Laana
ni nini? Laana ni hali ambayo humpata mtu kwa kupitia mambo
mabaya mabaya, yaani ukilaaniwa usitegemee jambo jema kwako labda Mungu
aingilie kati kwani laana ni kinyume cha Baraka, mtu akisema natamka laana juu
yako unachotakiwa kufanya ni kufuta laana hiyo kwa haraka sana. Wakala mkuu wa
Laana ni shetani na ikikupata mambo yako hayaendi sawa. Kama ambavyo Mungu
anabariki watu kwa kuwapa mambo mema vivyo hivyo shetani kupitia mawakala wake
ambao ni waganga wa kienyeji, majini, wachawi anaweza kukalaani kwa kukupa
mikosi, magonjwa, umaskini nk. Kwa maana laana ni kinyume cha baraka na kwa
kuwa shetani ni mpinzani wa Mungu hivyo furaha yake ni kuona unaharibikiwa ili
aharibu mahusiano yako na Mungu kwani watu wengi wakipitia misukosuko wanahisi
Mungu amewaacha.
AINA
ZA LAANA
LAANA
ZA WAZAZI
Hii ni laana inayotokana na wazazi baada ya kuwa mtoto
amefanyia vibaya au ameshindwa kuwaheshimu wazazi wake. Wazazi wapo wa aina
mbili wazazi wa mwilini na wazazi wa kiroho ambao ni wachungaji wetu. Hapa mtu
anawaza mimi baba yangu mzazi hataki niende kanisani na kasema nikienda
atanilaani kwa hili huwezi kulaanika kwani biblia inasema kama mbayuwayu na
laana isiyo sababu haimpati mtu. Ili kuepukana na aina hii ya laana ni lazima
tuwatii na kuwaheshimu wazazi wetu wa mwilini na wa kiroho.
“Mithali 26:2 Kama shomoro katika
kutangatanga kwake, Na kama mbayuwayu
katika kuruka kwake; Kadhalika laana
isiyo na sababu haimpigi mtu.”
LAANA
YA DHAMBI
Laana inayotokana na dhambi hii ni laana inayosababishwa
na mtu kutenda dhambi yaani mtu unatenda dhambi na hutaki kuiacha mwisho wa
siku unaangukia katika laana.
“wenye macho yajaayo uzinzi, watu wasiokoma kutenda
dhambi, wenye kuhadaa roho zisizo imara, wenye mioyo iliyozoezwa kutamani, wana
wa laana;” (2Petro 2:14)
LAANA
YA WIZI
hii ni laana ambaayo watu huipata kwa kumibia Mungu fungu
la kumi au sadaka, kutokutoa marimbuko. Lakini pia kuna laana ya wizi wa muda
watu tumejisahau kwenye suala la muda unakuta mtu ibada inaanza saa tatu we
unafika saa tano hapa umemwibia Mungu muda maana muda ambao ulitakiwa uwe
unafanya kazi ya Mungu kwa kuomba au kusifu wewe ulikuwa unafanya mambo yako.
Tubu hivi leo na uache kabisa kwa jina la Yesu.
“Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam,
taifa hili lote. Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba
yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo,” (Malaki
3:9-10)
LAANA
ZA UKOO
Hizi ni laana ambazo zimesababishwa na wahenga wa ukoo
pamoja na babu zetu, zamani zile za ujinga babu zetu hawakumjua Mungu hivyo
walitegemea miungu wengine kama miti mikubwa, mawe, mizimu na majini, hivyo
kuna mikataba waliingia mfano kuua watu, kunywa damu mbichi nk ambavyo viyu
hivi ni kinyume na utaratibu wa Mungu hivyo tunatakiwa kutubu kwa ajili ya koo
zetu na kufuta kila mikataba na laana walizotamka babu zetu kwa damu ya Yesu
uwe unazijua ma huzijui.
LAANA
ZA WACHAWI
Laana za wachawi, hizi ni laana zinazotokana na wachawi
wenyewe yaani wanakutafutia sababu ili wakupige kwa laana. Wachawi ni watu
kabisa lakini wao wamekubaliana na shetani kuzitenda kazi za uovu.
Wachawi wameingia na kusaini mikataba kabisa kwa shetani
mfano wanamwambia nipe nguvu za kuloga na mimi nitakupa mwanangu au mume wangu,
mama yngu nk. Kama unavyojua shetani ni takataka na makao yake ni kuzimu hivyo
kila kinachotoka kuzimu ni takataka ndivyo ilivyo kwenye maisha yetu ya kila
siku kwani shetani anaungana na wachawi kurusha laana kwa watu na laana hizi
huweza kumpata mtu hata pasipo sababu. Kama ambavyo Mungu akitaka kumbariki mtu
anatumia watu kama wachungaji ambao wakikutamkia baraka kwa jina la Yesu
zinakuwa. Na mara nyingi baraka hizi hutamkwa kwenye madhabahu takatifu ndivyo
ilivyo kwa shetani naye na vibaraka wake wana madhabahu zao kwenye nyumba za
wachawi, waganga wa kienyeji, milimani, kwenye vichuguu nk.
Hivyo mashetani wakiitwa wanapanda toka kuzimu na
wanakuja kusikiliza nini mganga au mchawi anatamka juu ya mtu fulani? Na mganga hutamka laana na wakati huo
huchinja wanyama, ndege, na hata wanadamu lengo ni kumwaga damu na damu hiyo
ndicho chakula cha majini. Hivyo damu ikimwagwa majini wanaimarika na kuwa
shupavu katika kusimamia kile kilichotamkwa kiweze kutimia kwa aliyetamkiwa.
Lakini leo hii tunayokafara ya mwisho ya damu ya Yesu ambayo kwayo kila laana
inafutwa na damu hii haijawahi kuisha wala kupungua nguvu.
“Maana katika watu wangu wameonekana watu waovu; huotea
kama vile watu wategao mitego; hutega mtego, na kunasa watu. Kama tundu
lijaavyo ndege, kadhalika nyumba zao zimejaa hila; kwa hiyo wamekuwa wakuu,
wamepata mali. Wamewanda sana, wang'aa; naam, wamepita kiasi kwa matendo maovu;
hawatetei madai ya yatima, ili wapate kufanikiwa; wala hawaamui haki ya
mhitaji. (Yeremia 5:26-28)”
Mungu anasema katika watu wangu wameonekana watu waovu,
kwa kifupi watu wote ulimwenguni ni watu wa Mungu kwani wameumbwa na Mungu
lakini wapo ambao wamemuasi Mungu na kukubali kufanya kazi na shetani na kwa
hiyo hata nia zao zimegeuzwa yaani zimekosa utu, huruma , na hao ndiyo
wanaoamua kufanya kazi za uchawi na kutoa laana kwa watu wengine.
Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa
jinsi ya mwili; (maana silaha za vita
vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;) (2wakorinto 10:3-4)
Ingawa tunaenenda katika mwili lakini hatu fanyi vita kwa
jinsi ya mwili. Hivyo katika kuomba kwako unatakiwa kushindana rohoni hapa
namaanisha hata ukimjua mchawi wa maisha yako usimfuate kwenda kumpiga mwilini
bali mpige rohoni kama ambavyo na wao huturoga rohoni lakini matatizo
yanatupata mwilini.
Kisha wana wa Israeli wakasafiri na kupanga katika nchi
tambarare za Moabu ng'ambo ya pili ya Yordani karibu ya Yeriko. Na Balaki mwana
wa Sipori akaona mambo yote ambayo Israeli wamewatendea Waamori. Moabu
akawaogopa hao watu sana, kwa kuwa walikuwa wengi; Moabu akafadhaika kwa sababu
ya wana wa Israeli. Moabu akawaambia wazee wa Midiani, Sasa jeshi hili la watu
litaramba vitu vyote vinavyotuzunguka, kama vile ng'ombe arambavyo majani ya
mashamba. Na Balaki, mwana wa Sipori, alikuwa mfalme wa Moabu zamani zile. Basi
Balaki akatuma wajumbe kwa Balaamu mwana wa Beori, hata Pethori, ulio kando ya
Mto, mpaka nchi ya wana wa watu wake, kwenda kumwita, akisema, Tazama, kuna
watu waliotoka Misri; tazama, wanaufunika uso wa nchi, tena wanakaa kunikabili
mimi. Basi, njoo wewe, nakusihi unilaanie
watu hawa; maana wana nguvu kunishinda mimi. Labda nitawaweza, tupate
kuwapiga, niwafukuze watoke katika nchi
yangu, kwa maana najua ya kuwa yeye umbarikiye hubarikiwa, na yeye umlaaniye
hulaaniwa. Wazee wa Moabu, na wazee wa Midiani, wakaenda, wakichukua ujira wa
uganga mikononi mwao; wakamfikilia Balaamu,
wakamwambia
maneno ya Balaki. ( Hesabu 22:1-7)
Na wewe leo kila aliyekuroga au kukulaani akuogope kwa
jina la yesu.
Mambo ya mtu yakiwa mazuri, afya njema, watoto umezaa,
mali unazo nk ndipo maadui wanainuka na kutaka kuyapinga mafanikio yako. hapa ndipo mafanikio yako huanza kuyumba
kwani ndipo wachawi wanapokutamkia laana ili uharibikiwe. Ukiona mchawi
anakuroga jua wewe si mtu wa kawaida yaani umeumbwa kwa namna ya kutisha. Leo
kila laana iliyotamkwa kwako na wachawi kwa sababu ya kuiogopa hatima yako
nawaponda kwa jina la Yesu.
Neno la Bwana ni uhai na ni kila kitu hivyo kila
kilichoandikwa kitatimia kwako kwa jina la Yesu ikiwa utaliitia jina la
Bwana.Kuna mahali mtu umefikia ni hatua nzuri lakini kwa hiyo hatua wachawi ndo
wanaamka kukutafutia laana ili uharibikiwe mambo yako. ili kukwepa laana hizi
lazima uwe mtiifu kwa Mungu toa zaka, sadaka, hudhuria ibada kwa kuwahi kabisa
komboa muda wako na usimubie Mungu zaka wala muda wake kwa jina Yesu.
Balaamu naye, huyo mwana wa Beori, huyo mchawi, wana wa
Israeli walimwua kwa upanga kati ya hao wengine waliowaua. (Yoshua 13:22)
Balaamu alikuwa mchawi wa kukodisha yaani alikuwa mchawi
aliyebobea kwenye mambo ya uchawi hadi watu wakawa wanamkodi ili kuwalaania watu
wao . lakini leo kila mchawi aliyeitwa
kukulaani namteketeza kwa jina la Yesu.
wakiiacha njia iliyonyoka, wakapotea, wakiifuata njia ya
Balaamu, mwana wa Beori, aliyependa ujira wa udhalimu; (2Petro 2:15)
Ole wao! Kwa sababu walikwenda katika njia ya Kaini, na
kulifuata kosa la Balaamu pasipo kujizuia,
kwa ajili ya ujira, nao wameangamia katika maasi ya Kora.(Yuda 1:11)
Kuna watu wengine wamejitumbukiza kwenye matatizo yaani
wamekuwa wachawi kwa sababu ya tamaa zao hivyo wamegeuka wamekuwa watoa laana kwa
wenzao kwa kuwa roho ya uchawi imeingia ndani yao. Lengo la watu hawa mara
nyingi hupenda mali za haraka, huchukia mafanikio ya wengine na kutaka yawe yao
mwisho wa siku wanajikuta wameangukia kuzimu.
Leo kila mwenye roho ya kutamani mafanikio yako namfyeka kwa jina la
Yesu. Na wewe kama unanyemelewa na hiyo roho ya tamaa naiondoa na kuifuta kwako
kwa damu ya Yesu.
Lakini ninayo maneno machache juu yako, kwa kuwa unao
huko watu washikao mafundisho ya Balaamu, yeye aliyemfundisha Balaki atie
ukwazo mbele ya Waisraeli, kwamba wavile vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu,
na kuzini. (Ufunuo 2:14)
Tamaa ya sadaka au kupokea msaada wa hovyohovyo unaweza
kukufanya ukaingia matatizoni mfano mtu
anakwambia nitakununulia kitanda, godoro, bure kabisa anakueleza kwamba hivi
vitu nimekununulia lakini…..
Ukiona kuna lakini jua shimo la kuzimu linakuita, kataa
kuitwa kuzimu kwa jina la Yesu.
Mfano mzuri ni
Baalamu ambaye watu walimtumia ili
alaani watu na kuwasababishia matatizo lakini leo kila Balaamu wa maisha yako
tunamnyonga kwa jina la Yesu. (Hesabu 22:8-14)
Yule punda akamwambia Balaamu, Je! Mimi si punda wako,
nawe umenipanda maisha yako yote hata leo? Nimezoea kukutenda hayo? Akasema,
La!( Hesabu 22:30)
“ Balaamu akamwambia Balaki, Nijengee hapa madhabahu
saba, ukaniandalie hapa ng'ombe waume saba, na kondoo waume saba. Balaki
akafanya kama Balaamu alivyonena. Balaki na Balaamu wakatoa sadaka, ng'ombe
mume mmoja na kondoo mume mmoja juu ya kila madhabahu” (Hesabu 23:1)
Wachawi wanapoamua kumloga mtu ni lazima wamjengee
madhabahu mara nyingi madhabahu hizi huwa ni za kulaania. Mfano Balaki na
Balaamu wali[ojenga madhabahu juu ya mlima.
Leo kila madhabahu zilizojengwa kwa ajili yako nazivunja kwa jina la
Yesu na kila laana iliyotamkwa juu ya maisha yako naifuta kwa jina la Yesu.
Kila pando asilopanda baba wa mbinguni litang’olewa leo nang’oa kila pando la
laana za wachawi juu ya maisha yako kwa jina la Yesu.
Ndugu yako anaweza akamuita mganga au akakodisha mchawi
toka mbali ili aje akulaani lakini leo kila laana na majini waliyokutumia
nayakusanya kwenye umbo moja na ninawarushia wao kwa jina la yesu.
“Akarudi kwake, na tazama, amesimama karibu na sadaka
yake ya kuteketezwa, yeye na wakuu wote wa Moabu pamoja naye. Akatunga mithali
yake, akasema, Balaki amenileta kutoka Aramu, Mfalme wa Moabu kutoka milima ya
mashariki, Njoo! Unilaanie Yakobo,
Njoo! Unishutumie Israeli. Nimlaanije, yeye ambaye Mungu hakumlaani? Nimshutumuje, yeye ambaye Bwana hakumshutumu?
Kutoka kilele cha majabali namwona; Na
kutoka milimani namtazama; Angalia, ni
watu wakaao peke yao, Wala hawatahesabiwa pamoja na mataifa. Ni nani awezaye
kufanya idadi ya mavumbi ya Yakobo, Au kuhesabu robo ya Israeli? Na nife kifo chake mwenye haki, Na mwisho wangu uwe mfano wa mwisho wake.
Balaki akamwambia Balaamu, Umenitendea nini? Nimekuleta ili Uwalaani adui
zangu, na tazama, umewabariki kabisa kabisa.
Naye akajibu, akasema, Je! Hainipasi kuangalia, niseme neno lile Bwana
atialo kinywani mwangu? Balaki
akamwambia, Haya! Njoo, tafadhali, hata mahali pengine, na kutoka huko utaweza
kuwaona; utaona upande wa mwisho wao tu, wala hutawaona wote, ukanilaanie hao
kutoka huko. Akamchukua mpaka shamba la
Sofimu, hata kilele cha Pisga, akajenga madhabahu saba, akatoa sadaka ng'ombe
mume mmoja na kondoo mume mmoja juu ya kila madhabahu. Akamwambia Balaki, Simama hapa karibu na
sadaka yako ya kuteketezwa, nami nitaonana na Bwana kule. Bwana akaonana na Balaamu akatia neno kinywani
mwake, akasema, Umrudie Balaki, ukaseme hivi. Akafika kwake, na tazama,
amesimama karibu na sadaka yake ya kuteketezwa, na wakuu wa Moabu pamoja naye.
Balaki akamwambia, Bwana amenena nini?
Naye akatunga mithali yake, akasema, Ondoka Balaki, ukasikilize;
Nisikilize, Ee mwana wa Sipori; Mungu si
mtu, aseme uongo; Wala si mwanadamu, ajute;Iwapo amesema, hatalitenda? Iwapo
amenena, hatalifikiliza? Tazama,
nimepewa amri kubariki, Yeye amebariki, nami siwezi kulitangua. Hakutazama uovu
katika Yakobo, Wala hakuona ukaidi katika Israeli. Bwana, Mungu wake, yu pamoja naye, Na sauti
kuu ya mfalme i katikati yao. Mungu
amewaleta kutoka Misri, Naye ana nguvu kama nguvu za nyati. Hakika hapana
uchawi juu ya Yakobo, Wala hapana uganga juu ya Israeli. Sasa habari za Yakobo
na Israeli zitasemwa, Ni mambo gani aliyoyatenda Mungu! Tazama, watu hawa wanaondoka kama simba mke,
Na kama simba anajiinua nafsi yake, Hatalala hata atakapokula mawindo, Na
kunywa damu yao waliouawa. Balaki
akamwambia Balaamu, Basi usiwalaani kabisa, wala usiwabariki kabisa. Lakini Balaamu akajibu akamwambia Balaki, Je!
Sikukuambia ya kwamba, Kila neno Bwana atakalolisema sina budi kulitenda? Kisha Balaki akamwambia Balaamu, Haya, njoo
sasa, nikupeleke mahali pengine; labda Mungu ataridhia kwamba unilaanie watu
hao huko. Basi Balaki akamchukua Balaamu
akaenda naye mpaka kilele cha mlima Peori, mahali paelekeapo upande wa nyika
iliyo chini yake. Balaamu akamwambia Balaki, Haya, unijengee hapa madhabahu
saba, kisha uniandalie ng'ombe waume saba, na kondoo waume saba”(Hesabu 23:6-29)
Katika maandiko hapa tunaona Balaki akimkodi Baraamu ili
amalaanie watu wake lakini badala ya laana ikawa baraka. Mungu wetu
tunayemtumikia anaouwezo wa kugeuza laana zikawa baraka ikiwa tutamwamwini na
kumtumikia kwa moyo wa kupenda. Maandiko yanasema nimlaanije?Yeye ambaye Bwana
hakumlaani?
Kumbe Mungu wetu hukamata vinywa vya waovu badala ya
kutamka laana wanatamka Baraka. Leo kila anaekusudia kukutamkia laana
nakikamata kinywa chake na ninatia maneno ya Mungu kinywani mwake mpaka
wakutamkie Baraka kwa jina la Yesu.
Leo naamuru kila kilichopotea kwenye maisha yako kupitia
laana za wachawi virejeshwe kwako kwa jina la Yesu. Na vinaporudi vibebe na
baraka zako zote kwa damu ya Yesu.
Mungu anasema atafanya mambo makubwa ambayo macho yako
hayawahi kuyaona wala masikio yako hayajawahi kuyasikia, leo naamuru mambo yote
makubwa yakufuate wewe na uzao wako kuanzia leo kwa jina laYesu.
“Basi Balaamu alipoona ya kuwa ilimpendeza Bwana kuwabariki
Israeli, hakwenda, kama hapo kwanza, ili kutafuta uchawi, bali alielekeza uso wake jangwani” (Hesabu 24:1)
Leo kazi yetu ni kuzigeuza na kuzibatilisha laana zote
ulizotamkiwa, au ambazo wanapanga kuzitamka juu ya maisha yako tunazigeuza ziwe
baraka kwa jina la YESU. Na madhabahu zilizojengwa juu yako nazivunja kwa
nyundo ya neno la Mungu.
<<<<<MUNGU AKUBARIKI SANA KWA KUJIFUNZA MANENO YA MUNGU>>>>>>>>>>
SOMA UJUMBE HUU NI MUHIMU SANA KATIKA MAISHA YAKO LEO ILI MUNGU AKUPANDISHE VIWANGO VYA JUU.
2 Mambo ya Nyakati 1:7-12
Usiku ule Mungu akamtokea Sulemani,
akamwambia, Omba utakalo nikupe. Sulemani akamwambia Mungu, Umemfanyia baba
yangu Daudi fadhili kuu, nawe umenimilikisha mimi badala yake. Basi sasa, Ee
BWANA Mungu, na limyakinie baba yangu Daudi neno lako; maana umenitawaza niwe
mfalme juu ya watu wengi kama mavumbi ya nchi. Basi sasa nipe hekima na
maarifa, nijue kutoka na kuingia mbele ya watu hawa; kwa kuwa ni nani awezaye
kuwatawala watu wako hawa walio wengi? Naye Mungu akamwambia Sulemani, Kwa
sababu neno hili lilikuwamo moyoni mwako, wala hukujitakia mali, wala utajiri,
wala utukufu, wala maisha ya wakuchukiao, wala hukujitakia maisha ya siku
nyingi; bali umejitakia hekima na maarifa, upate kuwatawala watu wangu,
niliokutawaza juu yao; basi hekima na maarifa umepewa; nami nitakupa mali, na
utajiri, na utukufu, kupita walivyokuwa navyo wafalme wote waliokuwa kabla
yako, wala baada yako hapatakuwa na mtu atakayekuwa navyo.
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
KANISA LA ELIM PENTEKOSTE NCHI YA UKOMBOZI- MUHAWA SINGIDA MJINI.
(NENO, MAOMBI NA MAOMBEZI)
Tuna ununuzi wa vifaa kwa ajili ya Mkutano wa Injili. Unaweza kuchangia kwa ajili ya kuhubiri injili na Mungu atakutana na wewe na kuzungumza na wewe na atatenda mambo makubwa sana kwenye maisha yako kuanzia leo.
TUNAHITAJI KUNUNUA.
1. VITAMBAA VYA MADHABAHU........TSHS, 60000/=
2.MAIKI WIRELESS....4......TSHS, 240,000/=
3. MAIKI ZA WIRE......4.......TSHS, 100,000/=
4. TRUBAI...........4..........TSHS, 60,000/=
5. MABATI 20@ 27,000......JUMLA NI TSHS, 540,000/=
6. DRAMS......1........TSHS, 1,100,000/=
7.SPEAKER FIDEK 3......TSHS, 2,100,000/=
WASILIANA NA MCHUNGAJI ILI MCHUNGAJI AKUOMBEE PAPO HAPO UTAKAPOCHANGIA KIMOJA WAPO KATI YA HIVYO HAPO JUU AU CHOCHOTE ULICHO NACHO TUNAPOKEA.
MUNGU AKUBARIKI SANA, AKUFUNGUE KWENYE HILO UNALOPITIA, MUNGU AKUINUE KATIKA FAMILIA, UCHUMI, KAZI NA MENGINEYO UNAYOHITAJI KATIKA MOYO WAKO.
NAMBA ZINAZOTUMIKA KATIKA MCHANGO NI NAMBA ZA MCHUNGAJI TU.
1. M-PESA 0762756542.....JINA: LAURENT MPOMA
2. AIRTEL MONEY: 0782859946....JINA: LAURENT MPOMA
3: TIGO PESA: 0714890889.....JINA : LAURENT MPOMA
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
KWA
MSAADA ZAIDI NA MAOMBEZI:
WASILIANA
NA MCHUNGAJI AU
FIKA
KANISANI,
KANISA LA ELIM PENTEKOSTE NCHI YA UKOMBOZI
(NENO, MAOMBI NA MAOMBEZI)
AU
WASILIANA NASI KUPITIA
FACEBOOK:
nchi ya ukombozi ministry
Follow
us on YOUTUBE: Upenyo Wa Mungu Tv
TELEPHONE:
+255762756542
WHATSAP:
+255762756542
BLOG:
NCHI YA UKOMBOZI MINISTRY
http://
nchiyaukomboziministrytz.blogspot.com/
MUNGU AKUBARIKI SANA KWA KUJIFUNZA MANENO YA MUNGU.
0 Comments