Kutoka 23:32 ''Usifanye maagano
pamoja nao, wala pamoja na miungu yao.''
Agano ni
kitu kikubwa sana, Agana la kipepo ni mapatano ya kishetani, ni mikataba ya
kishetani na MUNGU hataki tuingie agano lolote na shetani wala mawakala wake.
#Kuna watu wanapitia mateso mengi
sana, wengine wamefungwa katika vifungo bila wao kujijuwa basi chukua muongozo
huu utakusaidia au itasaidia familia yako#.
Biblia inapozungumza
habari ya watu waliofungwa wapate kufunguliwa, hii ina maana ya kuwa kuna watu
wamefungwa chini ya utawala wa nguvu za giza katika ulimwengu wa Roho. Watu
hawa wamefungwa kwenye magereza na Ibilisi.
Isaya 57:8 '' Na nyuma ya milango na
miimo umeweka kumbukumbu lako; kwa maana umejifunua nafsi yako kwa ajili ya
mwingine, si kwa ajili yangu, ukakwea juu; umekipanua kitanda chako, nawe
umefanya maagano na hao; ulikipenda kitanda chao hapo ulipokiona. ''
Maagano mabaya ni jambo baya sana
ndugu. kama zamani
uliwahi kuingia maagano ya kishetani basi kimbilia kanisani ukaombewe maana
maagano ni mkataba na ukiingia mkataba na shetani mwishowe anaweza kukuangamiza
tu na uzima wa milele ukaukosa.
Tutambue ya
kuwa Yesu aliposema amekuja kutuokoa hii inamaanisha kwamba kuna mahali ambako
tusingeweza kujikwamua wenyewe bila nguvu yake yeye mwenywe kuingia kati yetu.
#Aliyahidhirisha haya kwenye kitabu
cha nabii Isaya 61:1-2 Roho ya Bwana Mungu i juu yangu kwa sababu Bwana
amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema, amenituma ili kuwaganga
waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za
kufunguliwa kwao”.
Vunja
uhusiano wako na hiyo miungu pamoja na kazi zake na agano lililofanyika kati ya
familia au ukoo wako na hiyo miungu. Kila unapotamka mwisho wake sema kwa
sababu nimesamehewa. Ipo mistari mingi ya kuvunja maagano lakini mimi nitakupa
kifungu hiki cha mstari katika kuvunja maagano na mapoozo ya aina yoyote. “Tena itakuwa katika siku hiyo mzigo wake
utaondoka begani mwako na nira yake shingoni mwako, nayo nira itaharibiwa kwa
sababu ya kutiwa mafuta” Isaya 10:27
Kifungu
kingine ambacho waweza tumia ni kwa kutaja maneno haya wakati wa kuvunja
vifungo ama laana “Bwana Yesu, nasimama mbele zako na katika ulimwengu wa roho,
kujiachanisha nafsi yangu (Taja jina lako) na vifungo vya kuzimu kwa upande wa
baba yangu na mama yangu kwa sababu nimesamehewa.” Endelea vivyo hivyo kwa
kutaja, roho na mwili kwa kutumia maneno hayo hayo uponyaji hufanyika katika
nafsi, mwili na roho.
Mtegemee Roho Mtakatifu kwa maana
atakufundisha mengi ikiwemo kuomba na maagizo ya Yesu. Na kwa kufuata maagizo
ya Yesu na kuenenda kwa roho hivyo vifungo vya nafsi vitakwisha. Soma Wagalatia
5:16-25, Luka 22:40-46.
Kudumu
katika maombi, kuenenda kiroho na kuepuka uovu ni muhimu kwa sababu kwa kufuata
misingi hiyo ndipo unafunguliwa vifungo kwa kuombewa ama kwa nguvu inayotenda
kazi ndani yako kupitioa roho mtakatifu. Lakini pia ni muhimu kujua ya kwamba
sala ya toba pekee haitoshi kumfungua mtu kama ana vifungo na sio imani tu bali
na juhudi binafsi ya mtu itasaidia katika kumuweka huru. Wapo watu wanaotaka
kupokea miujiza bila ya kuwa na mabadiliko yoyote, ama bila kusoma neno la
Mungu na kukua kiroho ama bila kuomba. Wao husubiria siku za maombi, ama mikesha
ama makongamano ya maombi ili waombewe kisha baada ya hapo hawajishughulishi
katika kukua kiimani.
Kuwa hodari katika Bwana ili upate
ulinzi wa Mungu. Waefeso 6:10-11 Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na
katika uweza wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za Mungu mpate kuweza kuzipinga
hila za shetani”
Maana ya
kuwa hodari katika Bwana ni kukaa kwenye maombi, kusoma na kulishika neno lake
liwe ndani yako, na kutaka kumjua yeye zaidi. Sikuzote Sali kwa bidii katika
kupambana na muovu shetani ndo mana tunaambiwa vaeni silaha zote za Mungu ili
kuweza kupingana na hila za muovu shetani.
MUNGU AKUBARIKI SANA
MAOMBI NA MAOMBEZI, WASILIANA NA
MCHUNGAJI LAURENT MPOMA
NCHI YA UKOMBOZI MINISTRY
(HEMA LA MAOMBI NA MAOMBEZI)
MWAJA KITOPE – SINGIDA MJINI BARABARA
YA KENDA MWANKOKO.
PIGA/ TUMA MESEJI +255714890889
WHATSAP: +255762756542
YOUTUBE: youtube.com/channel/UCjXjSSDOweHXL3YE5edBNIg
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
SOMA: 2 Nya 1:7-12. Usiku ule Mungu
akamtokea Sulemani, akamwambia, Omba utakalo nikupe. Sulemani akamwambia Mungu,
Umemfanyia baba yangu Daudi fadhili kuu, nawe umenimilikisha mimi badala yake.
Basi sasa, Ee BWANA Mungu, na limyakinie baba yangu Daudi neno lako; maana
umenitawaza niwe mfalme juu ya watu wengi kama mavumbi ya nchi. Basi sasa nipe
hekima na maarifa, nijue kutoka na kuingia mbele ya watu hawa; kwa kuwa ni nani
awezaye kuwahukumu watu wako hawa walio wengi? Naye Mungu akamwambia Sulemani,
Kwa sababu neno hili lilikuwamo moyoni mwako, wala hukujitakia mali, wala
utajiri, wala utukufu, wala maisha za wakuchukiao, wala hukujitakia maisha ya
siku nyingi; bali umejitakia hekima na maarifa, upate kuwahukumu watu wangu,
niliokutawaza juu yao; basi hekima na maarifa umepewa; nami nitakupa mali, na
utajiri, na utukufu, kupita walivyokuwa navyo wafalme wote waliokuwa kabla
yako, wala baada yako hapatakuwa na mtu atakayekuwa navyo.
TUNAUNUNUZI WA VITU
KWA AJILI YA KANISA NA KUUJENGA MWILI WA KRISTO.
1. VITI 20 @20000/=
2. KIWANJA CHA KANISA 2,000,000/=
3. VITAMBAA VYA MADHABAHU 80,000/=
MUNGU AKUBARIKI SANA
KWA KUCHANGIA .
MCHUNGAJI LAURENT
MPOMA ATAKUOMBEA NA MUNGU WA MBINGUNI ATAKUGUSA NA KUKUFUNGUA.
AMINAAAA SANAA

0 Comments