SOMO: KUOMBEA HALI YA KIROHO YA ARDHI ILI UFANIKIWE KIMAISHA.
Kuna uhusiano sana kati ya ardhi na mafanikio yako kwa hiyo ni muhimu
sana kulifuatilia kwa karibu sana somo hili
MFANO WA KWANZA
Mwanzo 3:17-19
"Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke
wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi
imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha
yako; michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni; kwa jasho
la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo
ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi"
Laana maana yake ni
>>>Kutostawi
>>>Kutofanikiwa
>>>Kutokuwa na Furaha
>>>Kutofikia kiwango cha mafanikio ambacho Mungu
kakikusudia kwa ajili yako. Na Laana ni kinyume cha baraka.
Mungu aliposema ardhi imelaaniwa alikuwa anataka kumuambia
Adamu kuwa ukitaka kujua kitu gani umebeba kwa kutofuata maelekezo yangu kuwa
kuna laana iliyoko kwenye maisha yako na utakapoilima ardhi haitakuzalia
matunda yake.
MFANO WA PILI
Mwanzo 4:11-12
"Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua
kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako; utakapoilima ardhi
haitakupa mazao yake; utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani."
Laana ya hapa sura ya nne ni tofauti na ile sura ya tatu kwa
sababu laana ya Adamu ilikuwa ndani ya Adamu lakini katika sura ya nne tunaona
kuwa laana ipo kwenye ardhi moja kwa moja.Maana yake kwa kila mtu atakaye
kanyaga eneo hili anapata ile laana iliyoachiliwa kwenye ardhi .
MFANO WA TATU
2 Mambo ya Nyakati 7:11-14
"Nikizifunga mbingu isiwe mvua, tena nikiamuru nzige
kula nchi, au nikiwapelekea watu wangu tauni; ikiwa watu wangu, walioitwa kwa
jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia
zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya
nchi yao"
Uponyaji tunaoungalia hapa ni uponyaji wa ardhi na nchi ni
ardhi yenye mipaka halali ya kiumiliki,biblia inaposema kuwa nchi maana yake ni
ardhi na sio watu au taifa. Taifa ni ni kundi la watu waliokubaliana na mfumo
wa uongozi na wakae kwa pamoja. Kwenye biblia unaona kabila linageuka kuwa
Taifa au familia kuwa taifa. (Angalia katika Kitabu cha Mwanzo 49)
Mwanzo 49:1,28
"Yakobo akawaita wanawe, akasema, Kusanyikeni, ili
niwaambie yatakayowapata siku za mwisho.Hizo zote ndizo kabila za Israeli kumi
na mbili. Na hayo ndiyo aliyowaambia baba yao, na kuwabariki; mmoja mmoja kwa
mbaraka wake aliwabariki"
Hapa biblia haizungumzii uponyaji wa watu bali ni ardhi
.Biblia inasema tena nikiamuru nzige kula nchi maana nzige ni wadudu waharibifu
na wanaoharibu mazao au udongo na Tauni ni ugonjwa wa kuambukiza na kibiblia
ikitokea ugonjwa wa kuambukiza ina maana kunakuwa na shida kwenye ardhi.
Ukitokea ugonjwa wa kuambukiza katika eneo fulani huwa
wanaweka karantini na kufunga mipaka. Kitendo cha kuweka mpaka ni Roho
Mtakatifu anawajulisha kuwa shida hii imeishia mpaka hapa.
Suala hili la kufunga mipaka ili kuzuia maambukizo ya
ugonjwa ni ya kiroho kwanza kabla hayajawa ya kimwili.
MFANO WA NNE
Yeremia 22:29-30
"Ee nchi, nchi, nchi, lisikie neno la Bwana. Bwana
asema hivi, Andikeni habari za mtu huyu kwamba hana watoto, kwamba mtu huyu
hatafanikiwa siku zake zote; maana hapana mtu katika wazao wake
atakayefanikiwa, akiketi katika kiti cha enzi cha Daudi, na kutawala tena
katika Yuda."
Huyu ni Mungu anazungumza na nchi (ardhi yenye mipaka halali ya
kiumiliki) anaposema
>>>Ee nchi ,nchi sikia ---- ina
maana nchi inasikia
>>>Andika maana yake inaweza
tunza kumbukumbu
>>>Kuwa hatafanikiwa maana yake
ni kuwa inaweza fuatilia
Wakati adhabu inatolewa kwa mtu huyu alikuwa bado hana
watoto, lakini kumbukumbu iliandikwa kwenye ardhi kuwa hata watoto wake wakija
nao wasifanikiwe. Adhabu ilitolewa kwa sababu gani; angalia mstari wa 21 Mimi
nalisema nawe wakati wa kufanikiwa kwako; lakini ulisema, Sitaki kusikia. Hii
ndiyo iliyokuwa desturi yako tangu ujana wako, kutokuitii sauti yangu.
Fikiria wewe ni mtoto na umeingia kwenye adhabu ya baba au
mama na unatafuta kufanikiwa na haufaninikiwi sio kwamba akili huna bali unazo
lakini umezuiliwa kufanikiwa na ardhi kwa sababu ya kosa la baba yako na mama
yako je unaombaje?
Mwanzo 28: 10-20
"10-13"Yakobo akatoka Beer-sheba , kwenda harani.
Akafika mahali Fulani akalala huko usiku kucha , maana jua lilikuwa limekuchwa
,akatwaa jiwe moja la mahali pale akaliweka chini ya kichwa chake , akalala
usingizi palapale. Akaota ndoto, na tazama ngazi imesimamishwa juu ya nchi, na
ncha yake yafika mbinguni .Tena tazama malaika wanapanda na kushuaka juu ya
yake. Na tazama Bwana amesimama juu yake , akasema mimi ni Bwana, Mungu wa
Ibrahim baba yako na Mungu wa Isaka , nchi hii uilalayo ntakupa wewe na uzao
wako"
Lile Neno nchi hii ulalayo Kwa lugha nyingine ardhi unayolala iwe ni nyumba uliyojenga au hoteli au umejilaza mahali kwa muda mfupi au ni kwenye basi umelala au uko shambani umelala na ghafla unaota ndoto, sio kila mahali angeweza kulala ila eneo lile lilikuwa na umiliki kamili wa Mungu.
MUNGU AKUBARIKI SANA
KUJIFUNZA MANENO YA MUNGU
MAOMBI NA MAOMBEZI
WASILIANA NA
MCHUNGAJI LAURENT MPOMA
NCHI YA UKOMBOZI
MINISTRY
(HEMA LA MAOMBI NA
MAOMBEZI)
PHONE: +255714890889
WHATSAP:
+255762756542
TUMA MAHITAJI YAKO
LEO MCHUNGAJI ATAKUOMBEA NA KUKUPATIA USHAURI.
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
SOMA : (2 MAMBO YA NYAKATI 1:7: Usiku ule Mungu akamtokea sulemani,
akamwambia, omba utakalo nikupe).
Tunaupanuzi
wa kiwanja cha kanisa ambacho kinahitaji shilingi milioni tatu (3,000,000/=). Kiasi
chochote tunapokea. MUNGU akubariki sana kwa utoaji wako. Hakika Amini Mungu
anakwenda kukutana na wewe kama sulemani alivyotokewa usiku ule sasa ni zamu
yako.
UNAWEZA KUTUMA HAPA
MPESA: +255762756542……………..JINA: LAURENT MPOMA
TIGO PESA: +255714890889…………JINA: LAURENT MPOMA
AIRTEL MONEY: +255782859946…….JINA :LAURENT MPOMA
CRDB BANK: 0152363022800………LAURENT ELIAS MPOMA
NMB BANK: 50810025078……..LAURENT ELIAS MPOMA
0 Comments