MAOMBI YA KUFUTA MANENO MABAYA ULIYONENEWA JUU YAKO
Bwana Yesu asifiwe?
MITHALI 18:21
"Kifo na uzima viko katika nguvu za ulimi.Naye anayeupenda kuutumia atakula matunda yake"
Kabla ya maombi haya hakikisha umeomba msamaha kwa mtu yeyote uliyemkosea na pia kusamehe mtu yeyote aliyekukosea.
Mungu mwenyewe ni msamaha na atakusamehea tu kama nawe utasamehea wabaya wako.
usipotoshwe na mtu yeyote akakwambia kuwa maombi ya mtu aliyeokoka yatajibiwa sawasawa na ya mtu anayemkataa Yesu,huo ni uongo mtupu;kwani maombi ya mwokovu husikizwa sana na Mungu.
Huu ni mwelekeo tu wa kufuta maneno mabaya ulonenewa na wakwendeaye kinyume.
Maombi.
" Baba wa mbinguni katika Jina la Yesu Kristo nakushukuru kwa wema na wokovu ulionipa mimi mwanao.
Asante kwa kunipa ufunuo wa kuyajua haya ambayo yamekuwa vikwazo vya kubarikiwa kwangu.
Nisamehe dhambi na makosa niliyokutenda na niliyowatenda wanadamu.
Isaya 1:18 unasema hata dhambi zangu ziwe nyekundu utanisafisha na kunisamehea.Baba wa mbinguni nisamehe.
Ninafuta kila neno mbaya nililonenewa na wabaya wangu,nikanenewa na wachawi wakasema sitabarikiwa.Nalifuta neno hilo kwa damu ya Yesu Kristo katika Jina la Yesu kristo na ninabadilisha laana yao na kuwa baraka kwangu katika Jina la Yesu.
Kila neno ovu la kunifunga lililotamkwa kwa kazi yangu nalifuta kwa damu ya Yesu Kristo.
Aliyeninenea kushindwa nimelifuta neno hilo na kuandika kushinda katika maisha yangu katika Jina la Yesu Kristo.
Kila neno la kinywa la kushindwa nililojitamkia mwenyewe nalifuta kwa damu ya Yesu Kristo.
Kila laana niliyotamkiwa na wanadamu naifuta na kuitamka baraka kuanzia sasa katika Jina la Yesu Kristo.
Kila neno la kufunga ndoa yangu,mume wangu,mke wangu,boma letu,utajiri wetu ninalifuta na kuandika baraka katika Jina la Yesu Kristo.
MUNGU WA MBINGUNI AKUBARIKI SANA
KWA MAHITAJI AU MAOMBI NA MAOMBEZI
PIGA: +255714890889
0 Comments