1. KUKAA NDANI YA KRISTO.
Ni ngumu kuishi nje y mzabibu na kuzaa matunda hivyo ili
maombi yako yapate majibu lazima ukubali kuishi ndani ya wigo na uongozi wa
kumkubari Kristo na yeye kuwa sababu ya matokeo yako unayohitaji kupitia
maombi.Kuwa ndani ya wigo kutakufanya usiwe kinyume nq yale maelekezo anayotoa
Yohana 15:7
7 Ninyi mkikaa ndani yangu na maneno yangu yakikaa ndani
yenu, ombeni lo lote mtakalo nanyi mtatendewa.
2. Imani ni moja ya mambo saba ambayo ukiwa huna huwezi kupata
majibu sawasawa na unacho omba na wakati mwingine kutindikiwa na imani hufanya
maombi kuharibika na kubaki ukisubiri kitu ambacho imani yako ilishatindika.
Matayo 14:26-28
26 Lakini wanafunzi wake walipom wona akitembea juu ya
maji, waliingiwa na hofu kuu. Wakasema, “Ni mzimu.” Wakapiga mayowe kwa hofu.
27 Lakini mara moja Yesu akasema nao, akawaambia, “Jipeni moyo. Ni mimi;
msiogope.”
28 Petro akamjibu, “Bwana, kama ni wewe, niambie nije
kwako nikitembea juu ya maji.
Kupunguka kwa imani ya Peter ndipo kulipoleta ule uzamaji
wake ukisoma mistari ya hapo chini.Hivyo Mungu qnaweza kutoa jibu la maombi
yako ila kinachoharibu ni baada ya wewe kuanza kuwaza yale nilioomba kweli
Mungu atafanya?basi unasababisha malaika aliyekua ametumwa kuleta taarifa zenye
tumaini kurudi mbinguni.imani ikipung7q qu kuweka tashwishwi basi ni moja ya
kufanya kile tunachokiomba kisitoe majibu.
Waebrania 11:6
6 Na pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu kwa maana
kila mtu anayemjia ni lazima aamini kuwa yupo na kwamba yeye huwapa tuzo wale
wanaomtafuta kwa bidii.
Marko 11:24
Kwa hiyo nawaambieni, mnaposali na kuomba kitu, aminini
kwamba mmekipokea, nanyi mtapewa.
Ukiweka shaka basi tayari unachafua na kuharibu maombi
yako.
3. OMBA KATIKA ROHO.
Kuomba kusiko na kikomo huomba kuliko na
uendelevu,ukimruhusu roho mtakatifu akufundishe namna ya kuomba huwezi kuacha
kuomba kila muda hata umelala utashangaa unaomba katika roho,hauchoki na hii
inakua constantly,mtumishi mmoja anasema kuomba Yesu alijua lazima kila mkristo
aombe ila kule kunakoleta majibu ni kudumu kutika kuzungumza na Mungu sababu
kila unapomkumbusha nini unahitaji ni rahisi kupewa kile kilichobora.
Waefeso 6:18
Salini daima, mkiomba msaada wa Mungu. Salini kila wakati
kwa nguvu ya Roho. Kesheni bila kuchoka mkisali kwa ajili ya watu wote wa
Mungu.
Ukiweka limitations katika kumtafuta Mungu basi nayeye
ataweka limitations pia hivyo hebu kuomba kwetu kunakoleta majibu sio mpk
watumishi humu ndani wasema maombi wakati mwingine ona maisha yangu kama mjori
wa Kristo nahitaji kumtafuta Mungu.kuna vitu haviwi vyetu kama
hatujavilazimisha kuwa vyetu kujenga utarstibu au mazoea ya kuongea na mpenzi
Yesu.
Nguvu ya roho: hii nimeona mara nyingi kwa upande wangu
najua hata kwako unaiona umelala unashituka unakuta ulikua unaomba rohoni na
kuna muda unashangaa umeshurutishwa kuomba sio kwa kuzungumza bali kwa moyo
hutoi maneno ila unaomba na unaona unahitaji kuwa katika hali hio kwa muda
mrefu.kikawaida unaweza usielewe ila Roho Mtakatifu kuna mambo anakuvusha na
anakupa ushindi kwa kisemo rahisi wa goli la mkono bila kutumia nguvu nyingi.
4. KUSIMAMA KATIKA KATIKA NENO.
Maombi yako ili yapate kujibiwa yanahitaji neno la
Mungu,umewekeza nini unachokijua juu yako mbele za Mungu ukitumie kukidai,je
haki zako unazifahamu na unazitumiaje kuomba.
Zaburi 119:105-106
Neno lako ni taa ya kuniongoza, na mwanga katika njia
yangu. Nimeapa na kuthibitisha kiapo changu, kwamba nitashika maagizo yako
adili.
Neno litasimama kukutengeneza au kukuelekezq nini
unapashwa kuomba mbele za Bwana
Niliwahi kusikiliza ushuhuda wa mtu anasema kuna maombi
yanahitaji majibu ya papo kwa papo na kuna yale yanahitaji muda ili kutokea
hivyo yale yanayotokea papo kwa hapo basi yasikufanye unapoomba maombi ya
kutokea baada ya miaka 10 yakufanye usiamini Mungu atajibu,jambo zuri ni kuishi
ndani ya neno na kutokutoka kwenye kile ulichoomba na kuamini utapokea.
5. UWE MTU MWENYE KUSHUKURU.
Kuna mambo Mungu anatufanyia bila kumuomba basi hata kwa
hayo tuwe na neema ya kumshukuru maana katika yale mambo madogo ayafanyayo basi
kutafanya kuyanyunyiza yale mambo makubwa kutokea.
Mathayo 11:25-26
Wakati huo Yesu alisema, “Nakushukuru ee Baba, Bwana wa
mbingu na dunia, maana umewaficha wenye hekima na wenye elimu mambo haya, ukawafunulia
wadogo. Naam, Baba, ndivyo ilivyokupendeza.
Kuna mambo hayafiki sababu hujajua namna ya kumshukuru
Mungu hebu mrudishie utukufu kwa vile alivyofanya kwako na kwa ule umbali
aliokutoa ili vile vilivyokua vimesubiria wewe kushukuru viachiliwe
Kuna watu sio tu hawajui kumshukuru Mungu hata watu
waliofanya vitu kwenye maisha yao hawajawahi kuwambia asanteh hivyo inawawia
ungumu kujua kama huyu mtu alifurahia vacation niliyompa au extra bonus ya
mshahara wake niliyoongeza hakupenda?ndoa nyingi zinaonekana za kizamani sababu
baadhi ya wanandoa wanasahau asanteh ndio siraha ya kufichua hazina zingine
kutoka kwa wenzi wao.
6. UWE NA KAZI UNAFANYA.
Katika utekelezaji wowote wa maombi yanahitaji mtu awe na
kitu ili kupitia kile anachoomba kibarikiwe na kifike kule wewe muombaji
unaomba.Kuna watu wanaomba kuwa wafanyabiashara wazuri wakati hata mtaji wa
kuuzq karanga hana unampa kazi Mungu ya kuangalia aanze wapi kukubariki,maombi
yanahitaji utendaji huwezi kutaka kuwa mtu fulani bila kuwepo na maandalizi.Anahitaji
abariki uimbaji wako anza kuimba ainue watu watakaokaa upande wako watembee na
wewe,unahitaji gari basi uwe na mradi unaoweza kukupa milioni 10 au zaidi
kutokana na kile unachohitaji,wengi tumebaki kuamini katika miujizq na kusahau
kufanya kazi.
2 Wathesalonike 3:6-8
Onyo Kuhusu Uvivu
6 Ndugu wapendwa, katika jina la Bwana Yesu Kristo, tuna
waagiza mjitenge na kila ndugu ambaye ni mvivu na ambaye haishi kufuatana na
maagizo tuliyowapeni. 7 Maana ninyi wenyewe mnafa hamu jinsi mnavyopaswa kuiga
mfano wetu. Sisi hatukuwa wavivu tulipokuwa nanyi 8 wala hatukula chakula cha
mtu ye yote pasipo kulipa. Bali tulifanya kazi kwa juhudi usiku na mchana ili
tusimlemee mtu ye yote kati yenu.
Katika maombi mengi tunayoomba yamejaa uhitaji hivyo ili
kufullfill uhitaji wetu lazima tufanye kazi tusiwe wavivu kuwaza miujiza only
doing work gives us, our aspects of living.Hivyo ni vizuri kuwa na jambo
unafanya ili kile unachoomba kisione hata wewe muombaji unaupungufu
sehemu.baraka zinatazama nini unacho kwa ajiri ya kuikamilisha baraka ya kile
ulichoomba
7. KUISHI MAISHA YALIYOJAA UPENDO.
Kuna watu wanaomba masaa ya kutosha lakini kwa habari ya
upendo kuwatendea wengine hawana,na ubaya mkubwa wamejaa kisasi na
kutokuachilia.Maombi unayoomba hayawezi kuleta impact yoyote kama huwezi
kuuapply upendo kwa watu.
1 Wakorintho 13
Upendo
13 Kama ningekuwa na uwezo wa kusema kwa lugha za
wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa kama kelele ya kengele au
toazi. 2 Na kama nina uwezo wa unabii, na kuelewa siri zote na maarifa yote; na
hata kama nina imani kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, mimi
si kitu. 3 Kama nikitoa mali yote niliyo nayo, na kama nikitoa mwili wangu
uchomwe moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu.
4 Upendo huvumilia, upendo hufadhili; upendo hauna wivu
au majivuno.
5 Upendo hauna kiburi na haukosi kuwa na adabu. Upendo
hau tafuti kujipendeza nafsi; haukasiriki upesi, hauweki orodha ya mabaya. 6
Upendo haufurahii mabaya, bali hufurahia kweli. 7 Upendo huvumilia yote,
huamini yote, hutumaini yote, hustahim ili yote.
8 Upendo hauna mwisho. Lakini penye unabii, utakoma;
zikiwepo lugha zitakoma; yakiwepo maarifa yatakwisha.
Unaweza kuomba na kufanya mambo mengi yaliyo ya haki
lakinj bado ukishindwa kuwa mtu wa upendo bado huwezi kujibiwa
unachokiomba,upendo huambatana na kusamehe ukishindwa kupenda basi hata
kusamehe kwako kunakua shida.
Mt 18:22
Yesu akamwambia, Sikuambii hata mara saba, bali hata saba
mara sabini.
Yesu alijua wengi kusamehe ni ngumu hivyo alisema kuwa
watu wenye kusamehe ili kusababisha yale yafungwayo kwa kutokusamehe yasiwe
kwazo kwetu.
KAMA UKO NJE YA SINGIDA MJINI TUMIA NAMBA HIZI KUTUMA MCHANGO WAKO.
TIGO PESA 0714890889....................JINA: LAURENT MPOMA
M -PESA 0762756542.......................JINA: LAURENT MPOMA
AIRTEL MONEY - 0782859946.......JINA: LAURENT MPOMA
Mchungaji Kiongozi Laurent Mpoma atakuombea moja kwa moja na Mungu wa mbinguni atakuponya na kukurejeshea na kukuvusha kwenye hilo unalopitia.
BARIKIWA SANA.

0 Comments