Follow us

NGUVU YA MAOMBI YATOKANAYO NA MUNGU MWENYEWE

Tangazo

 


NGUVU YA MAOMBI YATOKANAYO NA MUNGU MWENYEWE

Mathayo 7:7 Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa.

Kinyume chake ni kuwa usipoomba hauwezi kupewa kitu hivyo kwa mwana wa Mungu anayehitaji kukua kila siku kiroho na kimwili anapaswa kuwa muombaji.

Aina hizo za maombi ni kama ifuatavyo

1.MAOMBI YA AKILI

Haya ni maombi ambayo mtu anapanga vitu ambavyo anahitaji Mungu amtendee na anakwenda navyo kwenye maombi yake

Mtu anaweza akawa anahitaji Mungu ampe Mme au mke mwema, ajira, kibali n.k kwahiyo anavipangia mda wa kuviombea vipaumbele hivi

Zaburi 5:3 Bwana, asubuhi utaisikia sauti yangu, Asubuhi nitakupangia dua yangu na kutazamia.*

Kwa maana nyingine unamuita Mungu muumbaji ili akusaidie mambo yako uliyoshindwa kwa akili zako na nguvu zako

Zaburi 57:2 Nitamwita MUNGU Aliye juu, Mungu anitimiziaye mambo yangu.

Kwahiyo utaona yakwamba haya ni maombi yatokanayo na akili za mtu.

Lakini kuna aina nyingine ya maombi ambayo kimusingi ndiyo yaliyobeba Ujumbe huu

2.MAOMBI YATOKANAYO NA MUNGU MWENYEWE*

Haya ni maombi yanayokuja nje ya ratiba na vipaumbele vya mtu

Yaani mtu anajikuta anaombea kitu ambacho hakukipanga tena wakati mwingine kwa mda ambao hakupanga aombe

Kibiblia aina hii ya maombi inatambulika pia kama

Maombi ya roho*

Au maombi ya kinabii*

Biblia inasema nitaomba kwa roho tena nitaomba kwa akili pia

1 kor 14:15 Imekuwaje, basi? Nitaomba kwa roho, tena nitaomba kwa akili pia; mtaimba kwa roho, tena nitaimba kwa akili pia.

Kwahiyo kuna maombi ya akili na maombi ya roho

Maombi ya roho ni maombi yatokanayo na Mungu na haya ndiyo maombi yenye nguvu maana yanagusa kwenye kiini cha maisha ya mtu moja kwa moja

Maombi ya roho ni maombi yenye uvuvio maalumu wa Roho mtakatifu, mtu anajikuta anabubujika rohoni kwaajili yake au wengine.

 >>>>>MUNGU AKUBARIKI SANA>>>>


MAOMBI NA MAOMBEZI

TMA MAHITAJI HAPA

0762756542

WHATSAP 0762756542

 

 

 

 

 

 

 

Post a Comment

0 Comments