MADHARA YA KUTUNZA
UCHUNGU KWENYE MOYO.
MITHALI 4:23 "Linda
sana moyo wako kuliko yote uyalindayo; maana huko ndiko zitokako chemchemi za
uzima" unaona, moyo haukuumbiwa kuingiza vitu, ila kutoa chemchemi za
uzima. Kwa mantiki hii, moyo unapoingiza vitu na vikakaa huko ndani, vitu hivyo
vinakuwa mzigo na kuanza kuharibu mfumo mzima wa utendaji kazi wake.
MITHALI 12:25
"Uzito katika moyo wa mtu huuinamisha; Bali neno jema huufurahisha"
kwa hiyo dalili ya kwanza kwamba moyo wako umeingiza vitu ambavyo havikustahili
na umeshindwa kuvibeba ni moyo kuwa mzito! Moyo unakuwaje mzito?
ISAYA 38:15b "Nitakwenda
polepole miaka yangu yote, kwasababu ya uchungu wa nafsi yangu" Nisikilize
itakusaidia, uzito ndani ya moyo hauwezi kuathiri moyo peke yake! Moyo ukiwa
mzito unaenda kuathiri pia mfumo wa akili, na mfumo wa akili ukiathirika na
mwili mzima unaathirika, check huyu mtu anasema nitakwenda polepole siku zote
za maisha yangu, kinachosababisha aende polepole ni uchungu uliomo moyoni
mwake.
Uchungu unapozidi moyoni na moyo ukaelemewa, moyo huanza
kusambaza uchungu huo mwilini kama sumu, kutokana na kushindwa kuhimili,
kwasababu moyo una kiwango cha kubeba vitu. Ndio maana utamkuta mtu akiwa na
uchungu mwingi moyoni kuna wengine huota vidonda mdomoni, hayo ni majibu ya
moyo kwamba, alo huku mimi nimezidiwa kwa hiyo kama kuna namna ya kuutoa mzigo
huu naomba uutoe.
Sasa unaweza kuelewa kwani Mungu anasema anatusamehe makosa
yetu kawaajili yake mwenyewe na si kwaajili yetu ISAYA 43:25, hii ni kanuni ambayo Mungu anataka kutufundisha kwamba
tusibebe mizigo ya chuki na uchungu mioyoni mwetu kwa kushindwa kusamehe,
kwasababu Mungu anajua athari za kutokusamehe na kutunza uchungu mioyoni mwetu!
Ndio maana anatufundisha kwamba, tunaposamehe ni kwa faida yetu wenyewe na wala
si ya wale tunaowasamehe.
Ningependa nizungumze mengi sana juu ya hili lakini kwa leo naomba niishie hapa! Kama unahisi shida za mwili wako ulizonazo kama vile magonjwa, na dalili nyingine nilizozitaja hapo juu vimesababishwa na uchungu moyoni mwako, na umeshindwa kabisa kusamehe, mwendee yesu kwa imani na umkabidhi mizigo hiyo sawasawa na MATHAYO 11:28-30 naye ni mwaminifu, atakutua mizigo hiyo na kukupa raha nafsini mwako. Ubarikiwe sana
MUNGU AKUBARIKI SANA
KUJIFUNZA MANENO YA MUNGU
MAOMBI NA MAOMBEZI
WASILIANA NA
MCHUNGAJI LAURENT MPOMA
NCHI YA UKOMBOZI
MINISTRY
(HEMA LA MAOMBI NA
MAOMBEZI)
PHONE: +255714890889
WHATSAP:
+255762756542
TUMA MAHITAJI YAKO
LEO MCHUNGAJI ATAKUOMBEA NA KUKUPATIA USHAURI.
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
SOMA : (2 MAMBO YA NYAKATI 1:7: Usiku ule Mungu akamtokea sulemani,
akamwambia, omba utakalo nikupe).
Tunaupanuzi
wa kiwanja cha kanisa ambacho kinahitaji shilingi milioni tatu (3,000,000/=).
Kiasi chochote tunapokea. MUNGU akubariki sana kwa utoaji wako. Hakika Amini
Mungu anakwenda kukutana na wewe kama sulemani alivyotokewa usiku ule sasa ni
zamu yako.
UNAWEZA KUTUMA HAPA
MPESA: +255762756542……………..JINA: LAURENT MPOMA
TIGO PESA: +255714890889…………JINA: LAURENT MPOMA
AIRTEL MONEY: +255782859946…….JINA :LAURENT MPOMA
CRDB BANK: 0152363022800………LAURENT ELIAS MPOMA
NMB BANK: 50810025078……..LAURENT ELIAS MPOMA
0 Comments