MAOMBI YA KUVUNJA NA KUSAMBARATISHA ROHO ZA ZILIZOACHILIWA KUHARIBU MAISHA YAKO.
Maombi haya ni kwa ajili ya wale ambao wanataka au wanatamani kujiondoa kwenye maagano ya Uharibifu,
Maagano yanayozungumziwa hapa ni yale ya kurithi au yaliyoingiwa na mhusika aidha kwa kujua au pasipo kujua kama anaingia kwenye maagano. Kwa sababu ni maagano ya uharibifu ni muhimu kujiondoa au kuvunja maagano hayo. Ili kuyavunja ni lazima utangaze kuyavunja, na inawezekana maagano mengine yapo hapo muda mrefu, kwa hiyo ni lazima kuomba kwa bidii soma Yakobo 5:16
Wakolosai 2:14-15, “akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani; akiisha kuzivua enzi na mamlaka, na kuzifanya kuwa mkogo kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba huo”
Wagalatia 3:13-14, “Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti ili kwamba baraka ya Ibrahimu iwafikilie Mataifa katika Yesu Kristo, tupate kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya imani”
Maombi na maombezi
1. Ninarudisha mamlaka yote aliyopewa shetani na mababu /mababa, katika Jina la Yesu.
2. Nina zilaani roho zote zinazoendelea kutilia mkazo hayo maagano katika maisha yangu na naziamuru kuniachia kwa Jina la Yesu[ Sema mara 3 na anza kusema hivi,”niachie kwa jina la Yesu
3. Kitu chochote kilichoingizwa kwenye maisha yangu,kwa mkono wa kipepo, ninakiamuru kiachie kwa JIna la Yesu
4. Kila aina ya sumu iliyopenyezwa kwenye maisha yangu nina iamuru itoke nje sasa, katika jina la Yesu, nina sukuma nje kwa damu ya Yesu.
5. Ee Bwana Yesu,shusha moto juu ya kila roho ya mauti na kuzimu,iliyoandaliwa kwa ajili yangu, katika jina la Yesu
6. Nina ponda kichwa na kukanyaga kila mkia wa majoka ya kiroho, katika jina la Yesu
7. Upanga wa moto, na uanze kukata kila kifungo walichokifunga wazazi, katika jina la Yesu
8. Ee Bwana, nifunulie agano lolote la siri ambalo shetani amefunga na nafsi yangu au anataka kufunga na nafsi yangu, katika jina la Yesu.
9. Kila pando,ambalo baba yangu wa mbinguni hakulipanda katika maisha yangu, nina kungo’a katika jina la Yesu.
10. Baba nina pitisha umeme katika ardhi ya mahali hapa sasa na kila agano na miguu yangu lianze kuvunjika sasa katika jina la Yesu.
11. Agano lolote la siri ambalo ni la uovu, ninakuvunja katika jina la Yesu
12. Nina nyunyiza damu ya Yesu kuvunja laana zote
13. [Imba wimbo huu kama unaweza, kama huwezi usilazimshe: Kuna nguvu ya ajabu, damuni mwa Yesu ]
14. Nina nyunyiza damu ya Yesu kuvunja laana zote za dhambi za wazazi wangu
15. Ee Bwana, badili laana zote zilizoelekezwa kwangu kuwa Baraka
16. Kila nguvu ya uovu iliyoelekezwa kwangu, ninakuamuru kurudi moja kwa moja, kwa mtumaji katika jina la Yesu.
17. Ee Bwana Mungu, ninaomba kila alichosema adui kwamba hakitawezekana katika maisha yangu, kikawezekane sasa kwa jina la Yesu.
18. Nina jiondoa na kujitenganisha katika kambi yoyote ya mateka inayomilikiwa na adui,katika jina la Yesu.
19. Nina jifungua na kujiondoa kutoka kwenye kila kifungo cha kurithi ,katika jina la Yesu.
20. Ee Bwana,tuma shoka lako la moto kwenye misingi ya maisha yangu na uharibu/ulikate kila pando ambalo amelipanda adui katika jina la Yesu.
21. Nina ipitisha Damu ya Yesu, katika mifumo yote ya mwili wangu [mfumo wa damu, wa fahamu, wa chakula, wa upumuaji, wa takamwili n.k] na kuisafisha mabaki yote ya urithi wa vitu viovu katika jina la Yesu.
22. Damu ya Yesu na moto wa Roho mtakatifu,unisafishe kila kiungo cha mwili wangu [Figo, moyo, mapafu, macho, masikio, n.k] katika jina la Yesu
23. Nina vunja mikataba yote ya kiukoo na kikabila inayonihusisha mimi katika jina la Yesu.
24. Nina jiondo/ninajivua/vunja laana zote za kikabila na kiukoo katika jina la Yesu
25. Nina tapika chakula chochote cha uovu nilicholishwa katika maisha yangu, katika jina la Yesu
26. Mapepo, majini, mizimu na wachawi manao fuatilia maisha yangu,na mpararaizi[mpooze] sasa katika jina la Yesu.
27. Shambulio lolote lilopangwa juu ya familia yangu, ninalibatilisha kwa ajili yangu katika jina la Yesu
28. Nina vunja matokeo mabaya yote kwa ajili ya jina la kiuovu, lilipachikwa kwenye nafsi yangu katika jina la Yesu
29. Nina batilisha laana zote, mikosi, majanga, ajali, maradhi yote yaliyoelekezwa kwenye maisha yangu katika jina la Yesu.
30. Muombe Mungu aondoe laana zote alizo ziachilia kwenye maisha yako kwa sababu ya kutotii neno lake[kumb 28:]
31. Pepo lolote lililo jipachika kwenye laana yoyote inayonihusu mimi, toka, katika jina la Yesu
32. Laana zote katika maisha yangu, badilika na kuwa Baraka, katika jina la Yesu
33. Utakapokuwa unataja laana zilizoorodheshwa hapo chini, sema kwa kumaanisha “vunjika, vunjika, vunjika” katika jina la Yesu. Nina jitenganisha na nyinyi katika jina la Yesu.
MAOMBI NA MAOMBEZI
WASILIANA NA MCHUNGAJI LAURENT MPOMA
0762756542
WHATSAP: 0762756542
0 Comments