MAMBO KUMI YA KUFANYA ILI UWEZE
KUPATA KIBALI MBELE ZA MUNGU
1: KUTENDA MEMA
Matendo mema
huleta kibali MUNGU alipokuwa anaona wivu kwa ajili ya ndugu yake Habili . Mwanzo 4:7 Kama ukitenda
vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo
inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde.
Mpendwa
wangu tenda mema utapata kibali.Fanya mema kuliko wenine nawe utaona kibali
chako kikiongezeka . Pokea uwezo huo wa kutenda mema kwa uweza wa jina la YESU.
2: KUSHIKA NENO LA MUNGU.
Katika
mithali Sura 3 unaona mambo makuu mawili ili uweze kupata KIBALI
NA AKILI NZURI. Mungu wetu anayo hazina ya Kibali na akili nzuri kwa watu watakaolishika na wale
watakaotembea katika rehema na kweli.
Mithali 3:1-4
1 Mwanangu,
usiisahau sheria yangu, Bali moyo wako uzishike amri zangu.
2.Maana
zitakuongezea wingi wa siku. Na miaka ya uzima, na amani.
3 Rehema na kweli zisifarakane nawe; Zifunge
shingoni mwako; Ziandike juu ya kibao cha moyo wako.
4 Ndivyo utakavyopata kibali na akili nzuri,
Mbele za Mungu na mbele ya mwanadamu
Neno Rehema
limetafsiriwa kwa lugha ya kingereza kama huruma ndio maana unakuta unapowauhurumia wengine
uwe na uhakika kwamba utakuwa na kibali.Kinyume chake ni kweli kwa mtu mkatili asiye na huruma watu huwa wanamuogopa
na kuwa mbali naye.
3: KIBALI KUTOKANA NA KUTUMIKI KUSUDI LA MUNGU .
weza kulitambua
kusudi la kuumbwa kwako uwe na uhakika
kabisa kibali cha MUNGU kitaachiliwa kwako kuhakisha kwamba unalifanikisha.
Kbali hiki kilikuwa juu ya MUSA Kutoka 11:3 Bwana akawapa watu hao kibali
machoni pa Wamisri. Zaidi ya hayo, huyo Musa alikuwa ni mkuu sana katika nchi
ya Misri, machoni pa watumishi wa Farao, na mabalbali choni pa watu wake.
Ukisoma kwa
utulivu kuanzia mstari wa pili utagundua kwamba MUNGU aliachilia kibali kwamba
kila walichokihtaji kutoka kwa Wamisri wakaweza kupatiwa. Hiki ndicho kibali
alichokipata Nehemia mbele ya mfalme na kuruhusiwa kupewa vitu kwa ajili ya ujenzi wa ukuta wa
Yerusalemu.
Mungu wetu
ambaye hhabadiliki na akuachilie kibali hiki sawa na lile kusudi la kuumbwa
kwako katika jina la Yesu.
4: KIBALI HUJA KWA MAOMBI.
Kuna watu
wanasema kibali hakiombwi lakini utamuona Esta na Wayahudi wakiomba kibali kwa
MUNGU aweze kupata kibali mbele za Mfalme. Uende ukawakusanye Wayahudi wote
waliopo hapa Shushani, mkafunge kwa ajili yangu; msile wala kunywa muda wa siku
tatu, usiku wala mchana, nami na wajakazi wangu tutafunga vile vile; kisha
nitaingia kwa mfalme, kinyume cha sheria; nami nikiangamia, na niangamie. Esta 4:16
MUNGU AKUBARIKI SANA
MAOMBI NA MAOMBEZI
WASILIANA NA MCHUNGAJI LAURENT MPOMA
+255714890889
WHATSAP: +255762756542

0 Comments