SOMO : MAANA YA PASAKA
Pasaka ya Kikristo ni sikukuu ambayo Wakristo karibu wote
hufanya kila mwaka ukumbusho wa kufufuka kwake Yesu Kristo siku ya tatu baada
ya kusulubiwa,
Pasaka ni sherehe ya Kiyahudi iliyowakumbusha jinsi Mungu
alivyowakomboa Waisraeli kutoka katika utumwa wa Misri mwaka wa 1513
»Neno "Pasaka" linatokana na neno la kiebrania
"PESACH" kwa kiingereza ni
lenye maana "PASS OVER" yaani "KUPITA JUU YA".
»Mwanzo wa Pasaka ulikuwa ni wakati wa nabii Musa (KUTOKA
12:14,17-18,21, KUTOKA 13:3-4; HESABU 9:21-30).
»Pasaka ni tendo la Bwana kupita juu ya nyumba za wana wa
Israeli huko Misri, pale alipoiona damu ya mwanakondoo wa Pasaka katika
vizingiti vya juu na miimo miwili ya milango yao alipita juu na kuacha
kuwaharibu. Walioharibiwa walikuwa ni Wamisri ambao alama ya damu haikuonekana
katika nyumba zao (KUTOKA 12:21-30).
»Mungu aliwaagiza wana wa Israeli kuikumbuka siku hii.
»Siku kuu hii ya Pasaka ilifanyika kuwa kumbukumbu kila
mwaka katika mwezi wa Kiyahudi unaoitwa " NISAN" (NEHEMIA 2:1)
au "ABIB" (KUTOKA 13:3-4).
Siku kuu hii ilifanyikwa kwa juma moja yaani siku ya 14 hadi siku ya 21.(KUTOKA
12:14,17-18; HESABU 9:1-5).
»Mwezi wa
"NISAN" au "ABIB" katika kalenda yetu ni kati ya mwezi
"MARCHI" na "APRILI". Kuanza kwa mwezi ABIB kunategemeanana
mwandamo wa mwezi . Ndiyo maana tarehe za siku kuu ya Pasaka hubadilika kila
mwaka, Lakini huwa ni kati ya mwezi Marchi na Aprili.
»Katika kusherekea siku kuu hii walihitajika kuchinja
wanyama wengi sana ili kupata damu kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa kama
ondoleo la dhambi. Kwa wastani katika kipindi cha Pasaka walichinjwa wanyama
256,500 (laki mbili hamsini na sita elfu na mia tano).
»Katika kusherehekea Pasaka, Wayahudi walifanya mkutano
mkubwa au konferensi ambapo
walikusanyika pamoja na kula na kunywa na kuwa na muda mrefu wa kulisikia Neno
la Mungu.
»Siku kuu hii iliendelea hadi katika kipindi cha Yesu
Kristo. Yesu kristo mwenyewe alikuwa akienda kusherekea Pasaka(LUKA 2:41-52;
YOHANA 2:13,23).
»Hiki kilikuwa ni kivuli cha Yesu Kristo kama mwanakondoo wa
Pasaka aliyechinjwa msalabani.
»Yesu kristo alitolewa kusulubishwa wakati wa pasaka kama
Pasaka wetu(YOHANA 18:39, 19:14-18; 1 WAKORINTHO 5:7). Kwa sababu hiyo, sasa
hatuna haja ya kuchinja wanyamatena kama sadaka bali ni kumwamini Yesu ambaye
ndiye sadaka yetu.
»Kila amwaminiye Yesu Kristo kwa Imani tu, damu ya Yesu
hunyunyizwa juu yake na kuoshwa dhambi zote na kuwa salama(1 PETRO 1:2). Sasa
hakuna haja tena ya kuchinja wanyama.Sasa tunaingia patakatifu pa
Bwana(hekaluni) kwa damu ya Yesu(WAEBRANIA 10:19). Shetani ni Mharibu lakini
hawezi kumharibu yeyote aliyenyunyiziwa damu ya Mwanakondoo (1 PETRO 1:2;
UFUNUO 12:11).
»Kila asiyemwamini Yesu ghadhabu ya Mungu inamkalia,
amekwisha hukumiwa (YOHANA 3:3,16-18). Kwa jinsi hiyo basi, ni busara mtu
kusherehekea Pasaka pale tu ambapo amekwisha nyunyiziwa damu ya Yesu na
kumshinda Shetani. Kinyume cha hapo, ni kufanya mchezo wa kuigiza(YOHANA
1:35-36, 10:10).
<<<<<MUNGU AKUBARIKI SANA>>>
MAOMBI NA MAOMBEZI
WASILIANA NA MCHUNGAJI LAURENT MPOMA
PIGA SIMU AU WHATSAP +255762756542
YOUTUBE: “NCHI YA UKOMBOZI TV”
0 Comments