Follow us

MAMBO 10 YANAYOWEZA KUHARIBU UHUSIANOWETU NA MUNGU.

Tangazo

 


MAMBO 10 YANAYOWEZA KUHARIBU UHUSIANOWETU NA MUNGU.

1. Pesa

Watu huwawakitumia muda mwingi wakitafuta pesa kuliko kuutafuta USO wa Mungu, kwa kuombana kusoma biblia.

MATHAYO 6:19-34

Sina maanaya kwamba uache kazi au uache kutafuta pesa, Bali tumfanye Mungu kuwa wa muhimukuliko pesa.

2. Vyombo ya habari na Mitandao yaKijamii

Internet, Magaeti,Tv, simu n.k tunapaswa tutumie kwa kiasi. Tusipokuwa makini tutajikuta muda wote tunautumia kwa kuchat, mtu ataanzia facebook, anaenda Instagram, baadaye Twitter kisha Snapchat, WhatsApp, Telegram, IMO, Wechat, Palmchat n.k hadi anakuja kumaliza kutembelea mitandao hiyo yote tayari siku imepita.

Mwingineyeye ni kuangalia runinga tu, anatoka chaneli hili anaenda ile au unakuta yeyeni mtu wa kubadili CD tu na hizi season ndio zimewamaliza kabisaaa.

Hebu tuwe namuda maalum wa kuwa katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii pia.

3. Kanisa/Dini

Watu wengihuamini Dini kuliko kumwamini Yesu kristo aliye njia, kweli na uzima.

Nenda kanisani na uishi kwa kulifuata neno la Mungu na so mapokeo ya kanisa au Dini.

4. Mahusiano

Mahusiano yetu kati ya wazazi,ndugu,jamaa,wafadhili wetu, watoto,wafanyakazi wenzetu,wakuu wetu wa kazi, boyfriends/girlfriends ……hawa wote wanauwezo mkubwa wa kututenga au kupoza upendo wetu kati yetu na Mungu. Ni asili yetu wanadamu kuwa na Mahusiano, lakini tusiruhusu moja ya uhusiano huu kuwa kuwa na nguvu kuliko Mungu .

KUMBUKA:Mungu ametuagiza tupendane 1 YOHANA 3:11….Kwa hiyo tunapopendana,tunatimiza agizo la Mungu. Lazima tuhakikishe kwamba tunampa Mungu muda wa kutosha(ample time) kila siku.

Uhusiano wa girlfriends, boyfriends na wakuu  wetu wa kazi ni uhusiano hatari sana ambao una 100% za kutuweka mbali na Mungu wetu. Tuwe makini na wakuu wetu wa kazi na tusiwe na girlfriends au boyfriends kwani ni dhambi.

WAEFESO 5:3 “Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu wo wote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu;”

5. Ratiba(Routine)

Hakikishaunatenga muda wa kuwa na Mungu wetu.

Katika ratiba zetu lazima kuwepo na muda wa Kusoma neno na kuomba. Na mruhusu Mungu akuongoze.

6. Kazi zetu

Kazi zetu hutufanya kuwa mbali na Mungu. Kwa maana watu wengi huwa tunatumia muda mwingi kwa kazi na kumsahau Mungu. Wakati mwingine tunajikuta katika wakati mugumu tunapokuwa kazini. Tufanye kazi kwa bidii na tutenge muda wa kuwa na Mungu wetu pia.Tusiwe kama Martha Bali tuwe kama Mariam LUKA 10:38-42

7. Our hobbies

Our hobbies can consume a lot of time.

Hobby ni jambo alipendalo mtu.

Hobbies zetu hutuchukulia muda mwingi sana.

Tunapaswa tuwe na kiasi katika hobby . 2 TIMOTHEO 4:5Bali wewe, uwe na kiasi katika mambo yote, vumilia mabaya, fanya kazi ya mhubiri wa Injili, timiliza huduma yako.”

Pia kuna hobbies zingine ambazo moja kwa moja ziko kinyume na mapenzi ya Mungu. Hivyo tunapaswa kuziacha mara moja katika Jina la Yesu, sema Amen kama umeelewa.

8. Kuhitaji baraka za Mungu kuliko  Mungu mwenyewe

Tuutafute kwanza ufalme wa Mungu  na hayo mengine yaani baraka tutazidishiwa.

Tunapaswa tumtafute Mwenye vitu na siyo vitu. Tukimpata mwenye vitu tujue tumeshapata vitu.

MATHAYO 6:33“Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.”

 

9. Wachungaji wetu

Wachungajinao wanaweza kututenga na Mungu.

Wachungaji wengi huaminisha waumini kuwa wao Ndio wanajua kila kitu…….na sababu  hiyo husema hakuna haja ya kuhangaika kusoma Vitabu vya neno la Mungu tukiwa nyumbani.

Hebu fikirikwa MTU anayeenda kanisani mara moja kwa juma maana yake anailisha roho yakemara moja tu kwa siku saba.

Je, unaweza kuishi juma zima kwa kula mlo mmoja tu kwa siku zote hizo? Hapana haiwezekani. Kama haiwezekani vivyo hivyo kwa Roho zetu ni ngumu kuishi kwa mlo mmoja tu kwa juma lote.

Hata kama umezingwa na shughuli jitahidi kupangilia ratiba yako ili baada ya Nazi uwe na muda wa Kusoma Biblià na kuomba.

KUMBUKA: Siwajibu wa wachungaji kutulisha kila tunachohitaji Kiroho Bali ni Wajibu wetu.

10. Sisi wenyewe

Kwa asili tuwenye dhambi na tunapofuata asili yetu tuna kuwa mbali na Mungu.

Kwa sababu  hiyo nasi ni vyema tukaishi kwa kumfuata Mungu wala tusifuatishe matakwa ya miili yetu.(tamaa zetu wenyewe). Tujikane na tuishi ndani ya Kristo WARUMI7:15-21

TumruhusuMungu aichunguze na kuitengeneza mioyo yetu. ZABURI 139:23-24.


MUNGU AKUBARIKI SANA KUJIFUNZA MANENO YA MUNGU KUPITIA BLOG HII YA nchiyaukomboziministrytz.blogspot.com

 MCHUNGAJI LAURENT MPOMA

NCHI YA UKOMBOZI MINISTRY

(HEMA LA MAOMBI NA MAOMBEZI)

MWAJA KITOPE SINGIDA MJINI.

PIGA/TUMA MESEJI HAPA +255714890889

WHATSAP: +255762756542

UNAWEZA KUTUMA SADAKA YAKO KWA AJILI YA HUDUMA

TUNA UNUNUZI WA VIFAA VYA HUDUMA .

1. VITI 

2. SPIKA

3. VITAMBAA VYA MADHABAHU

4. UPANUZI WA KIWANJA CHA KANISA

KIASI CHOCHOTE TUNAPOKEA NA MUNGU ATAKUBARIKI.


KABLA HUJATUMA WASILIANA NA MCHUNGAJI KWA NAMBA HAPO JUU.

Post a Comment

0 Comments