MAOMBI YA
KUMTEKETEZA SHETANI “NGUVU ZA GIZA”
Kuna watu
wanapitia mateso mengi sana, wengine wamefungwa katika vifungo bila wao kujijuwa
basi chukua muongozo huu utakusaidia au itasaidia familia yako.
Biblia
inapozungumza habari ya watu waliofungwa wapate kufunguliwa, hii ina maana ya
kuwa kuna watu wamefungwa chini ya utawala wa nguvu za giza katika ulimwengu wa
Roho. Watu hawa wamefungwa kwenye magereza na Ibilisi.
Tutambue ya
kuwa Yesu aliposema amekuja kutuokoa hii inamaanisha kwamba kuna mahali ambako
tusingeweza kujikwamua wenyewe bila nguvu yake yeye mwenywe kuingia kati yetu.
MAOMBI YA
KUMTEKETEZA SHETANI:
Baba katika
Jina la Yesu:
1.
Ninayaharibu na kuyateketeza mamlaka yote aliyopewa shetani na mababu/ mababa,
ndugu zangu katika Jina la Yesu.
2. Nina
zilaani na kuziteketeza kwa damu ya Yesu roho zote zinazoendelea kutilia mkazo
hayo maagano katika maisha yangu na naziteketeza na kuzivunavunja kwa Jina la
Yesu.
3. Kitu
chochote kilichoingizwa kwenye maisha yangu,kwa mkono wa kipepo, au majini
ninakiamuru kiachie kwa JIna la Yesu.
4. Kila aina
ya sumu iliyopenyezwa kwenye maisha yangu nina iamuru itoke nje sasa, katika
jina la Yesu, nina sukuma nje kwa damu ya Yesu.
5. Ee Bwana
Yesu, shusha moto juu ya kila roho ya mauti na kuzimu, iliyoandaliwa kwa ajili
yangu, katika jina la Yesu
6. Nina
ponda kichwa na kukanyaga kila mkia wa majoka ya kiroho, katika jina la Yesu
7. Upanga wa
moto, na uanze kukata kila kifungo walichokifunga wazazi, katika jina la Yesu
8. Ee Bwana,
nifunulie agano lolote la siri ambalo shetani amefunga na nafsi yangu au
anataka kufunga na nafsi yangu, katika jina la Yesu.
9. Kila
pando,ambalo baba yangu wa mbinguni hakulipanda katika maisha yangu, nina
kungo’a katika jina la Yesu.
10. Baba
nina pitisha umeme katika ardhi ya mahali hapa sasa na kila agano na miguu
yangu lianze kuvunjika sasa katika jina la Yesu.
11. Agano lolote
la siri ambalo ni la uovu, ninakuvunja katika jina la Yesu
12. Nina
nyunyiza damu ya Yesu kuvunja laana zote
13. Imba
wimbo huu kama unaweza, kama huwezi usilazimshe: Kuna nguvu ya ajabu, damuni
mwa Yesu
14. Nina
nyunyiza damu ya Yesu kuvunja laana zote za dhambi za wazazi wangu
15. Ee
Bwana, badili laana zote zilizoelekezwa kwangu kuwa Baraka
16. Kila
nguvu ya uovu iliyoelekezwa kwangu, ninakuamuru kurudi moja kwa moja, kwa
mtumaji katika jina la Yesu.
17. Ee Bwana
Mungu, ninaomba kila alichosema adui kwamba hakitawezekana katika maisha yangu,
kikawezekane sasa kwa jina la Yesu.
18. Nina
jiondoa na kujitenganisha katika kambi yoyote ya mateka inayomilikiwa na
adui,katika jina la Yesu.
19. Nina
jifungua na kujiondoa kutoka kwenye kila kifungo cha kurithi ,katika jina la
Yesu.
20. Ee
Bwana,tuma shoka lako la moto kwenye misingi ya maisha yangu na uharibu/ulikate
kila pando ambalo amelipanda adui katika jina la Yesu.
21. Nina
ipitisha Damu ya Yesu, katika mifumo yote ya mwili wangu [mfumo wa damu, wa
fahamu, wa chakula, wa upumuaji, wa takamwili n.k] na kuisafisha mabaki yote ya
urithi wa vitu viovu katika jina la Yesu.
22. Damu ya
Yesu na moto wa Roho mtakatifu,unisafishe kila kiungo cha mwili wangu [Figo,
moyo, mapafu, macho, masikio, n.k] katika jina la Yesu
23. Nina
vunja mikataba yote ya kiukoo na kikabila inayonihusisha mimi katika jina la
Yesu.
24. Nina
jiondo/ninajivua/vunja laana zote za kikabila na kiukoo katika jina la Yesu
25. Nina
tapika chakula chochote cha uovu nilicholishwa katika maisha yangu, katika jina
la Yesu
26. Mapepo,
majini, mizimu na wachawi manao fuatilia maisha yangu,na mpararaizi[mpooze]
sasa katika jina la Yesu.
27.
Shambulio lolote lilopangwa juu ya familia yangu, ninalibatilisha kwa ajili
yangu katika jina la Yesu
28. Nina
vunja matoke mabaya yote kwa ajili ya jina la kiuovu, lilipachikwa kwenye nafsi
yangu katika jina la Yesu
29. Nina
batilisha laana zote, mikosi, majanga, ajali, maradhi yote yaliyoelekezwa
kwenye maisha yangu katika jina la Yesu.
30. Muombe
Mungu aondoe laana zote alizo ziachilia kwenye maisha yako kwa sababu ya
kutotii neon lake[kumb 28:]
31. Pepo
lolote lililo jipachika kwenye laana yoyote inayonihusu mimi, toka, katika jina
la Yesu
32. Laana
zote katika maisha yangu, badilika na kuwa Baraka, katika jina la Yesu
33.
Utakapokuwa unataja laana zilizoorodheshwa hapo chini, sema kwa kumaanisha
“vunjika, vunjika, vunjika” katika jina la Yesu. Nina jitenganisha na nyinyi
katika jina la Yesu.
• Laana zote
za udhaifu wa kiakili na kimwili
• Laana zote
za kushidwa katika kila ninalofanya
• Laana zote
za umaskini
• Laana zote
za kuvunjika kwa familia
• Laana zote
za kuonewa na kudharauliwa
• Laana zote
za Uharibifu wa mtu binafsi,kama vile kujinyonga n.k
• Laana zote
za magonjwa sugu
• Laana zote
za kishirikina
• Laana zote
za kuharibikiwa mambo ya uzazi na viungo vya uzazi
• Laana zote
za kufanya kazi kwa bidii pasipo kuiona faida
• Laana zote
za kulowea mambo ya uovu kama vile zinaa, pombe, sigara n.k
34. Jitamkie
maneno ya Baraka wewe mwenyewe, kwa mfano kwa kusema “hakutakuwa na umaskini
tena, magonjwa tena n.k katika maisha yangu katika jina la Yesu.
35. Nina
jifungua na kujitenganisha na vifungo vya madhabahu zote za giza katika jina la
Yesu.Sema mara kadhaa ukifuatiwa na maneno yafuatayo “nina jitenganisha” katika
jina la Yesu.Tumia muda kidogo kwenye hilo.
36. Nina
tapika sumu zote za mashetani nilizozimeza katika jina la Yesu.
37.[Weka
mikono yako juu ya kichwa chako] Nina vunja kila mamlaka za giza katika maisha
yangu, katika jina la Yesu.Rudia “nina vunja katika jina la Yesu.
38. Taja
mambo yafuatayo kwa mamlaka na sema “vunjika kwa jina la Yesu.
• Mamlaka
zote za mizimu na miungu ya familia, ukoo, na kabila
• Mamlaka
zote za roho za kichawi zilzopo ndani ya familia, ukoo, kabila
• Mamalaka
zote zilizoshika rimoti za kudhibiti familia, ukoo, kabila
• Mamlaka
zote ovu ndani ya Familia, ukoo, kabila nk
39. Kila
mmiliki wa mzigo niliobebeshwa beba mzigo wako katika jina la Yesu[Mzigo
unaweza kuwa ugonjwa,mikosi wabebeshe wamilki]
40. Nina
zipoodhesha/nina zipararaizi madhabahu zote za giza katika jina la Yesu
41. Nina
zilaani madhabahu zote za uovu zilizoelekezwa zidi yangu katika jina la Yesu
42. Nina
agiza nyundo ya Mungu aliyeumba mbingu na nchi,iponde kila madhabahu ya giza
zilizoelekezwa kwenye maisha yangu katika jina la Yesu.
43. Ee Bwana
tuma moto wako na uteketeze madhabahu zote za giza zinazoinuka dhidi ya maisha
yangu,
44. Makuhani
wote wa madhabahu zote za giza wanaocheza na maisha yangu,wakutane na upanga wa
roho mtakatifu. Katika jina la Yesu.
45. Mkono
wowote unaotaka kunikamata na kuniteka kwa ajili ya Maombi haya ninayoomba
kauka katika jina la Yesu.
46. Nina
waamuru makuhani wa madhabahu za giza kunyweni damu wenyewe katika jina la Yesu
47. Nina
rudisha urithi wangu ulioibiwa na madhabahu za giza katika jina la Yesu.
48.
Ninafuta/ninaliondoa jina langu kwenye madhabahu za giza katika jina la Yesu
49. [Weka
mkono wako mmoja kifuani] Ninaziondoa Baraka zangu kwenye madhabahu za giza
katika jina la Yesu
50. [Weka
mkono mmoja kifuani na mwingine kichwani] Ninaondoa kitu chochote kile
kinachoniwakilisha mimi [kama vile nguo] kwenye madhabahu za giza katika jina
la Yesu.
51. [Taja
kiungo chochote katika mwili wako ambacho akifanyi kazi ipasavyo au kama ni
mwili wote taja mwili] na useme maneno yafuatayo “nina kuondoa kwenye madhabahu
za giza” katika jina la Yesu. Tamka hivyo mara saba.
52. Nina
jitenganisha kutoka kwenye maagano yote ya damu na nguvu za giza katika jina la
Yesu
53. Damu ya
Yesu na unene kwa ajili yangu dhidi ya maagano yote na nguvu za giza
54. Nina
tamka Uharibifu dhidi ya roho chafu zote katika maisha yangu.Katika Jina la
Yesu.
55. Nina
jitenganisha na laana zote za maagano katika jina la Yesu
56. Nina
jitenganisha mimi na familia yangu kutoka katika kila agano la damu katika jina
la Yesu.
57.
Ninajitenganisha na kila agano la damu la kurithi katika jina la Yesu.
58. Nina
iondoa damu yangu kwenye madhabahu za giza katika jina la Yesu
59. Nina
iondoa damu yangu kutoka kwenye benki za damu kwenye ulimwengu wa giza katika
jina la Yesu
60. Nina
vunja kila agano la damu la kutokukusudia kwa jina la Yesu
61.Ee bwana,
damu ya mnyama yeyote iliyomwagika kwa niaba yangu, Naipoteze nguvu ya agano
sasa, kwa jina la Yesu
62. Kila
tone la damu linalotamka mabaya dhidi yangu, na ikae kimya sasa, kwa damu ya
Yesu
63.
Ninajifungua na kujiondoa kutoka kwenye kila agano la damu la kifamila, kiukoo,
kabila katika jina la Yesu.
64. Nina
jitenganisha na kila agano la damu nililoingia kwa kujua au kutojua kwa jina la
Yesu
65. Ee Bwana
kila agano la damuna nguvu za giza lipoteze nguvu na uhalali wake juu yangu
katika jina la Yesu.
66. Damu ya
agano jipya la Bwana na Mwokozi wangu Yesu Kristo, naiikemee damu ya agano na
nguvu za giza ilijipanga kinyume name. Kwa jina la Yesu
67. Nimepewa
mamlaka ya kubatilisha haki zote zilizopo kwenye maagano yote ya damu na nguvu
za giza . kwa jina la Yesu.
68.Agano
lolote la damu na nguvu za giza lililofungwa kwenye kiungo chochote kwenye
mwili wangu, nalivunjike sasa.Kwa jina la Yesu
69.
Ninapokea vitu vyote vilivyoibiwa au kuchukuliwa na adui kupitia maagano na
nguvu za giza. Kwa jina la Yesu.
70. Nina
vunja agano lolote la damu na nguvu za giza kwenye damu yangu . Kwa jina la
Yesu AMEN.
BAADA YA KUFANYA HAYO MAOMBI, SASA
ENDELEA KUSOMA UJUMBE WA MUNGU KWAKO:
Mtegemee
Roho Mtakatifu kwa maana atakufundisha mengi ikiwemo kuomba na maagizo ya Yesu.
Na kwa kufuata maagizo ya Yesu na kuenenda kwa roho hivyo vifungo vya nafsi
vitakwisha. Soma Wagalatia 5:16-25, Luka 22:40-46. Kudumu katika maombi,
kuenenda kiroho na kuepuka uovu ni muhimu kwa sababu kwa kufuata misingi hiyo
ndipo unafunguliwa vifungo kwa kuombewa ama kwa nguvu inayotenda kazi ndani
yako kupitioa roho mtakatifu. Lakini pia ni muhimu kujua ya kwamba sala ya toba
pekee haitoshi kumfungua mtu kama ana vifungo na sio imani tu bali na juhudi
binafsi ya mtu itasaidia katika kumuweka huru. Wapo watu wanaotaka kupokea
miujiza bila ya kuwa na mabadiliko yoyote, ama bila kusoma neno la Mungu na
kukua kiroho ama bila kuomba. Wao husubiria siku za maombi, ama mikesha ama
makongamano ya maombi ili waombewe kisha baada ya hapo hawajishughulishi katika
kukua kiimani.
Kuwa hodari
katika Bwana ili upate ulinzi wa Mungu. Waefeso 6:10-11 Hatimaye, mzidi kuwa
hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za Mungu
mpate kuweza kuzipinga hila za shetani”
Maana ya
kuwa hodari katika Bwana ni kukaa kwenye maombi, kusoma na kulishika neno lake
liwe ndani yako, na kutaka kumjua yeye zaidi. Sikuzote Sali kwa bidii katika
kupambana na muovu shetani ndo mana tunaambiwa vaeni silaha zote za Mungu ili
kuweza kupingana na hila za muovu shetani.
Mungu
akubariki sana
MAOMBI NA MAOMBEZI
PIGA: 0714890889
WHATSAP: 0762756542

0 Comments