Kuna sababu nyingi tu zinazomfanya mtu au kitu kipokee laana. Sababu hizo ni kama zifuatazo:-
LAANA YA KUJITAMKIA AU KUTAMKIWA KWA KUJUA AU
PASIPO KUJUA.
Nianze na
mfano kwanza; unakuta mtu anasema, “sisi ukoo wetu ni maskini tu hata
tufanyaje”, “kwa hii kozi niliyosoma sijui kama nitapata kazi kwa kweli”,
“watoto wa mama fulani hawaolewagi”, “mimi masomo ya sayansi hata nifanyaje
siji kufaulu”, hiyo ni baadhi ya misemo iliyobeba laana ndani yake.
Na hakika
lazima kuna nguvu itafuatilia kuhakikisha inatimiza makusudi yaliyopo ndani ya
misemo hiyo. Na mara nyingi laana ya namna hii, watu wengi tunajitamkia pasipo
kujua kuwa tunachokitamka kitatimia katika maisha yetu. (Warumi 12:14, Yakobo
3:9).
LAANA ITOKANAYO NA KUWALAANI
WATUMISHI WA MUNGU WALIOBARIKIWA.
Kubali
ukatae, mtu yoyote au kitu chochote Mungu alichokibariki mwanadamu hawezi
kukilaani. Na ikiwa umemlaani au kutamka maneno mabaya juu ya mbarikiwa yoyote
wa Mungu, laana hiyo inafanyika kuwa baraka kwa uliyemtamkia lakini inakurudia
wewe kama laana (Hesabu 23:11 na Hesabu 24:10).
Hesabu
22:12. Mungu akamwambia Balaamu, usiende pamoja nao; wala usiwalaani watu hawa,
maana wamebarikiwa.
Mwanzo 12:3.
Nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa
zote za dunia watabarikiwa.
Mwanzo
27:29b. Atakayekulaani alaaniwe, na atakayekubariki abarikiwe.
LAANA YA WAZAZI.
Hii unaweza
ukaipata kutokana na jinsi unavyowatendea wazazi wako. Haijarishi wazazi wako
ni watu wa namna gani au wamewahi kukukosea nini, watabaki kuwa wazazi wako na
ni lazima uwape hushima yao (Kutoka 20:12). Kitu chochote kibaya
utakachowafanyia au kuwasemea wazazi wako, Mungu atajilipishia kisasi katika
maisha yako au hata uzao wako (Mathayo 15:4).
Mwanzo
9:24-25. Nuhu akalevuka katika ulevi wake, akajua mwana wake mdogo
alivyomtendea (alimchungulia na kuuona uchi wake). Akasema, na alaaniwe
Kanaani; atakuwa mtumwa kabisa kwa ndugu zake.
Pasipo
kujarisha wazazi wako wanatabia gani, laana yoyote watakayo itamka juu yako au
manung’uniko yoyote utakayo wasababishia yatafanyika kuwa laana itakayo laani
maisha yako.
Kumbukumbu
la Torati 27:16. Na alaaniwe amdharauliye baba yake au mama yake. Na watu wote
waseme, Amina.
Laana hii ni
tofauti na nyingine, inahitaji upate kibali cha wazazi pia ili kuifuta katika
maisha yako. Ikiwa hadi hapa, umetambua uko chini ya laana ya wazazi, huna budi
kuwataka radhi kwa uliyowahi kuwakosea.
LAANA YA KUWANYANYASA
WAGENI, YATIMA NA WAJANE.
Hii ni laana
inayowapata watu kwa sababu ya tamaa ya mali, mara nyingi; anapofariki mume
mwenye uwezo kifedha wa mwanamke fulani au baba mwenye uwezo kifedha wa watoto
fulani ndugu wa marehemu wanaanza kuwanyanyasa mke na watoto wa marehemu kwa ajili
ya kuwadhurumu mali na kuwazushia mambo kibao.
Kwa kosa
hilo Mungu hujilipishia kisasi juu ya yoyote aliyehusika kufanya hivyo pasipo
kujali kuwa unaowanyanyasa wanamjua au hawamjui Mungu, machozi yao ni kiberiti
cha kuwasha hasira ya Mungu kwako. Kwani Mungu amesema yeye ni mume wa wajane
na baba wa yatima (Yakobo 1:27, Zaburi 68:5).
Kutoka
22:21-24. Usimwonee mgeni, wala kumtendea jeuri; kwa kuwa ninyi mlikuwa wageni
katika nchi ya Misri. Usimtese mjane ye yote aliyefiwa na mumewe, wala mtoto
yatima. Ukiwatesa watu hao katika neno lo lote, nao wakanililia mimi, hakika
yangu nitasikia kilio chao, na hasira yangu itawaka moto, nami nitawaua ninyi
kwa upanga; na wake wenu watakuwa wajane, na watoto wenu mayatima.
Kumbukumbu
la Torati 27:19. Na alaaniwe apotoaye hukumu ya mgeni, na yatima, na mjane
aliyefiliwa nu mumewe. Na watu wote waseme, Amina.
LAANA ITOKANAYO NA
KULA/KUIBA FUNGU LA KUMI LA MUNGU.
Laana hii
imewafunika watu wengi sana makanisani, unakuta mtu anafanya biashara au ni
mfanyakazi katika ofisi au shirika fulani lakini hana maendeleo yoyote, na
wengine wanapokea mishahara mikubwa lakini fedha inapotea katika mazingira
yasiyo na maelezo kamili.
Kama wewe ni
mmoja wapo, amabaye huoni mafanikio licha ya fedha nyingi unayoipata, biashara
yako haikui licha ya kuwa unaitangaza sana, tambua unatembea chini ya laana kwa
kutotoa fungu la kumi.
Malaki 3:9.
Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi (zaka-fungu la kumi), naam,
taifa hili lote.
LAANA ITOKANAYO NA
KUTENDA DHAMBI AU KUTOTII MAAGIZO YA MUNGU.
Mwanadamu
anapofanya dhambi, hasira ya Mungu inawaka juu yake, na Mungu anaagiza laana
juu ya mwanadamu huyo kwa makusudi ya kumkumbusha mwanadamu huyo kuwa anatakiwa
kurejea kwa Mungu na kuziacha njia zake mbaya.
Mwanzo 3:17.
Akamwambia Adamu, kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti
ambao nalikuagiza, nikisema, usiyale (kutotii); ardhi imelaaniwa kwa ajili
yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako.
Kumbukumbu
la Torati 11:26-28. Angalieni, naweka mbele yenu hivi leo baraka na laana;
baraka ni hapo mtakapoyasikiza maagizo ya Bwana, Mungu wenu, niwaagizayo hivi
leo; na laana ni hapo msiposikiza maagiza ya Bwana, Mungu wenu, mkikengeuka
katika njia niwaagizayo leo, kwa kuandama miungu mingine msiyoijua.
LAANA ITOKANAYO NA
KUMWAGA DAMU.
Watu wengi
sana wanatembea na laana hii pasipo wao wenyewe kujua, kwa kuwaua watu (ili
wapate mali na utajiri) au kwa kutoa mimba maisha yako yanalaaniwa. Ndiyo maana
utawakuta wengine wana mali nyingi lakini hawana amani na wengine wamehangaika
kila sehemu kutafuta watoto lakini hawapati, ni kwa sababu wamesahau damu
waliyoimwaga miaka mingi iliyopita, damu ambayo bado inadai kisasi juu yao,
mbele za Mungu.
Mwanzo
4:10-11. Akasema (Mungu), umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia
kutoka katika ardhi. Basa sasa umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa
chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako.
LAANA ITOKANAYO NA
KUFANYA UZINZI NA MZAZI WAKO AU MZAZI WA MKE AU MUME (MKWE) WAKO AU NDUGU YAKO
WA DAMU.
Laana hii
huwapata wale wanaotimiza masharti ya waganga wa kienyeji hasa, ili kujipatia
mali za kishirikina.
Kumbukumbu
la Torati 27:20,22, na 23. Na alaaniwe alalaye na mke wa baba yake, kwa kuwa
amefunua mavazi ya babaye. Na watu wote waseme, Amina. Na alaaniwe alalaye na
umbu lake, binti ya babaye, au binti ya mamaye. Na watu wote waseme, Amina. Na
alaaniwe alalaye na mkwewe, mamaye mkewe. Na watu wote waseme, Amina.
LAANA YA KUFANYA
MAPENZI NA MNYAMA.
Ni kwa mtu
yo yote aliyewahi kufanya mapenzi na mnyama kwa kutimiza masharti ya
kishirikina na uchawi, kwa taama binafsi au kwa minajili ya kujipatia fedha,
kwa mfano; mbwa, farasi n.k.
Kumbukumbu
la Torati 27:22. Na alaaniwe alalaye na mnyama wa aina yo yote. Na watu wote
waseme, Amina.
Kuna sababu
au vitu vingi vinavyoweza kukusababishia laana katika maisha yako, kazi au
biashara yako, ama vitu unavyovimiliki kama shamba au nyumba.
Na kitu
kibaya zaidi ni kwamba laana inarithiwa, kutoka kizazi kimoja kwenda
kinachofuata. Unaweza usione matokea ya laana katika maisha yako ya sasa na
ukaamua kunyamaza ilihali ukijua kuna mambo uliwahi kufanya yanayofanana na
hayo hapo juu. Nakuambia hiyo laana ni lazima ikufuatilie kama siyo wewe basi
ni uzao wako, na kuna watu wanaishi chini ya laana zilizosababishwa na wazazi
wao ambao unaweza ukakuta hawapo hai kwa sasa.
Kumbukumbu
la Torati 28:45-46. Na laana hizi zote zitakujilia juu yako, zitakuandama na
kukupata, hata uangamizwe, kwa kuwa hukusikiza sauti ya Bwana, Mungu wako,
kushika maagizo yake na amri zake alizokuagiza; nazo zitakuwa juu yako kwa
ishara na ajabu, na juu ya uzao wako milele.
JE, UNAWEZA KUWA
UMELAANIWA PASIPO WEWE KUJUA?
Hakika jibu
ni ndiyo; unaweza kuwa ulifanya uovu au jambo lolote kati ya hayo yanayoweza
kusababisha laana katika maisha yako, na bado hujaona matokeo ya hiyo laana
katika maisha (labda uwe ulitubu na kuvunja laana hiyo), kinyume na hapo laana
hiyo bado iko juu yako na inakufuatilia kama siyokukupata wewe basi ni uzao
wako, kama tulivyoona kuwa laana inarithiwa (kumbukumbu la Torati 28:45-46).
NI VITU GANI VINAWEZA
KULAANIWA?
Kwanza wewe
mwenyewe unaweza kupokea laana katika mwili wako, vitu unavyomiliki kama ardhi,
nyumba, mifugo n.k huweza kulaaniwa kwa ajili yako.
ARDHI. Unailima ardhi lakini hupati mazao
kutoka kwake, unazingatia kilimo cha kisasa lakini mavuno ni haba.
Torati
29:27. Ndipo ikawashwa hasira ya Bwana juu ya nchi (ardhi) hii, kwa kuleta juu
yake (ardhi) laana yote iliyoandikwa katika kitabu hiki.
UZAO WAKO. Watoto wako wanakuwa wasumbufu
haijawahi kutokea; wana kiburi, wana tabia mbaya, umetumia upole na ukali
kuwakanya lakini hawakusikii, au hata hawana mafanikio kwa kila jambo
wanalolifanya.
Torati
28:18. Utalaaniwa uzao wa tumbo lako.
MIFUGO YAKO. Unajitahidi kufuga mifugo kwa njia
za kisasa, lakini mifugo haiongezeki, ikizaa watoto wanakufa, au kila siku
unaibiwa wewe, mifugo yako inapotea pasipo kuonekana.
Torati
28:18. Utalaaniwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, maongeo ya ng’ombe
wako, na wadogo wa kondoo zako (mifugo yako).
Kazi za
mikono yako na uchumi wako kwa ujumla. Unafanya kazi au biashara ambayo huoni
faida yake, zaidi ya kukupatia fedha ya kujikimu tu. Umekuwa na uchumi ule ule
miaka nenda rudi na ndiyo kwanza unazidi kushuka chini.
Torati
28:20. Bwana atakuletea laana na mashaka, na kukemewa katika yote utakayotia
mkono wako kuyafanya (kazi na biashara zako), hata uangamie na kupotea kwa
upesi; kwa ule uovu wa matendo yako, uliyoniachia kwayo.
NYUMBA YAKO. Unaweza ukawa umejenga nyumba
lakini huna furaha nayo, hutamani kuendelea kuishi ndani yake, unaona ni
afadhari ukapange kuliko kuendelea kuishi ndani ya nyumba yako uliyoijenga au
kuinunua kwa fedha yako mwenyewe.
Mithali
3:33. Laana ya Bwana i katika nyumba ya waovu, bali huibariki maskani ya wenye
haki.
MWILI WAKO. Unapata magonjwa yasiyo na sababu,
ukifuatilia chanzo cha magonjwa au wapi ulipata maambukizo hakuna unakoweza
kupata jibu. Na hata ukienda hospitali bado hupati uponyaji.
2 Nyakati
7:13. Nikizifunga mbingu isiwe mvua, tena nikiamuru nzige kula nchi, au
nikiwapelekea watu wangu tauni (magonjwa).
ANGA AU MBINGU. Mvua hainyeshi au hainyeshi kwa
wakati. Maombi yako hayafiki mbele za Mungu, anga imefungwa isipitishe kitu
chochote kwa ajili yako.
2 Nyakati
6:26. Ikiwa mbingu zimefungwa, hata hakuna mvua, kwa sababu wamekukosa wewe.
Hadi kufikia
mwisho wa somo hili nina imani kuwa umetambua laana ni nini na ikiwa upo chini
ya laana na hukujua, basi leo umefumbuliwa macho. Sitaki nikuache hivi hivi,
nitafanya maombezi kwa ajili yako ili Mungu akurehemu na kukufungua vifungo
vyote vya laana. Kwanza kabisa nataka nikuombe rehema na kisha nivunje na
kufuta laana zote na kutamka baraka katika maisha yako.
Unachotakiwa
kufanya ni kunipa ushirikiano ambao ni; unatakiwa kuwa na imani thabiti, kwani
si mimi ninayetenda hili, bali Yesu Kristo mwenyewe anakwenda kuhusika na
ninakuhakikishia utatoa ushuhuda mzuri wa ushindi baada ya maombi haya.
Wewe
mwenyewe utakwenda kuyasoma maombi haya, ni maombi yenye nguvu na uwezo wa
Mungu (Yehova); kwa imani gusa kioo cha kompyuta yako, simu yako au kitu
chochote unachotumia kufuatilia somo hili:-
Toba: Ee
Yesu Kristo nasogea mbele zako mimi na nafsi yangu, ninaomba unisamehe dhambi
zangu zote, unitakase kwa damu yako ya thamani iliyomwagika pale msalabani kwa
ondoleo la dhambi za wanadamu. Ulifute jina langu katika kitabu cha hukumu na
uliandike katika kitabu chako cha uzima. Amina.
MAOMBI: Mungu Baba katika jina la Yesu
Kristo, ninamleta mtu huyu asiye na msaada wo wote zaidi yako, na imani iliyomo
ndani yake kwako, msamehe makosa yake yote, umtakase na kumuosha kwa damu ya
Yesu Kristo. Ninafuta kila laana na mikosi katika misha yake, iliyosababishwa
na kila namna ya sababu, ninatamka baraka na ushindi katika maisha yake yote,
yeye mwenyewe, familia yake na uzao wake wote unakwenda kubarikiwa sasa, mifugo
yake, kazi za mikono yake, mashamba yake na nyumba yake, vyote vikabarikiwe
sasa, kwa jina la Yesu Kristo. Amina.
0 Comments