MAOMBI YA KUFUTA MANENO LAANA ULIYONENEWA JUU YAKO.
MITHALI 18:21 "Kifo na uzima viko katika nguvu za
ulimi.Naye anayeupenda kuutumia atakula matunda yake"
Kabla ya maombi haya hakikisha umeomba msamaha kwa mtu
yeyote uliyemkosea na pia kusamehe mtu yeyote aliyekukosea.
Mungu mwenyewe ni msamaha na atakusamehea tu kama nawe
utasamehea wabaya wako.
Husipotoshwe na mtu yeyote akakwambia kuwa maombi ya mtu aliyeokoka yatajibiwa sawasawa na ya mtu anayemkataa Yesu,huo ni uongo mtupu kwani maombi ya mwokovu husikizwa sana na Mungu.
Neno lako Isaya 1:18 unasema hata dhambi zangu ziwe nyekundu
utanisafisha na kunisamehea.Baba wa mbinguni nisamehe.
Ninafuta kila neno mbaya nililonenewa na wabaya
wangu,nikanenewa na wachawi wakasema sitabarikiwa.Nalifuta neno hilo kwa damu
ya Yesu Kristo katika Jina la Yesu kristo na ninabadilisha laana yao na kuwa
baraka kwangu katika Jina la Yesu.
Kila neno ovu la kunifunga lililotamkwa kwa kazi yangu nalifuta kwa damu ya Yesu Kristo.
<<<<<AMINA SANA MUNGU AKUBARIKI SANA KWA KUCHUKUA HATUA>>>>
WASILIANA NA MCHUNGAJI LAURENT MPOMA
PIGA +255762756542, +255782859946
WHATSAP: +255762756542
0 Comments