Mithali 10:22
[22]Baraka
ya BWANA hutajirisha,
Wala
hachanganyi huzuni nayo.
Ee Bwana
Yesu, naomba Baraka zako ulizonibariki ROHONI ziwe halisi katika ulimwengu
unaooneka kwa jina la Yesu.
Mithali 21:5
[5]Mawazo ya
wenye bidii huuelekea utajiri tu;
Bali kila
mwenye pupa huuelekea uhitaji.
Bwana Yesu,
ninaomba mawazo yangu na maneno ya kinywa changu yapate kibali mbele zako.
Mawazo yangu yawe ya mtu mwenye bidii, mawazo yangu yavute utajiri na heshima
kwa jina la Yesu.
Kila mahali
ambapo fedha na utajiri na heshima yangu imefichwa naamuru moto ufike hapo kwa
jina la Yesu.
Kila tumbo
lililoficha hazina ya utajiri na fedha zangu. Naamuru lipasuke lizitapike mali zangu na Baraka za
Bwana juu yangu kwa jina la Yesu
Ninakataa
kuwa mhitaji kwa jina la Yesu, Bwana wewe ni mchungaji wangu, nakataa
kupungukiwa na kitu.
Njoo kwenye
maono, njoo kwenye ndoto, njoo kwenye mawazo. Unipe hekima kuyaelekea maji ya
utulivu, nipe macho ya kuona malisho ya hatma yangu kwa jina la Yesu.
Roho
Mtakatifu, naomba uutengeneze upya moyo wangu.
Ondoa tabia ya pupa ndani yangu ili
nisiangukie kwenye kundi la wahitaji na masikini. Bwana Yesu, nakusihi kwa
mamlaka yako, niumbie moyo mpya wenye utulivu ndani yangu.
Nijulishe hekima kwa siri, nifanye kuwa mtu
mkuu kwa utukufu wako kwa jina la Yesu
Mithali 21:6
[6]Kupata
akiba ya mali kwa ulimi wa uongo
Ni moshi
upeperushwao; ni kutafuta mauti.
Bwana
nakuomba unifunge kinywa nisinene kwa uongo. Naomba mauti iniepuke kwa jina la
Yesu.
Mauti ya
biashara, mauti ya mtaji, mauti ya kazi na kibali futika kwa jina la Yesu.
Nakuomba
Bwana wangu, unirehemu na unisamehe. Mahala popote nilipotumia uongo ili
kujipatia fedha na akiba unisaidie nisipatikane na madhara.
Natubu na
naacha uongo . Ee Bwana uniinue na kunisimamisha kiuchumi kwa jina la Yesu.
Mithali 22:4
[4]Thawabu
ya unyenyekevu ambao ni kumcha BWANA
Ni utajiri,
na heshima, nayo ni uzima.
Bwana,
unifanikishe kwa hekima yako na nguvu zako. Unijaze moyo wa unyenyekevu na haki
yako.
Unihuishe na
kukifuta kiburi cha moyo wangu kwa jina la Yesu.
Achilia Baraka kwenye maisha yangu na uniinue
kutoka katika umasikini kwa jina la Yesu.
Mithali 23:4
[4]Usijitaabishe
ili kupata utajiri;
Acha
kuzitegemea akili zako mwenyewe.
Bwana
nimejua leo kwamba utajiri wa kweli unatoka kwako.
Ninaomba
unijaze maarifa yako na nguvu zako, nakataa kujitumainia, nahamisha ufahamu na
akili yangu kwako. Unishike kwa hekima yako.
Nakataa
utajiri wa mateso, unibariki na kunitajirisha kwa jina la Yesu
Isaya 60:5
[5]Ndipo
utakapoona na kutiwa nuru,
Na moyo wako
utatetemeka na kukunjuka;
Kwa kuwa
wingi wa bahari utageuzwa kukujia,
Utajiri wa
mataifa utakuwasilia.
Bwana,
unabii huu utimie kwenye maisha yangu haraka kwa jina la Yesu.
Utajiri wa
mataifa na uje juu yangu leo kwa jina la Yesu.
Kila
kilichokuwa kinazuia fedha zangu mahali naamuru kianguke kwa jina la Yesu.
Uchumi
wangu,
Isaya 60:11
[11]Malango
yako nayo yatakuwa wazi daima;
Hayatafungwa
mchana wala usiku;
Ili watu
wapate kukuletea utajiri wa mataifa,
Na wafalme
wao wakiongozwa pamoja nao.
Ee Malango
yangu, sikia Neno la Bwana.
Funguka na
uache utajiri wangu uje. Funguka na uache heshima yangu ionekane.
Kila hazina
iliyokuwa imefichwa, naipa macho, ianze kuona mlango ulio wazi kunifuata
kuanzia sasa.
Hazina za
fedha, hazina za uzima na afya, hazina
ya amani na furaha, hazina ya mali na utajiri.
Nakubariki
wewe na familia yako, kuanzia saa hii mpaka saa tatu usiku siku ya leo kila
atakayesoma hapa na kuamini maneno haya hataona njaa
Nawabariki
wote kwa jina la Yesu.
MCHUNGAJI LAURENT MPOMA
NCHI YA UKOMBOZI MINISTRY
(HEMA LA MAOMBI NA MAOMBEZI)
MWAJA KITOPE SINGIDA MJINI
+255714890889
WHATSAP: +255762756542
TUMA MAHITAJI YAKO KWA NAMBA HAPO
JUU.
UNAWEZA KUCHANGIA SADAKA YAKO KWA
AJILI YA UJENZI WA KANISA KATIKA VITU VIFUATAVYO:
1. VITI
20 @ 20,000/=
2. MAIKI
2= 150,000/=
3. ENEO
LA KANISA 500,000/=
4. SIKA
2 = 1900,000/=
5. VITAMBAA
VYA MADHABAHU.= 100,000/=
TIGO PESA: +255714890889................JINA: LAURENT MPOMA
M-PESA: +255762756542.....................JINA: LAURENT MPOMA
AIRTEL MONEY: +255782859946.........JINA: LAURENT MPOMA
MCHUNGAJI ATAKUOMBEA .
MUNGU AKUBARIKI SANA WEWE
UNAYECHANGIA KWA AJILI YA MUNGU NA AKUFUNGULIE MALANGO YAKO YA UCHUMI.
0 Comments