Mipango
mitano 5 muhimu kukusaidia kufikia malengo yako mwaka mpya
Andika mambo
haya mahali ili uyatumie kuweka mkakati
wako kuwa wa maana kwa ajili ya mwaka ujao.
1. Tofautisha mipango yako ya kikazi
na kibinafsi
Malengo yako ya kikazi yatakuwa ni tofauti na yale ya
kibinafsi ,licha ya kwamba yanategemeana. Vinginevyo huenda usifanikiwe kwa
kiasi ambacho ulikitarajia.
2. Andaa mpango kwa
ajili ya mwaka mpya
Fikiria ni malengo gani hasa unayotaka kuyafikia tarehe 31
Disemba ya mwaka ujao. Kisha, panga hatua unazohitaji ili uweze kuyafikia
malengo hayo.
Andika mahali shughuli muhimu au mafanikio
unayotarajia kuyaona kama viashiria vya vitakavyokuwezesha kufikia mafanikio
hayo.
Viashiria
hivi vinaweza kuwa miradi, au ujuzi wa kitaaluma.
Pia, angalia
uwezekano wa vikwazo vya mafanikio uliyoyapanga. Kama mwaka huu umetufundisha
kitu fulani, hicho ndicho kitakacho kuwa mpango wa pili au wa tatu kama mambo hayatakwenda ulivyopanga.
Huenda
usihitaji mipango hii mbadala.
Kuwa na
mipango hii mbadala hatahivyo hutusaidia kuwa na kiasi fulani cha utulivu wa akili,huku
tukijiandaa kusonga mbele na mpango wa awali.
3.
Panga orodha ya mambo ambayo hautayafanya
Kupanga
orodha ya mambo ambayo hautayafanya haimaanishi kuwa unaachana na mambo ambayo
hutaki kuyafanya. Ni pia kuachana na mambo ambayo yanakuzuia kiutendaji kufikia
malengo yako.
4: Tenga muda kwa ajili yako binafsi.
Panga muda
wako binafsi wa likizo au mapumziko
mapema. Kama unahisi kuwa unahitaji kwenda kutembea mahala fulani,
jipange mapema na utenge kiasi cha pesa zinazoweza kukuwezesha kwenda likizo.
Mchoko na
msongo wa mawazo wa kuendelea kufanya kazi
bila kupumzika sio mzuri kwa afya yako binafsi, na wala kufanya kazi kwa
muda mrefu bila kupumzika hakukuongezei uwezo wa ufanisi wa kikazi kwa ajili ya
kufikia malengo yako.
5. Panga mradi wako wa kando ili
ukuongezee kipato
Angalia kati
ya mambo unayoyapenda uyatumie kama
mradi wako wa kando wa kukuongezea kipato, usitegemee sana kazi
unayoifanya pekee kama chanzo cha mapato yako.
MUNGU AKUBARIKI SANA
0 Comments