MAOMBI YA
KUMILIKI MILANGO YA BARAKA ALIYOIKAMATA SHETANI
BWANA YESU
ASIFIWE!
Isaya 60:11
'' Malango yako nayo yatakuwa wazi daima; Hayatafungwa mchana wala usiku; Ili
watu wapate kukuletea utajiri wa mataifa, Na wafalme wao wakiongozwa pamoja
nao.''
Katika
ulimwengu wa roho baraka zako zote huwa ziko katika maeneo ambapo ili upate
baraka yako uitakayo unatakiwa kubisha kwenye ulimwengu wa roho wa nuru ili
ufunguliwe na kuchukua baraka yako, ndio maana katika maombi imani ni jambo la
muhimu sana.
Kuna
baraka nyingi sana ambazo unazihitaji katika maisha yako.
Kuwa na afya
njema ni baraka, kuna na mchumba kisha ndoa ni baraka, kufaulu masomo ni
baraka, kuwa na ufahamu mzuri ni baraka, kumiliki nyumba au kiwanja ni baraka,
kupata kazi nzuri ni baraka , Kununua gari ni baraka, kupandishwa cheo kazini
ni baraka na hata kuwa na uchumi mzuri ni baraka, N.k maana baraka ziko nyingi
sana.
BWANA
YESU siku moja akatoa siri ya ushindi katika maombi akisema;
‘’7 Ombeni,
nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa; kwa maana
kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa. Au kuna
mtu yupi kwenu, ambaye, mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe? Au akiomba
samaki, atampa nyoka? Basi ikiwa ninyi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu
vipawa vyema, je! Si zaidi sana BABA yenu aliye mbinguni atawapa mema wao
wamwombao? -Mathayo 7:7-11‘’
Kuna kuomba,
kuna kutafuta kwa njia ya maombi na kuna kuomba kufunguliwa mlango kwa njia ya
maombi, ndio kubisha huko.
Kama kuna
kubisha basi kuna mlango pia maana huwezi kugonga hodi ukutani na ukuta
ukafunguka bali utagonga hodi mlangoni na mlango utafunguliwa.
Baraka mfano wake ni kama kiti ambacho kipo ndani ya
nyumba na wewe uko nje umesimama huku unatamani kukaa maana umechoka kusimama.
Kama utataka kukikalia kile kitu ambacho kiko ndani inakubidi kufungua mlango
na kuingia ndani na kukichukua kisha unatoka nje na kukiweka chini kiti hicho
na unakaa kwa furaha zako.
Nyumba hiyo
ni ulimwengu wa roho na kiti ni baraka yako. Sasa ili uchukue kiti na kukikalia
inakubidi kwanza uuone malango kisha kama mlangoni kuna adui basi hakikisha
unamuondoa adui huyo kwa maombi ya vita kupitia jina la YESU KRISTO. Kisha
baada ya kumuondoa adui huyo unafungua mlango kwa maombi kwa imani katika jina
la YESU KRISTO. Baada ya kufungua mlango unaingia ndani kwa maombi ya imani kwa
jina la YESU KRISTO na unachukua baraka yako na kutoka nje ndipo katika
ulimwengu wa mwili itaonekana baraka hiyo na
utaanza kuitumia baraka yako hiyo. Kama ni mume wako ukimfungua kwa
maombi katika ulimwengu wa roho ndipo utaona anabadilika katika ulimwengu wa
mwili na kuwa mtu mzuri tu bila kukusaliti tena.
Kama
umefungua kamba zilizikuwa zimemnasa mchumba wako baada ya maombi utamuona
mchumba wako katika ulimwengu wa mwili na utaona akianza mikakati ya posa au
mikakati ya ndoa. Ila ni lazima kwanza ushinde katika ulimwengu wa roho ndipo
utaona ushindi katika ulimwengu wa mwili.
Ukiona mtu
ni askofu ni kwa sababu alianza kuwa askofu kwanza katika ulimwengu wa roho
ndipo akaja kuwa askofu katika ulimwengu wa mwili.
Ukimuona mtu
ni rais au waziri ni kwa sababu alianza kuwa waziri kwanza katika ulimwengu wa
roho ndipo akaja kuwa waziri katika ulimwengu wa mwili.
Ukiona ndoa
ina furaha ni kwa sababu kwanza walishinda katika ulimwengu wa roho ndipo
wakaja kuona ushindi katika ulimwengu wa mwili.
Kila jambo
huanzia kwenye ulimwengu wa roho ndipo linakuja kutokea katika ulimwengu wa
mwili.
MUNGU
hukujulisha sana kwa njia ya ndoa na maono kile kinachoendelea katika ulimwengu
wa roho ili kwa maombi yako kama ni kizuri ukimiliki katika ulimwengu wa mwili
na kama ni kibaya ukiharibu katika ulimwengu wa roho ili kisije kutokea katika
ulimwengu wa mwili.
Mtu mmoja
alikuwa anaota ndoto mara kwa mara akiwaongoza watu wengi na kuwapangia
majukumu. Wakati anaota ndoto hizi alikuwa ni maskini wa kutupwa katika familia
yao na hakukuwa na uwezekano wa yeye kuja kuwa kiongozi mkubwa katika taifa.
Lakini kwa uaminifu kwa MUNGU na kukaa kwenye kusudi lake MUNGU alikuja kuwa kiongozi mkubwa katika taifa.
Yusufu
katika Biblia aliona ndugu zake wakimwinamia na aliona akiwa kiongozi mkubwa na
jambo hilo likaja kutokea maana mambo yote huanzia katika ulimwengu wa roho
kabla ya kuja kutokea katika ulimwengu wa mwili.
Mwanzo
36:5-11 ''5 Yusufu akaota ndoto, akawapa ndugu zake habari, nao wakazidi
kumchukia; akawaambia, Tafadhalini, sikieni ndoto hii niliyoiota. Tazama, sisi
tulikuwa tukifunga miganda shambani, kumbe! Mganda wangu ukaondoka ukasimama,
na tazama, miganda yenu ikazunguka ikainama mbele ya mganda wangu. Ndugu zake
wakamwambia, Je! Kweli wewe utatumiliki sisi? Nawe utatutawala sisi? Wakazidi
kumchukia kwa ajili ya ndoto yake, na kwa maneno yake. Akaota tena ndoto
nyingine, akawaambia ndugu zake, akasema, Angalieni, nimeota ndoto nyingine; na
tazama, jua na mwezi na nyota kumi na moja zikaniinamia.Akawaambia baba yake na
ndugu zake; baba yake akamkemea akamwambia, Ni ndoto gani hii uliyoiota? Je!
Mimi na mama yako na ndugu zako tutakuja tukusujudie hata nchi?Ndugu zake
wakamhusudu; bali baba yake akalihifadhi neno hili. ''
Hapo ni
mfano mmoja tu katika mifano nyingi ambayo inathibitisha kwa kila jambo
linalotokea katika maisha ya mtu limeanzia katika ulimwengu wa roho kabla ya
kuja kuonekana katika ulimwengu wa mwili.
Yusufu
alianza kuwa kiongozi mkubwa katika ulimwengu wa roho ndipo miaka ya baadae
akaja kuja kuwa kiongozi mkubwa yaani akaja kuwa waziri mkuu katika taifa la
ugenini na wale ndugu zake waliomwinamia
ndotoni ndio hao hao walikuja kumwinamia katika ulimwengu wa mwili.
Mwanzo
41:38-44 '' Farao akawaambia watumwa wake, Tupate wapi mtu kama huyu, mwenye
roho ya MUNGU ndani yake? Farao akamwambia Yusufu, Kwa kuwa MUNGU
amekufahamisha hayo yote, hapana mwenye akili na hekima kama wewe. Basi wewe
utakuwa juu ya nyumba yangu, na kwa neno lako watu wangu watatawaliwa. Katika
kiti cha enzi tu nitakuwa mkuu kuliko wewe.Farao akamwambia Yusufu, Tazama,
nimekuweka juu ya nchi yote ya Misri. Farao akavua pete yake ya muhuri mkononi
mwake, akaitia mkononi mwa Yusufu; akamvika mavazi ya kitani nzuri, na kumtia
mkufu wa dhahabu shingoni mwake. Akampandisha katika gari lake la pili
alilokuwa nalo. Na watu wakapiga kelele mbele yake, Pigeni magoti. Hivyo
akamweka juu ya nchi yote ya Misri.Farao akamwambia Yusufu, Mimi ni Farao, na
bila amri yako, mtu asiinue mkono wala mguu katika nchi yote ya Misri.''
Miaka mingi
baade Yusufu aliwaona ndugu zake na akazikumbuka zile ndoto maana kila jambo
huanzia katika ulimwengu wa roho ndipo linakuja kutokea katika ulimwengu wa
mwili.
Mwanzo
42:8-9 ''Yusufu akawatambua nduguze, bali wao hawakumtambua yeye.Yusufu
akazikumbuka zile ndoto alizowaotea. Akawaambia, Wapelelezi ninyi, mmekuja ili
mwuone utupu wa nchi. ''
Kwa Yusufu
haikuishia hapo tu kupewa cheo kikubwa katika taifa la ugenini bali hata ndugu
zake wale aliowaona katika ndoto zamani na wao walikuja kumwinamia kama alivyoona katika ndoto
zamani(Mwanzo:43:28)
Ndugu yangu
naomba ujue kwamba vitu vyote vinavyokutokea katika ulimwengu wa mwili ni kwa
sababu vilianza katika ulimwengu wa roho.
Unaweza
kutaka kununua kiwanja katika eneo fulani lakini katika ulimwengu wa roho
ukaona vita kubwa, unatakiwa umpige kwanza kwa jina la YESU mkuu wa kipepo
aliyelishikilia eneo hilo, limiliki kwanza katika ulimwengu wa roho kwa maombi.
Mnaweza kuwa
na vita kubwa na mchumba wako kumbe kuna wakuu wa giza wa kiukoo mnatakiwa
muwaponde kwanza kwa mawe ya MUNGU.
Unaweza kuwa
ni mwimbaji na unataka kurekodi nyimbo zako za injili lakini kabla ya kurekodi
unaona vita kubwa kumbe kuna mkuu wa giza ambaye anajua kabisa kwamba kama
ukirekodi hakika nyimbo zako zitakuwa chanzo cha watu wengi kuokoka, mharibu
kwanza kizuizi huyo wa kipepo, mharibu kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la
YESU KRISTO.
Kama mtu anaumwa maana yake alianza
kuumwa kwanza katika ulimwengu wa roho ndipo akaja kuumwa katika ulimwengu wa
mwili, kama ukiudhibiti ugonjwa kwa maombi katika ulimwengu wa roho hakika
ugonjwa huo hutauona katika ulimwengu wa mwili.
Tatizo lako ukilishinda katika
ulimwengu wa roho hakika na kwenye ulimwengu wa mwili utalishinda jambo hilo.
Ndugu mmoja alikuwa anaota ndoto mara
kwa mara anabadilika na kuwa wanyama mara wadudu mara ndege za ajabu ajabu na
kupaa.
Siku moja anakaota anakuwa ngome na
kutembea, siku nyingine akaota akiwa binadamu kama kawaida ila ana mapembe kama ya ng'ombe, Siku nyingine
akaniambia ameota anatembea ghafla akageuka na kuwa bundi na kuweza kuruka.
Nilimwambia
kwamba roho ya uchawi inamfuatilia au inamtumia kabisa bila yeye kujua.
Kuna watu
hutumika kichawi bila wao kujua.
Watu wa rohoni
wanaweza wakajua kabisa kwamba wewe ni mchawi kwa sababu wanakuona katika
ulimwengu wa roho na huku wewe mwenyewe wala hujui kama ni mchawi maana
hujawahi kumroga mtu, lakini kumbe unatumika kichawi bila kujua. Huyu baada ya
miezi kadhaa akaniambia kwamba wanataka kumfanya kuwa kiongozi wa ukoo wao na
kwa jinsi hiyo ametakiwa kujifunza madawa na uchawi kidogo. Nikamkumbusha
kuhusu ndoto zile na hatari zake.
Ndugu zangu
adui akikuweza katika ulimwengu wa roho hakika na katika ulimwengu wa mwili
atakuweza pia ndio maana huwa unaona mipango ya shetani juu yako kupitia ndoto
ili tu uombe kinyume na mipango ile na haitakutokea.
Unaweza
ukaota umekufa na kwa sababu huoni ukifa ukadharau kumbe hakika unakuja kufa
kiroho au uchumi wako unakufa au kazi yako inakufa. Kila jambo huanzia katika
ulimwengu wa roho ndipo linakuja kutokea katika ulimwengu wa mwili.
Unaweza
kutaka kufungua biashara fulani katika eneo fulani, pesa unayo ya kutosha
kabisa lakini unaona ugumu sana juu ya jambo hilo, unatakiwa umharibu kwanza
kizuizi wa kipepo aliyelishikilia eneo hilo.
Nimeanzia
mbali ili unielewa vizuri zaidi katika somo la leo la kumiliki milango ya
baraka aliyokuwa ameishikilia adui.
Kwa sababu umenielewa juu ya vitu vyote
kuanzia katika katika ulimwengu wa roho twende sasa kwenye kiini cha somo langu
na maombi.
Mwanzo 22:17 ‘’ katika kubariki
nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za
mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui
zao;‘’
Uzao wa
Ibarahimu ulipewa kibali na MUNGU cha kumiliki milango ya baraka ambayo adui
alikuwa ameikalia.
Uzao wa
Ibrahimu ni wateule wote wa KRISTO waliookoka.
mimi Peter
Mabula na wewe ndugu uliyeokoka ni uzao wa Ibrahimu na warithi sawasawa na
ahadi ya MUNGU.
Wagalatia
3:29 ''Na kama ninyi ni wa KRISTO, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi
sawasawa na ahadi.''
Kuna siri
kubwa katika Neno Kumiliki milango ya adui.
Kama
unavyoona kuna utawala wa kiserikali katika kila eneo ndivyo hivyo hivyo
shetani naye na jeshi lake anao utawala katika kila Eneo.
Ndio maana
Biblia inawataja watawala wa kishetani ikisema;
''Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya
damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu
ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.-Waefeso 6:12''
Unalishawahi
kujiuliza kwamba hao maadui zetu ambao ni falme za kipepo, mamlaka za
kishetani, wakuu wa giza na majeshi ya pepo wabaya huwa wako wapi?
Ni serikali ya kishetani inayotawala ambayo
wewe mteule wa KRISTO una mamlaka kuliko hiyo serikali ila tu kama utaitumia hiyo mamlaka yako ya
KRISTO kwa maombi.
Kama ambavyo
unapohamia mtaa fulani au kijini fulani utaripoti kwa viongozi wa kijiji au
mtaa ndivyo hivyo hivyo ulimwengu wa roho wa giza una viongozi wa kipepo katika
kila Eneo hivyo ili ulikamate eneo hilo ni lazima uwashinde viongozi hao wa
kipepo.
Inawezekana
hujanielewa lakini ngoja nitoe mifano;
Askofu Moses
Kulola kabla ya kuanza kuhubiri injili ya mafanikio makubwa katika Tanzania
aliingia katika maombi ya kufunga siku 4 mlimani. Katika maombi hayo akiwa
katika siku ya mwisho ya maombi aliona jitu kubwa la kutisha likija alipo na
lilipokaribia lilimwambia kwanini anataka kulichukua eneo lake huyo mkuu wa
giza, yaani Tanganyika kwenye ulimwengu wa roho wa giza kulikuwa na mtawala
wake ambaye ndiyo huyo roho ya kuzimu, kwa maombi Askofu Moses Kulola alimshinda
yule mtoto wa shetani ndio maana akaanza kuhubiri injili ya mafanikio sana.
Kila Eneo huwa lina utawala wa aina tatu. Kuna utawala wa kibinadamu, kuna
utawala kutoka ulimwengu wa roho wa giza na utawala wa MUNGU hutawala pote na
una mamlaka ya mwisho.
Kumbe ili
ulipate eneo fulani kwa ajili ya kitu fulani chako chema inabidi kwa maombi
umpige mkuu wa giza wa eneo husika.
Biblia
inasema wateule watakapopakanyaka patakuwa pao maana yake watakuwa na mamlaka
ya kupatiisha kwa jina la YESU waliyenaye, hata utawala wa shetani utasalimu
amri maana wao wana BWANA YESU mwenye nguvu zote milele.
David Yonggi
Cho wa Korea kusini Ni mhubiri mwenye kanisa kubwa wanaloabudu pamoja kuliko
makanisa yote duniani. Alipoitwa na BWANA YESU ili amtumikie alianza
kumtumikia. Lakini mwanzo tu wa huduma yake aliona mkuu wa giza anayelimiki
eneo la Korea yote. Ilibidi Mchungaji
Yonggi Cho apambane kwa maombi na mkuu yule giza. alipomshinda kwa maombi
kupitia jina la YESU ndipo huduma yake ilistawi na huduma hiyo imefikia hatua
ya sadaka zinahesabiwa kwa zaidi ya siku 2 na sadaka hiyo kuipeleka bank ni kwa
msafara mkubwa kukiwa na ulinzi mkubwa wa Polisi wengi.
Ndugu,
ukishinda katika ulimwengu wa roho hata katika ulimwengu wa mwili utashinda
pia.
Leo omba
ukimtoa aliyekaa katika mlango wa baraka yako katika ulimwengu wa roho.
Omba
ukifungua mlango wa baraka yako na kwa imani chukua baraka yako ili ije
ionekane katika ulimwengu wa mwili.
BWANA YESU
amekufungulia mlango wa baraka mbele yako. Ni kazi yako tu kupambana kwa njia
ya maombi ili upate baraka zako ambazo utazipata ndani baada ya kuingia kupitia
mlango huo.
Ufunuo 3:8
''Nayajua matendo yako. Tazama, nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako, ambao
hapana awezaye kuufunga, kwa kuwa unazo nguvu kidogo, nawe umelitunza neno langu,
wala hukulikana jina langu.''
Mwanzo
kabisa Isaya 60:11 inasema kwamba malango yako au milango yako itakuwa wazi
lakini haiwi wazi bila wewe kuomba iwe wazi.
Baraka
zilizoahidiwa katika andiko hilo hazitakuja kwako bila maombi na utakatifu
katika KRISTO.
Leo Ondoa
maadui waliokaa katika milango yako ya baraka .
Fungua
milango ya baraka zako.
chukua
baraka yako.
Baada ya
kuomba maombi ya toba ya kweli na kuacha uovu nakuomba omba maombi haya kama
wewe ni muombaji mchanga lakini kama wewe unajua kuomba basi huhitaji maombi
haya ila kwa sababu umelielewa fundisho basi omba ukiliiendea hitaji lako.
MAOMBI YA
KUMILIKI MILANGO YA BARAKA ALIKUWA AMEISHIKILIA SHETANI.
BABA katika jina la YESU KRISTO aliye hai.
Ninakushukuru
na kukuabudu pekee uliye MUNGU muumba mbingu na dunia.
asante kwa
siku ya leo na asante kwa uzima ulionipa katika mwanao YESU KRISTO Mwokozi
wangu.
Nakushukuru
kwa ufunuo huu wa leo na naomba kwa damu ya YESU na kwa jina la YESU unipe
ushindi.
Umesema
katika Neno lako katika Mathayo 16:19 Kwamba ''Nami nitakupa wewe funguo za
ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni;
na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni. ''
Leo
nawafunga maadui zako wote walioshikilia milango yangu ya baraka katika
ulimwengu wa roho, nawafunga kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU
KRISTO.
Nawatupa
kuzimu maadui wote walioshirikia milango ya baraka yangu.
Adui
aliyeshikilia mlango wangu wa kupata baraka ya mchumba namharibu na
kumwangamiza adui huyo kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Adui
aliyelishikilia eneo langu la biashara hata sipati faida niitakayo, namharibu
na kumwangamiza adui huyo kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Adui
aliyeshikilia uchumi wangu,
namharibu na
kumwangamiza adui huyo kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Adui
aliyeishikilia ndoa yangu hata inakuwa na migogoro kila siku,namharibu na
kumwangamiza adui huyo kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Adui
aliyeishikilia kazi yangu, namharibu na kumwangamiza adui huyo kwa damu ya YESU
KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Adui aliyeshikilia
kipato changu na kuniletea madeni yasiyoisha,
namharibu na
kumwangamiza adui huyo kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Adui aliyeshikilia ufahamu wangu,
namharibu na
kumwangamiza adui huyo kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Adui
aliyewashikilia ndugu zangu na ukoo wangu,
namharibu na
kumwangamiza adui huyo kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila mlango
wa baraka yangu uliokuwa umefungwa sasa naufungua kwa damu ya YESU KRISTO na
kwa jina la YESU KRISTO.
Mlango wa
kugunga ndoa ndoa ulikuwa umefunga,
sasa
naufungua kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Mlango wa
kupata kazi uliokuwa umefungwa,
sasa
naufungua kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Mlango wa
biashara ulikuwa umefungwa,
sasa
naufungua kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Mlango wa
kupanda cheo uliokuwa umefungwa,
sasa
naufungua kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Mlango wa
kumtumikia MUNGU uliokuwa umefungwa,
sasa
naufungua kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Mlango wa
kupona magonjwa ulikuwa umefungwa,
sasa
naufungua kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Mlango wa
furaha katika familia uliokuwa umefungwa,
sasa
naufungua kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Mlango wa
mafanikio ya rohoni na mwilini uliokuwa umefungwa,
sasa
naufungua kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila mlango
wa baraka yangu ulikuwa umefungwa leo
naufungua kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
Sasa naita
baraka yangu iliyo katika ulimwengu wa roho ili ije sasa katika ulimwengu wa
mwili.
Namuita
mchumba wangu aliyekuwa amezuiliwa katika ulimwengu wa roho, Namwita kwa jina
la YESU KRISTO aliye hai. Ewe Mchumba njoooooooooooooo kwa jina la YESU KRISTO.
Ninaiita
kazi yangu kwa jina la YESU KRISTO.
Ewe kazi
yangu njooo kwa jina la YESU KRISTO.
Ewe uzima
njoooo kwa jina la YESU KRISTO.
Ewe ufahamu
mzuri darasani njoo kwa jina la YESU KRISTO.
Ewe ndoa
safi njooo kwa jina la YESU KRISTO.
Ewe Kiwanja
njooo kwa jina la YESU KRISTO.
Ewe nyumba njooo
kwa jina la YESU KRISTO.
Ewe huduma
nzuri njooo kwa jina la YESU KRISTO.
Ninaita baraka zangu zote kwa jina la
YESU KRISTO zije.
Kwa jina la
YESU KRISTO kila mlango wa baraka yangu utakuwa wazi kama Isaya 60:11
inavyoseama na hakuna adui hata mmoja atakaye ufunga mlango wa baraka yangu.
Nazifunika
kwa damu ya YESU KRISTO baraka zangu zote na adui hatazipata kamwe.
Nakushukuru
JEHOVAH MUNGU wangu kwa ushindi wa ajabu ulionipa leo.
Jina lako
litukuzwe MUNGU uliye hai.
Katika jina
la YESU KRISTO Mfalme wa uzima na ushindi, nimeomba na kupokea ushindi.
Amen Amen.
Ndugu
uliyesoma ujumbe huu ubarikiwe sana.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU
ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Ni mimi Mchungaji Laurent Mpoma
HUDUMA YA NCHI YA UKOMBOZI
(HEMA LA MAOMBI NA MAOMBEZI)
UNAWEZA KUCHANGIA HUDUMA KWA SADAKA
MPESA: +255714890889
TIGO PESA: +255714890889
AIRTEL MONEY: +255782859946
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
TUNAUNUNUZI WA VIFAA HIVI KWA AJILI
YA HUDUMA
1.
VITI 20 @ 20000/=
2.
KIWANJA CHA KANISA 500,000/=
3.
SPIKA 2,000,000/=
4.
VITAMBAA VYA MADHABAHU 60,000/=
5.
MABATI 100 @ 21000/=
6.
MBAO 40 @8000/=
TUNAPOKEA HATA KIDOGO
MUNGU AKUBARIKI SANA, NAKUOMBEA KATIKA JINA LA YESU ALIYE
HAI, UTAFUNGULIWA .
CHANGIA KUPITIA NAMBA HIZO HAPO JUU
ZA NA MCHUNGAJI ATAKUFANYIA MAOMBI MOJA KWA MOJA KWA KUKUPINGIA SIMU.
KABLA HUJATUMA WASILIANA NA MCHUNGAJI
KWANZA.
0 Comments