MCHUNGAJI LAURENT MPOMA
NCHI YA UKOMBOZI MINISTRY SINGIDA TANZANIA
(NENO, MAOMBI NA MAOMBEZI)
MITHALI
18:21 "Kifo na uzima viko katika nguvu za ulimi.Naye
anayeupenda kuutumia atakula matunda yake" Kabla ya maombi haya hakikisha
umeomba msamaha kwa mtu yeyote uliyemkosea na pia kusamehe mtu yeyote
aliyekukosea.
Mungu mwenyewe ni msamaha na atakusamehea tu kama nawe
utasamehea wabaya wako. Husipotoshwe na mtu yeyote akakwambia kuwa maombi ya
mtu aliyeokoka yatajibiwa sawasawa na ya mtu anayemkataa Yesu,huo ni uongo
mtupu;kwani maombi ya mwokovu husikizwa sana na Mungu.
Huu ni mwelekeo tu
wa kufuta laana/mabaya ulonenewa na wakwendeaye kinyume.(Mtu uliyemchukulia
mumewe si m-baya wako wewe ndiye mbaya wake) Maombi. " Baba wa mbinguni
katika Jina la Yesu Kristo nakushukuru kwa wema na wokovu ulionipa mimi mwanao.
Asante kwa kunipa ufunuo wa kuyajua haya ambayo yamekuwa vikwazo vya kubarikiwa
kwangu. Nisamehe dhambi na makosa niliyokutenda na niliyowatenda wanadamu.
Isaya 1:18 unasema hata dhambi
zangu ziwe nyekundu utanisafisha na kunisamehea.Baba wa mbinguni nisamehe.
Ninafuta kila neno mbaya nililonenewa na wabaya wangu,nikanenewa na wachawi
wakasema sitabarikiwa.Nalifuta neno hilo kwa damu ya Yesu Kristo katika Jina la
Yesu kristo na ninabadilisha laana yao na kuwa baraka kwangu katika Jina la
Yesu. Kila neno ovu la kunifunga lililotamkwa kwa kazi yangu nalifuta kwa damu
ya Yesu Kristo. Aliyeninenea kushindwa nimelifuta neno hilo na kuandika
kushinda katika maisha yangu katika Jina la Yesu Kristo.
Kila neno la kinywa la kushindwa nililojitamkia mwenyewe
nalifuta kwa damu ya Yesu Kristo. Kila laana niliyotamkiwa na wanadamu naifuta
na kuitamka baraka kuanzia sasa katika Jina la Yesu Kristo. Kila neno la
kufunga ndoa yangu,mume wangu,mke wangu,boma letu,utajiri wetu ninalifuta na
kuandika baraka katika Jina la Yesu Kristo. Kutoka sasa nimefunguliwa kutoka
kwa maneno ya kutamkiwa na niko huru. Najifunika kwa damu ya Yesu Kristo kutoka
sasa hakuna tamshi mbaya litakalonipata. Katika Jina la YESU nimeomba na
nimefunguliwa, AMEN."
<<<<<<<<<<<Mungu akubariki sana>>>>>>>>>
TUMA MAHITAJI YAKO NA MCHUNGAJI ATAKUOMBEA
+255714890889
WHATSAP: +255762756542
FACEBOOK: nchi ya ukombozi ministry
YOUTUBE: Chuma Cha Mungu Tv
0 Comments