Follow us

MAMBO 7 YANAYOZUIA MAFANIKIO YAKO.

Tangazo

 


MAMBO 7 YANAYOZUIA MAFANIKIO YAKO.

1.Tabia yako ya kujilinganisha na watu.

 Kamwe Usilinganishe mapambano yako ya maisha na ya mtu mwingine yeyote, na usikatishwe tamaa na mafanikio ya watu wengine. tengeneza njia yako mwenyewe katika mapambano yako kwa kujihamsisha mwenyewe na kutokukata tamaa. usisahau kuishi kulingana na kipato chako.

2. Tabia yako ya kutokujiamini.

Kujiamini ni pale unapoamini kuwa una uwezo wa kipekee Tofauti na mtu mwingne. Unapojiamini unaupatia nguvu uwezo uliopo ndani yako ambao utakuwezesha Kufanya mambo makubwa zaidi Katika maisha yako.Ikiwa hutojiamini utazui hali yako ya uthubutu wa kujaribu katika kufanya Mambo kwa ajili ya mafanikio yako.

3. Marafiki wanaokuzunguka.

Mhenga mmoja aliwahi kusema "Nionyeshe rafiki yako nami nitakuambia jinsi ulivyo". akiwa na maana ya kuwa wewe ni mtu wa 5 katika idadi ya marafiki zako wa karibu wanaokuzunguka.

  Ikiwa una marafiki 4 wavivu na wewe utakua mvivu wa 5. Ikiwa una marafiki 4 wambea na wesengenyaji na wewe utakuwa mbeya na msengenyaji wa 5. Ikiwa utakuwa na marafiki wa 4 walalamikaji na wewe utakuwa mlalamikaji wa 5.

4. Tabia yako ya kuishi bila malengo.

Uwezo wako wa kuwejiwekea malengo ndio ustadi wako  mkuu wa mafanikio yako. Malengo yako hufungua akili yako chanya na hutoa mawazo yenye nguvu kwa ajili ya kufikia malengo uliyojiwekea. Ikiwa utaishi kwa malengo mafanikio yako yatapatikana hatua kwa hatua. Na itakusaidia kuongeza umakini wako katika kila unachokifanya tena kwa kutokupoteza mda wako.

5. Tabia yako ya kuairisha mambo.

Tabia yako ya kujisemea kuwa "Nitafanya kesho" kwa kile ambacho ulipaswa ukifanye leo, Ni miongoni mwa mambo yanayozuia mafanikio yako. Chochote unachotaka kukifanya, kifanye leo. Kwasababu, kesho unayoisubiria haitofika ina kesho yake pia.

6. Tabia yako kutokukubali kushindwa nakuchukulia kama mafunzo.

Unapojiandaa vya kutosha katika kila unachokifanya, ni lazima ujifunze kuwa kutakuwa na wakati utafanikiwa, na kutakuwa na wakati utashindwa, nyakati zote hizi mbili ni muhimu. Ikiwa wakati wa kushindwa utatokea basi usikate tamaa bali utumie wakati huo kujifunza ni wapi umekosea na uanze upya.

7.Tabia yako ya kujidharau kwa kujiwazia mabaya.

Vile unavyofikiri na kuwaza ndivyo inavyokua au kutokea, hupaswi kujidharau kwa kujiwazia vibaya au kwa kuhofia maneno ya watu kupitia kile unachokifanya,  au kushindwa kwako. Amini kuwa wewe ni wakipekee na una NGUVU na uwezo mkubwa ndani yako ulio pewa na Muumbaji wako. hakuna mwingine kama wewe katika dunia hii na hatotokea.

     UKIAMINI KATIKA MUNGU, HAKUNA LINALOSHINDIKANA

Post a Comment

0 Comments