Mapenzi ya Mungu ni kila muumini, mmoja mmoja, akue na kufika katika kiwango
cha imani, nguvu na neema aliyokuwa-nayo BWANA wetu Yesu Kristo. Ndio maana “…
alitoa wengine kuwa Mitume, Manabii, Wachungaji, Wainjilisti na Waalimu, kwa
kusudi la kuwakamilisha watakatifu [wote], ili mwili wa Kristo [Kanisa]
ujengwe, hata na sisi sote [kama waumini], tukue na kufika katika kimo cha
utimilifu wa Kristo, ili tusiwe watoto wachanga … ili tusiwe tena watoto
wachanga, tukitupwa-tupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu,
kwa hila za watu [na] kwa ujanja, … lakini tuishike kweli katika upendo na
kukua, hata tumfikie Yeye, katika yote, Yeye aliye kichwa, yaani Kristo ”
(Efeso 4:11-15).
Lakini watoto wa Mungu wengi wamekuwa wavivu katika kumtafuta Mungu na
kukua katika imani (Waenrani 5:11-14), ndio maana BWANA Yesu anawagombeza sana
wanafunzi wake kwa kushindwa kumtoa pepo (Mathayo 17:14-21). Hali hiyo
inawahusu wanafunzi wengi wa Yesu wa leo. Hali hiyo inamhuzunisha sana Yesu
mpaka leo. Katika semina hii, tulijifunza namna ya kukua katika imani, neema na
nguvu za Mungu, ili tusitawaliwe na mazingira, bali sisi ndio tuyatawale
mazingira yote kwa ushindi na mafanikio. Unaweza kupata mafundisho haya kwa
kuweka ‘order’ katika duka la mtandanoni, sehemu ya chini ya ukurasa huu. Jina
la CD/DVD hii ni Jifunze Vita Kiroho. Nakutakia neema ya Mungu ya kukua na
kuongezeka katika imani, neema na nguvu (Rum 1:17, Yoh 1:17, Zab 84:1-7 na 2Kor
3:18).
Maombi na maombezi
piga: 0714890889

0 Comments