MCHUNGAJI LAURENT MPOMA
NCHI YA UKOMBOZI MINISTRY
(HEMA LA MAOMBI NA MAOMBEZI)
Laana ni bahati mbaya au maneno mabaya ya maapizo yanayotamkwa kumuelekea mtu fulani yeye mwenyewe au kitu fulani kinachomuhusu, kwa mfano; kazi, shamba, watoto, masomo n.k kwa makusudi ya kumdhuru mtu huyo au kitu kinachomuhusu. Kwa kifupi laana ni kinyume cha baraka.
Laana
inaweza ikasababishwa kwa makusudi maalumu (mfano: laana ambayo ni matokeo ya
dhambi za wanadamu) au pasipo kujua (mfano: laana ya kujitamkia sisi wenyewe),
kwa njia zote hizi mbili laana inafanya kazi iwe kwa makusudi au pasipo kujua.
Laana, ili
itende kazi ni lazima iwe imeunganishwa na nguvu fulani zisizo za kawaida,
nguvu za ziada “supernatural powers”,
nguvu hizo ni lazima ziwe zinazidi nguvu za mtu au kitu kinacholaaniwa.
Nachomaanisha hapa ni kwamba, mdogo hawezi kumlaani mkubwa; shetani hawezi
kumlaani Mungu, na mtu aliyesimama katika kweli na haki ya Mungu hawezi
kulaaniwa na shetani kutokana na ile nguvu ya Mungu iliyomo ndani yake.
Kwa maana
hiyo, kwa maneno yetu wenyewe au ya watu wa karibu nasi na matendo ya maisha
yetu ndiyo sababu kubwa ya laana katika maisha yetu na vizazi vyetu vijavyo.
Kwa sababu kila tunachokitamka na tunachokitenda kinafuatiliwa kutimilizwa na
falme mbili tofauti; ufalme wa Mungu na ufalme wa shetani. Ni hakika na kweli,
ufalme wa shetani hufuatilia hasa mambo ambayo ni hasi kuyatimiliza katika
maisha yetu, kuwa mwangalifu sana.
Mwanzo
2:16-17. Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu (Adamu), akisema, matunda ya kila mti
wa bustani waweza kula, walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya
usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.
Nataka
nikuoneshe kitu hapo, wakati Mungu anampa maagizo Adamu kwa habari ya chakula
ambacho ni matunda Biblia haisemi kuwa shetani naye alikuwepo akiyasikiliza
maagizo hayo. Lakini kwa hakika shetani alikuwepo japo Adamu hakumuo na
aliyasikia vizuri sana maagizo hayo. Hili tunalithibitisha kutokana na kitendo
chake (shetani) cha kumfuata Hawa na kumwambia habari ile ile ihusuyo maagizo
waliyopewa na Mungu.
Mwanzo 3:1.
Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya Bwana
Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, msile matunda
yote ya miti ya bustani?
Nataka ujue
yule alikuwa ni shetani aliyevaa umbo la mnyama nyoka. Na ndipo ujue kuwa kila
unachokitenda ama kukizungumza, shetani anakuona na kukusikia na kama Biblia
inavyosema kuwa shetani ni mshitaki wetu (Ufunuo 12:10), ndivyo ilivyo,
anafanya kazi mchana na usiku kuhakikisha matendo na maneno yetu hasi yanatimia
na tunapata mateso. Hiyo ndiyo furaha yake.
Ikiwa
tumetamka au tumetamkiwa maneno ya kuyalaani maisha yetu, ufalme wa giza
unatuma mapepo yatkayo kufuatilia mchana na usiku ili kuhakikisha ile laana
iliyotamkwa juu yako inatimia na kukupata.
Na jinsi
ufalme wa Mungu unavyotenda kazi kwa habari ya laana katika maisha yetu,
tutaona katika kipengele cha aina za laana.
Laana inaletwa/sababishwa na nani?.
Laana huweza kusababishwa na:-
Mungu. Mungu hatusababishi wanadamu laana
kama kitu cha furaha kwake, bali ni matokeo ya dhambi zetu. Tunapomkosea Mungu
huamua kuachilia laana katika maisha yetu kwa makusudi ya kutufanya tumrudie
yeye baada ya kutambua tunataabika kwa sababu tumemuacha Mungu.
Mwanzo 5:29.
Akamwita jina lake Nuhu, akinena, huyu ndiye atakayetufariji kwa kazi yetu na
kwa taabu ya mikono yetu katika nchi aliyoilaani Bwana (Mungu).
Kumbukumbu
la Torati 28:15. Lakini itakuwa usipotaka kuisikiza sauti ya Bwana, Mungu wako,
usiyaangalie kufanya maagizo yake yote na amri zake, nikuagizazo hivi leo
(ukiamua kutenda dhambi), ndipo zitakapokujia laana hizi zote na kukupata.
Malaki 2:2.
Kama hamtaki kusikia, na kama hamtaki kuitia moyoni (amri ya Mungu), ili
kulitukuza jina langu, asema Bwana wa majeshi, basi nitawapelekeeni laana, nami
nitazilaani baraka zenu; naam, nimekwisha kuzilaani, kwa sababu hamyatii haya
moyoni.
Shetani. Huyu jamaa naye huweza kusababisha
laana katika maisha yako, kama tulivyoona hapo juu. Pili, unapoamua kuishi
maisha ya dhambi ni kwamba unakuwa umedanganywa (umesababishiwa laana) na
ibilisi ambaye alishalaaniwa kwanza. Tutaona hapo mbele vitu vinavyoweza
kulaaniwa ndipo utaelewa kwa undani zaidi, labda nikupe mfano, mtu anapokuwa na
mateso yaliyotoka kuzimu kama mapepo, huyo anakuwa chini ya laana ya shetani.
Ufunuo wa
Yohana 20:10. Na yule ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la
moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uwongo. Nao watateswa
mchana na usiku milele na milele.
2 Petro
2:14. Wenye macho yajaayo uzinzi, watu wasiokoma kutenda dhambi, wenye kuhadaa
roho zisizo imara, wenye mioyo iliyozoezwa kutamani, wana wa laana (wana wa shetani,
wana wa ufalme wa giza).
Mwanadamu. Mwanadamu akisimama yeye kama yeye
hana nguvu wala uwezo wa kulaani, lakini anaposimama upande mmoja wapo aidha
kwa Mungu au kwa shetani, huweza kusababisha laana. Kwa sababu akiwa upande wa
Mungu akitamka neno zuri au baya linatokea (Mathayo 21:18-19, 1 Wafalme 17:1 na
18:1), kutokana na ile nguvu ya Mungu iliyomo ndani yake. Na mwanadamu huyo
huyo akisimama upande wa shetani laana atakayoitamka itatokea, kwa sababu
furaha ya shetani ni kuwaona wanadamu wanapata shida na mateso, lazima atatuma
roho chafu (mapepo) ziifuatilie na kuitimiza laana hiyo kwa mtamkiwa.
Warumi
12:14. Wabarikini wanaowaudhi; barikini, wala msilaani (mwanadamu ana uwezo wa
kulaani).
Yakobo 3:9.
Kwa huo (ulimi) twamhimidi Mungu Baba yetu, na kwa huo (ulimi-maneno ya kinywa)
twawalaani wanadamu waliofanywa kwa mfan wa Mungu.
Kwa maana
hiyo unaweza kuwa unatembea chini ya laana katika maisha yako, au vitu fulani
katika maisha yako vinaweza vikawa vimelaaniwa pasipo wewe kujua. Na laana hiyo
inaweza ikawa imesababishwa na Mungu, shetani au mwanadamu kama jinsi
tulivyoona hapo juu.
0 Comments