Follow us

SOMO: UKIAMINI YOTE YAWEZEKANA

Tangazo

 


SOMO: UKIAMINI YOTE YAWEZEKANA

 Maandiko: Marko 9:19-23

19 Akawajibu, akasema, Enyi kizazi kisichoamini, nikae nanyi hata lini? Nichukuliane nanyi hata lini? Mleteni kwangu 20 Wakamleta kwake; hata alipomwona, mara yule pepo alimtia kifafa; naye akaanguka chini, akagaa-gaa, akitokwa na povu. 21 Akamwuliza babaye, Amepatwa na haya tangu lini? Akasema, Tangu utoto. 22 Na mara nyingi amemtupa katika moto, na katika maji, amwangamize; lakini ukiweza neno lo lote, utuhurumie, na kutusaidia. 23 Yesu akamwambia, Ukiweza! Yote yawezekana kwake aaminiye. 24 Mara babaye yule kijana akapaza sauti, akasema, Naamini, nisaidie kutokuamini kwangu.

Imani ya kweli katika Yesu ni msingi imara katika maisha ya kiroho. Ni jibu la mambo yote. Ni mkono unaochukua majawabu ya mahitaji yetu kutoka ulimwengu usioonekana na kuyafikisha kwenye ulimwengu wa mwili, tukaona kwa macho na kushika kwa mikono yetu.

Imani ni nini?

Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.

(Ebr 11:1)

Imani inakuthibitishia kuwa kitu unachokihitaji kimepatikana sasa wakati kinatarijiwa; imani inakiona:kitu halisi na kukikamata wakati hakipo.

 

Nchi ya Israeli ilikumbwa na ukame mbaya sana, ikatokea njaa kali, ikasababisha watu kula watoto wao, punda na mavi ya njiwa. Katika nyakati hizo za ukame nabii Elisha aliyekuwa na imani katika Mungu alitangaza kuwa kesho kutapatikana unga tele na nafaka mbalimbali. .Imani iliona mbali ikavuka mipaka ya ufahamu wa kibinadamu. Askari wa mfalme aliona kmwili Elisha aliona kiroho.

Elisha akasema, Lisikieni neno la Bwana; Bwana asema hivi, Kesho panapo saa hii, kipimo cha unga mzuri kitauzwa kwa shekeli, na vipimo viwili vya shayiri kwa shekeli, langoni pa Samaria (2Fal 7:1)

Kesho yake kweli yote yalitimia; soma (2Fal 7:1-20) Askari wa mfalme alikufa kwa kutokuamini.

 

Imani inazaliwa na inakua.

Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo. (Rum 10:17)

Imani ya kweli inazaliwa kwa kusikia Neno la Kristo. Imani inakua kila wakati inapotumika kuleta majibu ya mambo magumu. Yesu alifundisha somo la imani inayoleta matokeo.

(Mathayo 17:20) Yesu akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amini, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu.

Imani inayoweza kuhamisha milima ya matatizo yako yote, inanza na kiasi cha punje ya haradali iliyo ndogo kuliko punje ya mchicha. Fahamu kuwa punje hiyo ikipandwa inaota na kukua hadi kuwa mti mkubwa. Na imani yako itakua kwa kadiri unavyoitumia kutatua matatizo yanayokukabili siku kwa siku.

Daudi alikuwa na ujasiri wa kukabiliana na Goliathi kwa sababu imani yake ilikua katika Bwana kwa kuwaua simba na dubu.

(1Sam17:36 ) Mtumishi wako alimwua simba na dubu pia; na huyu Mfilisti asiyetahiriwa atakuwa kama mmoja wao, kwa sababu amewatukana majeshi ya Mungu aliye hai.

Baba wa kijana tuliyemsoma hapo juu alimwomba Yesu kwa mashaka akisema, “lakini ukiweza neno lo lote, utuhurumie, na kutusaidia”. Bwana Yesu alimjibu kwa maneno yake , “Ukiweza! Yote yawezekana kwake aaminiye”. Yule baba alitambua haraka kosa lake akatubu na kuamini. Yesu akamponya mwanawe saa ileile.

Kizazi chetu tunafanana na baba huyo; tunafahamu kuwa Yesu anaponya, anaokoa na kutenda miujiza mingi. Inapokuja kwenye mahitaji yako wewe binafsi imani inapungua. JiulizeYesu amekufanyia nini? na unamtarajia akufanyie nini katika matatizo yako?  Je unaamini kweli anaweza? Je moyoni mwako mna mahangaiko na kutangatanga kutafuta ufumbuzi?. Kutokuamini ni dhambi na kunakukosesha majibu ya mahitaji magumu ya moyo wako. Mungu hashindwi na neno lolote.

MUNGU AKUBARIKI SANA



MAOMBI NA MAOMBEZI

WASILIANA NA MCHUNGAJI LAURENT MPOMA

(NCHI YA UKOMBOZI MINISTRY)

CALL: +255762756542

WHATSAP: +255762756542

Youtube>>>Upenyo wa Mungu Tv" kisha SUBSCRIBE

 

 

 

 

 

 

Post a Comment

0 Comments