NJIA YA KWANZA NI ELIMU: ni muhimu sana watu kuwa na elimu katika ulimwengu wa leo kwa sababu mambo hayawezi kufanikiwa pasipo maarifa. Elimu inaweza kukutoa sehemu moja hadi nyingine. Kila jambo linahitaji elimu na elimu si ya shuleni tu bali elimu hupatikana popote pale ulipo; kwa mfano umemuona dada fulani kafunga kilemba chake vizuri na wewe unafunga kama yeye, watu wakikuona wanasema ‘mama fulani leo umetokelezea hatariii, hongera’ kumbe umeigilizia, ulipata elimu ya kufunga kilemba kutoka kwa dada yule.
Ukisoma
Mithali 15:14 inasema “Moyo wa mwenye
ufahamu hutafuta maarifa” kumbe tunapaswa kuyatafuta maarifa ili tuwe na
ufahamu na tuweze kufanikiwa kwa jambo
fulani. Mtu mwenye maarifa ya jambo fulani uwezo wake wa kufanikiwa huwa ni
mkubwa sana.
Mithali 24:5
“…mtu wa maarifa huongeza uwezo; Elimu inaweza kukufanya ukaketi kwa wakuu.
Danieli 1:3-6 “Mfalme akamwambia Ashpenazi, mkuu wa matowashi wake, awalete
baadhi ya wana wa Israeli, wa uzao wa kifalme, na wa uzao wa kiungwana; vijana
wasio na mawaa, wazuri wa uso, wajuzi wa hekima, werevu kwa sababu ya maarifa
yao, wenye kufahamu elimu, watakaoweza kusimama katika jumba la mfalme; tena
alimwambia awafundishe elimu ya Wakaldayo, na lugha yao.Huyo mfalme akawaagizia
posho ya chakula cha mfalme, na ya divai aliyokunywa, akaagiza walishwe hivyo
muda wa miaka mitatu; ili kwamba hatimaye wasimame mbele ya mfalme.”
NJIA YA PILI NI WATU: Mungu anaweza kutumia watu ili
kutufanikishia mambo yetu. Watu wanaweza kukusaidia kwa kukupa hiki au kile ili
ufikie malengo yako. Inaweza ikawa ni kukusomesha, kukupa mtaji, kukutafutia
kazi au hiki au kile.
NJIA YA TATU NI MKONO WA MUNGU
MWENYEWE: mkono wa
Mungu unapotaka kutenda hauchagui wenye elimu au wasio na elimu. Mkono wa Mungu
hauhitaji refarii wa kukupigia debe ili upate kazi au uolewe. Mkono wa Mungu
mwenyewe unapotenda jambo huwa hauchanganywi na kitu chochote. Mungu ni Mungu
mwenye wivu hivyo anapotaka kutenda huwa natenda mwenyewe ili zile sifa na utukufu
usiwe wa kugawana kwa wanadamu na Yeye, Yeye hutaka sifa zote ziwe zake. Mkono
wa Mungu mwenyewe unamtambua na kumtumia mtu yeyote yule bila kujali elimu
yake. Petro na Yohana hawakuwa na elimu kubwa ya darasani lakini walichapa kazi
ya Mungu na ikasonga mbele. Mkono wa Mungu unamtambua na kumtumia yeyeto yule
sawa na Mungu apendavyo. Mungu akimgusa mtu aje kukuoa hautasumbuliwa katika
ndoa, fahamu wanadamu wanakupa mke/mme lakini hawakusaidii kuishi naye bali
Mungu anakupa mke/mme na anakupa akili ya kuishi naye. Mungu akitenda
jambo akili ya kibinadamu haitafasri.
Unaweza
ukafanikiwa kwa njia ya elimu au watu lakini njia hizi huwa zina kasoro. Watu
wakitusaidia kupata mafanikio watataka kurudishiwa shukurani na kama hautafanya
hivyo tayari ni kosa kwa watu hao.
Mungu
hafanyi kwa sababu umeomba bali Mungu
hufanya kwa sababu unatembea vizuri na Mungu, kwa sababu unauhusiano mzuri na
Mungu.
Kwa Hana na
Sarai njia ya elimu na watu zilishindwa kuwasaidia ili wapate watoto lakini
Mkono wa Mungu mwenyewe uliwagusa wakapata watoto katika jina la Yesu.
Tunamwamini Mungu asiyezuiwa na mazingira, utasa wa Hana haukumzuia Mungu
kumpatia Hana mtoto, utasa na ubibi kizee wa Sara haukumzuia Mungu kumpatia
Sara mtoto. Mungu akitaka kufanya jambo hazuiwi na kitu chochote.
0 Comments