Follow us

SOMO :MAOMBI YA KUFUTA VIAPO VYOTE VINAVYOFANYA KAZI KINYUME NA MAISHA YAKO

Tangazo

MCHUNGAJI LAURENT MPOMA
NCHI YA UKOMBOZI MINISTRY
(HEMA LA MAOMBI NA MAOMBEZI)

MAOMBI YA KUFUTA VIAPO VYOTE VINAVYOFANYA KAZI KINYUME NA MAISHA YAKO

Kiapo ni maneno yaliyotamkwa yanayoweza kuleta laana juu ya mtu au familia.

Kiapo kinaweza kumfunga mtu kwa lile jambo alilolijiapiza Au Aliloapizwa .

Mtu anasema Naapa kuwa Sitakuacha Mpaka kifo baada ya Muda anaanza kutoka Nje ya ndoa Madhabahu na kiapo Kina Mshuhulikia

Mtu Yuko kwenye Mahusiano wanaapizana Mimi Sitaolewa na mtu Mwingine Tena na Mimi sitaoa mtu mwingine tena mwisho wa siku Mahusiano yanavunjika na anataka Kuolewa au Kuoa anasahau kuna Kiapo alishaapa

Yoshua 6:26-27 “Naye Yoshua akawaapisha kiapo wakati ule, akasema, Na alaaniwe mbele za Bwana mtu yule atakayeinuka na kuujenga tena mji huu wa Yeriko; ataweka msingi wake kwa kufiliwa na mzaliwa wa kwanza wake, tena atayasimamisha malango yake kwa kufiliwa na mtoto wake mwanamume aliye mdogo.Basi Bwana alikuwa pamoja na Yoshua; sifa zake zikaenea katika nchi ile yote.”

Aliwaapisha kwasababu hakuweza kuwaacha hivihivi ili mtu asije kujenga tena Yeriko na akijenga atafiwa. Kiapo kinaendana na taratibu zake na huyu anayekuapisha anasema ukifanya hivi na hivi yatakupata haya.

Siku hizi utakuta familia kila mwaka anakufa mtu maana yake kuna viapo vya kifamilia. Ukirudi nyuma miaka ya nyuma tulikua hatumjui Mungu hivyo wazazi wetu walikua wanafanya viapo kwa miungu na mashetani, viapo vile vimefata familia zetu mpaka leo hii.


ZAIDI INGIA HAPA>>>nchiyaukomboziministrytz.blogspot.com

AMINA SANA MUNGU AKUBARIKI SANA

TUMA MAHITAJI HAPA NA MCHUNGAJI ATAKUOMBEA.

0714890889

YUOTUBE: Upenyo Wa Mungu Tv

Post a Comment

0 Comments