SOMO: MADHARA YA KUAPA KIAPO WAKATI WA UCHUMBA.
Kuna watu wapo katika hali ya kukata tamaa kabisa ya
kuoa/kuolewa baada ya kusubiri na kuomba kwa muda mrefu bila majibu
yoyote.Wakati mwingine wamefikia hali ya kusema ataoa au kuolewa na mtu yoyote
Yule atakayekuja mbele yake ,maana haoni tumaini lolote katika kumsubiri Mungu.
Zipo sababu kadhaa kwanini mtu anaweza kupitia hali hiyo
,lakini leo nataka kuongelea madhara ya
kiapo ambacho watu huweka wakati wa uchumba. Wengi wamefungwa hapa bila kujua
,hivyo naamini kupitia ujumbe huu utaenda kuwafungua wengi …AMINA.
Wakati wapo katika mahusiano ya awali au uchumba huwa
wanafunikwa na wimbi kubwa sana la upendo ambao linawafanya hata wasiweze kuona
mbele, Na ndio maana husema mapenzi ni upofu na kupitia upofu huu wengi
wanaishia kujuta baadaye na kujilaumu yale waliyofanya nyuma.
Unakuta watu wapo katika uhusiano kwa malengo ya kuja kuoana
hapo baadaye na wanaanza kuishi maisha ambayo kiukweli ni kama wanandoa tayari
,na mbaya zaidi wanajiingiza kwenye VIAPO kuwa hatutakuja kuachana na kama
ikitokea mmoja wetu amemuacha mwenzake basi asioe /kuolewa ,wengine hudiriki
hata kuweka viapo vya mauti kwa kusema kama mmoja akimuacha mwenzake basi kufa
na aafe.
Bila kujua kwa maana wamefunikwa na upofu hu wa mapenzi
wanajikuta wameingia kwenye mtego wa Ibilisi na kushindwa kutoka.Kiapo hiki uwa
kina dumu milele kama hakitaondolewa au labda mpaka pale wahusika watakapokufa
(inategemea na aina ya kiapo chenyewe).
Kuna utofauti kidogo kati Kiapo na Nadhiri,
• Kiapo ni
makubaliano baina ya watu wawili au zaidi kuwa watafanya au kutofanya jambo Fulani, Na kama mmoja wao akitokea
kwenda kinyume basi Adhabu Fulani itakuwa juu yake.
Watu hutumiza makubaliano hayo kwa kutaja mbingu ,kitu
chochote katika dunia ,miungu au Mungu. Pia waapaji huweza kuapa kwa kutumia
damu zao wenyewe kwa kuikata sehemu zao za mwili na kulishana au kuzigusanisha
damu zao,huweza kutumia sadaka abayo huitoa kwa pamoja nk
Kiapo mara nyingi huusisha mtu na mtu .Soma 1 Samwei 20:12-17,Mwanzo
24 :1-4
• Nadhiri ni
maombi ambayo mtu huomba kwa Mungu kwa ahadi kuwa kama Mungu akimjibu ombi lake
hilo basi atafanya kitu Fulani kwa ajili ya Mungu.
Nadhiri humuusisha mtu na Mungu.Soma 1 Samweli 1 :10 -11
Sasa watu wanapoweka viapo hivyo wanaweza wakaja baadaye
wakasahau ni nini ambacho wameapa na kwenda kinyume na kiapo hicho na hapo
ndipo madhara yanapojitokeza,Ile adhabu waliyokubaliana kuwa itokee kama
wakishindwa kutekeleza kiapo hicho hujionesha hapa na kuanza kufanya kazi.
KWANINI KIAPO KINA NGUVU
1 . IPO NGUVU KATIKA MAKUBALIANO YA PAMOJA
Neno la Mungu linasema “ Amina (Hakika) , Nawaambia yoyote
mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa na mbinguni” Mathayo 18:18(a)
Hivyo kama mmeapa kuwa kama mkichana msioe/kuolewa basi
mbingu itayahifadhi maneno hayo na ikitoea mmeachana duniani basi mbingu
itatimiza kile amabacho mmekubaliana cha kutokuoa au kuolewa.
2 . IPO NGUVU YA UUMBAJI KATIKA KINYWA.
Binadamu tumeumbwa kwa mfano wa Mungu ( Mwanzo 1:26), mungu
aliumba dunia kupitia Neno ,alitamka na vitu vikawa kama alivyotamka (Mwanzo
sura 1). Hivyo kama tumeumbwa kwa mfano wa Mungu ,nguvu hiyo ya uumbaji ipo pia
vinywani mwetu tunapotamka vitu (hasa kwa Imani).
Ndio maana biblia inasema “Mauti na Uzima huwa katika uwezo
wa ulimi ,Na wao waupendao watakula matumda yake “ Mithali 20: 21
3 . KIAPO NI KINYUME CHA NENO LA MUNGU.
Biblia inakataza tusiape , hivo kama ukiapa utakuwa umetenda
dhambi na dhabi yoyote ina hukumu.Kma ni mtu uliyeokoka halafu ukaapa ina maana
utakuwa umetoka katika mapenzi ya MUngu na kumpa ibilisi nafasi ya kukutesa
katika maisha yako.Na kiapo kinatesa..!
“Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa Usiape uongo ila
mtimizie Bwana nyapo zako.Lakini mimi nawaambia Usiape kabisa hata kwa mbingu
maana ndicho kiti cha enzi cha MUngu,wala kwa kwa nchi maana ndiyo pa kuwekea
miguu yake ,wala kwa Yerusalemu kwa maana nido mji wa Mfalme mkuu , wala usiape
kwa kichwa chako maana hauwezi kufanya unwele mmoja kuwa mweupe au mweusi”
Mathayo 5:32-36
Kutokana na sababu hizo tulizoziona kiapo kinaweza kukutia
katika mateso na kifungo kukibwa katika maisha yako na bila kufahamu hili na
kupata msaada wa kiroho utaendelea kutumikia kiapo hicho na kuwa gereza lako la
milele.
NIFANYE NINI ILI NIONDOKANE NA MADHARA YA KIAPO NILICHOWEKA?
• Jambo la
kwanza na la muhimu ni kujichunguza ni wapi uliweka maagano na mtu na ukashinwa
kuyatekeleza.
• Ingia kwenye
maombi ya Toba ,tubu kwa dhambi hiyo uliyoifanya na omba Munguakusaidie kutoka
hapo . Hapa wakati mwingine utahitajika hata kufanya maombi ya kufunga ya muda
mrefu (Itategemea na vile Roho Mtakatifu atakavyosema nawe).
• Vunja agano
hilo uliloweka kwa kinywa chako. Uliweka agano kwa kinywa chako na unatakiwa
ulivunje kwa kinywa chako.
“…..Na yoyote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa
mbinguni “ Mathayo 18:18(b)
Fungua kiapo hicho kwa jina la Yesu.
Kama umeona unafanya hivi nabado hakuna mafanikio au Mungu
anakuuongoza uende kwa mtumishi Fulani ili akusaidie basi fanya hivyo.
USIKUBALI KUWEKA KIAPO NA MTU YOYOTE KWA AJILI YA
CHOCHOTE..KIAPO CHAKO HAKIKUFANYI UONEKANE MUAMINIFU BALI KITAKUFANYA UINGIE
KWENYE HUKUMU ISIYO NA SABABU.MOYO USIKUDANGANYE ..YEREMIA 17:9
“LAKINI NFUGU ZAIDI YA YOTE
NDUGU ZANGU ,MSIAPE KWA MBINGU WALA KWA NCHI ,WALA KWA KIAPO
KINGINECHO..BALI NDIYO YENU NA IWE NIYO NA SIYO YENU NA IWE SIYO ,MSIJE MKAANGUKIA
HUKUMU” YAKOBO 5:12
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
MUNGU AKUBARIKI SANA
KUJIFUNZA MANENO YA MUNGU
MAOMBI NA MAOMBEZI
WASILIANA NA
MCHUNGAJI LAURENT MPOMA
NCHI YA UKOMBOZI
MINISTRY
(HEMA LA MAOMBI NA
MAOMBEZI)
PHONE: +255714890889
WHATSAP:
+255762756542
TUMA MAHITAJI YAKO
LEO MCHUNGAJI ATAKUOMBEA NA KUKUPATIA USHAURI.
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
SOMA : (2 MAMBO YA NYAKATI 1:7: Usiku ule Mungu akamtokea sulemani,
akamwambia, omba utakalo nikupe).
Tunaupanuzi wa kiwanja cha kanisa ambacho kinahitaji
shilingi milioni tatu (3,000,000/=). Kiasi chochote tunapokea. MUNGU akubariki
sana kwa utoaji wako. Hakika Amini Mungu anakwenda kukutana na wewe kama
sulemani alivyotokewa usiku ule sasa ni zamu yako.
UNAWEZA KUTUMA HAPA
MPESA:
+255762756542……………..JINA: LAURENT MPOMA
TIGO PESA:
+255714890889…………JINA: LAURENT MPOMA
AIRTEL MONEY:
+255782859946…….JINA :LAURENT MPOMA
CRDB BANK:
0152363022800………LAURENT ELIAS MPOMA
NMB BANK:
50810025078……..LAURENT ELIAS MPOMA

0 Comments