kumcha na kutimiza mapenzi yake" ( Tafsiri ya Habari Njema )
👉 Umeona kwamba Neno la Mungu limeweka
wazi kabisa kwamba unapokuwa mwenye dhambi Mungu hatakusikiliza kabisa wakati
unamuomba. Kwahiyo ili Mungu ajibu maombi yako ni lazima uishi maisha ya
Utakatifu, achana na kufanya dhambi kwa siri/kujificha.
2 Muombajisharti ukae ndani ya kristo Yesu.
"NinyiMKIKAA Ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, Ombeni mtakalo lote
nanyi mtatendewa"
👉 Mungu hawezi kuyajibu maombi yako
kama wewe hujakaa ndani ya Yesu Kristo. Ninaposema kukaa ndani ya Yesu Kristo
maana yake nilazima Uokoke sawa.
3 Muombajisharti Uombe kwa Bidii sana.
"Eliya
alikuwa mwanadamu mwenye tabia moja na sisi, AKAOMBA kwa BIDII mvua isinyeshe,
na mvua haikunyesha juu ya nchi muda wa miaka mitatu na miezi sita"
Eliya
aliomba kwa bidii sana kuhusu mvua kutonyesha na Mungu akajibu hayo maombi
yake.
"Basi
Petro akalindwa gerezani, nalo kanisa LIKAMWOMBA Mungu kwa JUHUDI/BIDII kwa
ajili yake"
Hapa
tunaliona kanisa likimuombea kwa bidii Petro wakati alipokamwatwa na mfalme
Herode na kutokana na kanisa kuomba kwa bidii Mungu alisikia maombi yao
akawajibu na kumtoa Perto ndani ya gereza.
Kuomba kwa
bidii maana yake ni kuomba bila kukata tamaa aidha kwa kukatishwa na wanadamu
au mazingira.
MAHITAJI AU UNAHITA MAOMBEZI TUMA HAPA
0 Comments