Follow us

SOMO:KUMPENDA MUNGU HAKUKO MDOMONI BALI NI KWA KUISHI MAISHA MATAKATIFU

Tangazo

 

Bwana Yesu asifiwe wana wa Mungu ni siku njema tena Bwana ametupa kwa neema yake.Hivyo hatuna budi kurudisha heshima na utukufu kwake.

Pale unaposema unampenda Mungu halafu uishi maisha yanayompendeza ni kosa kubwa sana.Watu wengi wakiulizwa unampenda Mungu kila mtu.atajibu ndio na wala hakuna atakayesema hapana ata yule mpagani.Mtu Mungu siku ya leo Bwana analo neno Juu yako usiseme unampenda Mungu wakati maisha unayoishi yanamtukuza Shetani uwe na uhakika Jehanamu itakumeza.

MATHAYO 15:8"WATU HAWA UNIHESHIMU KWA MIDOMO ILA MIOYO YAO IKO MBALI NAMI"

Nyakati za leo watu  humpenda Mungu kwa midomo yao ila maisha yao hayako kwa Mungu.uwenda nasema na wewe unayesoma ujumbe huu unasema unampenda Mungu wakati wewe ni mzinzi/muasherati, unasema unampenda Mungu wakati wewe ni msengenyani,unasema unampenda Mungu wakati hutoi fungu la kumi, unasema unampenda Mungu wakati wewe ni mwizi, unasema unampenda Mungu wakati wewe ni Muongo, unasema unampenda Mungu wakati husaidii wenye shida ,unasema unampenda Mungu wakati wewe mtukanaji, mtu wa Mungu nataka nikwambie kusema kwako unampenda Mungu halafu njia zako ni ovu uwe na uhakika Jehanamu utaenda kama usipo tubu leo na kuacha Maovu yako.

Kumpenda Mungu si swala kusema kutoka mdomoni tu bali la kupasa upendo huo utoke kutoka moyoni mwako.Kama vile  Mungu alivyo upenda ulimwengu huu hata akamtoa mwanaye wa pekee ili ulimwengu ukombolewe nɗivyo ivyo yatupasa nasi kumpenda Mungu .

YOHANA 14:15"MKINIPENDA MTAZISHIKA AMRI ZANGU

Tunaona hapo wana wa Mungu kumbe ukimpenda Mungu lazima uzishike amri zake ,uwezi kusema unampenda Baba ako halafu anakuagiza jambo unaenda kinyume na alivyosema ,amua leo mtu wa Mungu kujitenga na mambo ambayo yanakufanya usimpende Mungu toka moyoni mwako kwani itakuwa ni hasara kubwa watu wanajua unampenda Mungu mwisho ukajulikani ulikuwa humpendi hakika itakuwa ni aibu kubwa sana.

Ni muda wa kujitathimin kweli unampenda Mungu au unasema tu ila matendo yako kinyume na maneno yako.

MITHALI 8:17"NA WAPENDA WALE WANIPENDAO NA WALE WANITAFUTAO KWA BIDII WATANIONA"

Mungu anasema nawapenda wale wanipendao na ikiwa watanitafuta kwa bidii wataniona, uwezi kusema unampenda Mungu wakati huna Muda kusoma neno lake, uwezi kusema unampenɗa Mungu wakati huna Muda wa kuomba ,hapo uwezi sema unampenda wakati huna wasaa wa kumtafuta.Mtu Mungu amua leo kumpenda Mungu kwa moyo wako wote.

Post a Comment

0 Comments