Follow us

SOMA KISA HICHI KILICHOMKUTA HUYU BABA BAADA YA SIMU KUITA BAHATI MBAYA AKIWA KANISANI

Tangazo

 


Soma Kisa Hichi Kilichomkuta Huyu Baba Baada ya Simu Kuita Bahati Mbaya Akiwa Kanisani

Simu yake iliita kwa Bahati mbaya wakati wa ibada akiwa kanisani

 Mchungaji alimfokea

 Waumini walimzonga baada ya maombi ya ibada

Wakati anarudi nyumbani, njia nzima mkewe aliendelea kumsema kwa kutokuwa makini

Akajisikia vibaya sana, huzuni, na aibu juu

 Jioni yake, ili kupoteza mawazo, alikwenda bar

 Aliagiza bia, akaiweka mezani. Kwa kuwa alikuwa na mawazo mengi, akaigusa pombe ikamwagika

 Muhudumu alikuja, akampa pole kwa unyenyekevu, na akafuta meza kiustaarabu, kisha akamfuta jamaa ilipommwagikia kiunyenyekevu

 Meneja wa bar ile alimpa jamaa bia ya ofa kufidia iliyomwagika

Muhudumu wa kaunta alipomletea alim'busu akim'bembeleza, "Usijali, hakuna ambaye hana makosa!"

 Jamaa hajawahi kukosa 'ibada' ktk bar hiyo tangu siku ile

 SOMO:

Unavyowatendea watu kunaweza kujenga au kuwabomoa, hasa wanapokosea

Post a Comment

0 Comments