Follow us

VIFUNGO VYA MWILINI

Tangazo




VIFUNGO VYA MWILINI 

 Utangulizi:

Mungu anawapenda sana wanadamu na Biblia inasema wazi kuhusu hili katika kitabu cha Maombolezo 3:31; Ni raha yake kuona hatuna matatizo na tunaishi kwa amani. Mungu hakumuumba mwanadamu ateseke bali alimuumba afanikiwe akiwa duniani na kuishi kwa furaha.

 Wakati huohuo, shetani kwa asili hapendi mtu aliyeumbwa na Mungu afanikiwe na ndio maana katika Luka 3:16 inasema, “…ambaye shetani amemfunga miaka kumi na minane…” (Matendo 10:38; 2Wathesalonike 2:18-19) kwa maandiko hayo tunaweza kujua kuwa shetani anaweza kufunga, kuzuia, kupinga na kushindana na mtu.

 Kwa asili shetani ni mshindani na furaha yake ni kuwatesa wanadamu ambao wanapendwa na Mungu. Yeye hufanya hivi ili kuumiza moyo wa Mungu kupitia wanadamu walioumbwa na Mungu.

 SHETANI ANAWEZA KUMFUNGA MTU:

Kama tulivyoona kuwa shetani anapenda kuwatesa wanadamu na ili kutimiza lengo lake njia mojawapo anayotumia ni kuwafunga watu. Na tunapotaja vifungo, tunakuwa tunazungumzia vifungo vya aina kuu tatu, yaani, Vifungo vya mwilini, Vifungo vya rohoni na vifungo vya nafsini kwasababu mtu ni roho inayokaa ndani ya nyumba iitwayo mwili. Katika hatua hii ya kwanza tunaanza kuangalia kwa undani kuhusu vifungo vya mwilini:-

 Mwili ni nini?

Hatuwezi kujua namna mwili unavyoweza kufungwa bila kujua asili ya mwili wa binadamu. Tuanze kwa kuangalia andiko hili Mwanzo 2:7 “BWANA Mungu akamfanya mtu kutoka katika mavumbi ya ardhi…” kumbe asili ya mwili wa mwanadamu ni mavumbi au udongo. Na ndio maana katika Isaya 64:8 Biblia inasema, “… sisi tu udongo nawe ni mfinyanzi wetu...” nabii Isaya ambaye aliwahi kumuona Mungu lakini alijua ukweli huu kuwa mwili ni mavumbi (Ayubu 7:21, 34:15). Kumbe pamoja na kuwa umevaa vizuri au umeupamba mwili vizuri lakini asili yake ni udongo na katika ulimwengu wa roho huonekana kuwa ni udongo kabisa. Kwa ufupi mwili wa mwanadamu ni udongo na mtu anapokufa mwili huirudia nchi (Mhubiri 12:7) yaani mavumbi.

>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>> 

MUNGU AKUBARIKI SANA KUJIFUNZA MANENO YA MUNGU

MAOMBI NA MAOMBEZI

WASILIANA NA MCHUNGAJI LAURENT MPOMA

 

NCHI YA UKOMBOZI MINISTRY

(HEMA LA MAOMBI NA MAOMBEZI)

PHONE: +255714890889

WHATSAP: +255762756542

TUMA MAHITAJI YAKO LEO MCHUNGAJI ATAKUOMBEA NA KUKUPATIA USHAURI.

>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>> 

SOMA :  (2 MAMBO YA NYAKATI 1:7:  Usiku ule Mungu akamtokea sulemani, akamwambia, omba utakalo nikupe).

Tunaupanuzi wa kiwanja cha kanisa ambacho kinahitaji shilingi milioni tatu (3,000,000/=). Kiasi chochote tunapokea. MUNGU akubariki sana kwa utoaji wako. Hakika Amini Mungu anakwenda kukutana na wewe kama sulemani alivyotokewa usiku ule sasa ni zamu yako.

UNAWEZA KUTUMA HAPA

MPESA: +255762756542……………..JINA: LAURENT MPOMA

TIGO PESA: +255714890889…………JINA: LAURENT MPOMA

AIRTEL MONEY: +255782859946…….JINA :LAURENT MPOMA

 

CRDB BANK: 0152363022800………LAURENT ELIAS MPOMA

NMB BANK: 50810025078……..LAURENT ELIAS MPOMA



Post a Comment

0 Comments