VITU
VITAKAVYOKUWEZESHA UITUMIE IPASAVYO MAMLAKA ULIYOPEWA NA MUNGU.
Marko 11: 27-28 ‘’ 27 Wakafika tena Yerusalemu, wakati Yesu
akitembea hekaluni, viongozi wa makuhani, walimu wa sheria pamoja na wazee
wakamjia.
28Wakamwuliza, “UNAFANYA MAMBO HAYA KWA MAMLAKA GANI? Naye
ni nani aliyekupa MAMLAKA YA KUFANYA HAYO?
Matendo ya Mitume 4:5-7 ‘’ 5 Siku ya pili yake viongozi wa
Kiyahudi, wazee na waandishi wa sheria wakakusanyika Yerusalemu, 6 walikuwepo
Kuhani Mkuu Anasi, Kayafa, Yohana, Iskanda na wengi wa jamaa ya Kuhani Mkuu. 7
Wakiisha kuwasimamisha Petro na Yohana katikati yao, wakawauliza, “Ni kwa UWEZO GANI AU KWA JINA LA NANI mmefanya
jambo hili?”’’
Yesu aliulizwa swali hili kuwa ni kwa mamlaka ya nani
unafanya jambo hili. Hata wanafuzni wa Yesu pia waliulizwa swali hili. Maana
kwa akati ule viongozi wa dini hawakujua kuwa walifanya kwa mamlaka ya nani na
ni nani aliwepa mamlaka kwa sababu hawakuwahi ona. Maana wangejua wasingeuliza.
Pointi ni kuwa si vile vinavyofanyika unapokuwa na mamlaka bali ni VITU GANI
vitakuwezesha kutumia mamlaka uliyopewa na Mungu.
MAANA YA MAMLAKA–
ni haki ya kisheria inayompa mtu uwezo wa kuamua na kusimamia utii juu ya kile
alichokiamua.
Kwa hiyo kwa kujua maana hii utajua ni kwanini wale viongozi
wa dini waliomuuliza Yesu lile swali na walilowauliza akina Petro na wanafunzi
ili wajue kuwa ni mamlaka ipi ndiyo waliyokuwa nayo na ni nani aliyesimamia
utii wa kile walichofanya maana wakuu wa dini walijua vizuri sana sharia.
LEO TUTAPITIA MAMLAKA
AINA 11 AMBAZO YESU AMETUPA.
1. MAMLAKA JUU YA
UUMBAJI NA MUNGU.
Mwanzo 1: 24-27 , Mungu katupa mamlaka ya kutawala kila kitu
alichokiumba Yeye. Na ona sasa ugomvi wa Musa na Farao na wale waganga na
wachawi ulikuwa kwenye viumbe. Ndio maana utaona Musa aligeuza fimbo yake ikawa
nyoka na ikameza zingine za wale wachawi. Ivi unajua wachawi wanapigana vita
kwa kutumia viumbe mfano Paka, Panya,Nyoka,Mbwa, bundi n.k
Musa alisema kama mimi ni mtumishi wa Mungu na tuone
kinachowatokea na ghafla ardi ikafumbua kinywa chake na ikawameza. Yoshua
alipojua kuwa maadui zake walikuwa wanapigana nae kutoka kwenye nguvu
zilizokuwa kwenye jua na yeye akaamua kulisimamisha jua. Nae Shetani aliamua
kutumia mawambi na upepo ili kupigana na Yesu na wanafunzi wa Yesu hawakujua
cha kufanya lakini Yesu alijua cha kufanya.
2. MAMLAKA JUU YA
PEPO NA MARADHI.
Luka 9:1 ‘’ Yesu akiisha kuwaita wale kumi na wawili pamoja,
aliwapa mamalaka na uwezo wa kutoa pepo wachafu wote na kuponya magonjwa
yote,’’
Kuwa na mamlaka haimaanishi kuwa unaweza kuitumia sawasawa
kama Mungu anavyotaka bali kwa hiyo unahitaji sana kuomba sana ili Mungu akupe
maarifa vizuri namna ya kutumia mamlaka hii uliyopewa na Mungu.
3. MAMLAKA JUU YA
MFUMO WA UTAWALA WA GIZA/ SHETANI.
Waefeso 6:12 ‘’ wamba mweze kuzipinga hila za Shetani. 12
Kwa maana kushindana kwetu si juu ya nyama na damu, bali dhidi ya falme,
mamlaka, dhidi ya wakuu wa giza na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa
roho’’
Mamlaka ya hapa ni tofauti na ile mamlaka ya kwenye Luka 9:1
, kwa mfano mamlaka juu ya Tanzania na mamlaka ya juu ya watanzania ni tofauti
kwa sababu Mamlaka juu ya Tanzania ni juu ya mfumo bali mamalaka juu ya
watanzania ni juu ya watu. Kwa hiyo mfano Tanzania kiongozi akifa, watu
watahuzunika afu baadae watateua mwingine maana nafasi ile ipo kisheria. Kwa
maana hiyo huwezi tumia mamlaka juu ya pepo ili kuja kushughulikia falme. Hizi
ni mamlaka unahitaji kujua.
4. MAMLAKA JUU YA
UFALME WA MBINGUNI.
Mathayo 16:19 ‘’ 19 Nitakupa funguo za Ufalme wa Mbinguni na
lo lote utakalolifunga duniani litakuwa limefungwa Mbinguni, lo lote
utakalofungua duniani litakuwa limefunguliwa mbinguni.’’
Kwa hiyo jua kuwa mamlaka zina mipaka, kwa hiyo ili jambo
lifunguliwa Duniani ndipo linafunguliwa na mbinguni. Lakini order intoka
Duniani.
Pia Mungu ametupa kufungua vitu vingine. Kwa hiyo ujio wa
Dhambi Duniani iliondoa ufalme wa Mungu. Hata wale waliofungwa na kuzimu
unaweza wafungua. Kwa hali hii ni hatari sana kwa Mtu aliyeokoka kutokaa kwenye
mamlaka ya ufalme wa Mungu. Hivyo Mungu anaweka watu kwenye mamlaka ili waweze
kuzisimamia. Mtu yeyote anapookoka anahamishwa kutoka ufalme wa giza na kuletwa
kwenye ufalme wa Mungu.
5. MAMLAKA JUU YA
DHAMBI.
Warumi 6:12-14 ‘’ 12 Kwa hiyo, msiruhusu dhambi itawale
ndani ya miili yenu, ipatikanayo na kufa, ili kuwafanya mzitii tamaa mbaya.
13Wala msivitoe viungo vya miili yenu vitumike kama vyombo vya uovu vya kutenda
dhambi, bali jitoeni kwa Mungu, kama watu waliotolewa kutoka mautini kuingia
uzimani. Nanyi vitoeni viungo vya miili yenu Kwake kama vyombo vya haki. 14Kwa
maana dhambi haitakuwa na mamlaka juu yenu, kwa sababu hampo chini ya sheria,
bali chini ya neema.
Warumi 7:15-24 ‘’14 Kwa
maana tunajua kwamba sheria ni ya kiroho, lakini mimi ni wa kimwili nikiwa
nimeuzwa kwenye utumwa wa dhambi. 15Sielewi nitendalo, kwa maana lile
ninalotaka kulitenda, silitendi, lakini ninatenda lile ninalolichukia. 16Basi
kama ninatenda lile nisilotaka kutenda, ni kwamba ninakubali kuwa sheria ni
njema. 17Lakini, kwa kweli si mimi tena nitendaye lile nisilotaka bali ni ile
dhambi ikaayo ndani yangu. 18Kwa maana ninafahamu kwamba hakuna jema lo lote
likaalo ndani yangu, yaani, katika asili yangu ya dhambi. Kwa kuwa nina shauku
ya kutenda lililo jema, lakini siwezi kulitenda. 19 Sitendi lile jema nitakalo
kutenda bali lile baya nisilolitaka, ndilo nitendalo. 20Basi kama ninatenda
lile nisilotaka kutenda, si mimi tena nifanyaye hivyo, bali ni ile dhambi
ikaayo ndani yangu.
21Hivyo naiona sheria ikitenda kazi. Ninapotaka kutenda
jema, jambo baya liko papo hapo. 22Kwa maana katika utu wangu wa ndani
naifurahia sheria ya Mungu. 23Lakini ninaona kuna sheria nyingine inayotenda
kazi katika viungo vya mwili wangu inayopigana vita dhidi ya ile sheria ya
akili yangu.Sheria hii inanifanya mateka wa ile sheria ya dhambi inayofanya
kazi katika viungo vya mwili wangu. 24Ole wangu, mimi maskini! Ni nani
atakayeniokoa na mwili huu wa mauti?.’’
Kwa hiyo tulitegemea hapa Paulo aliposema kuwa Dhambi
isitawale maishani mwenu na tulitegema Yeye asiwe na dhambi lakini tunachokiona
hapa ni kuwa Pualo anakiri kuwa anadhambi, Kwa hiyo haikukugurantee wewe kuwa
na upako kama Paulo na usiwe na dhambi. Na Tafsri ya dhambi ni Uasi lakini hii
nayo uhalali wa dhambi kututawala bali sisi tushinde dhambi.
Utajiuliza ni Kitu gani kilikuwa kinamkwamisha Paulo jibu
lake ni hili ni MWILI, hata siku moja jaribu kumuuliza Yesu kuwa ni kitu gani
kilikuwa kinakukwamisha kwenda msalabani na ulilia sana pale Getsamen
atakuambia ni Mwili ndio maana alisema roho I radhi ila mwili ni dhaifu.
Nia na Mwili ni Mauti , maana mwwili hauendi mbinguni na
mwili hautiii cha Mungu.
Kwa hiyo ile wewe kuwa na mamlaka juu ya pepo wabaya au
maradhi haikupi kibali cha kwenda mbinguni maana Yesu alisema watasema mbona
tulitoa unabii, pepo kwa jin lako lakini yeye atawaambia kuwa sikuwajua ninyi.
Na ndio maana aliwaambia wanafunzi wake msifurahi kwa kuwa pepo wanawatii bali
furahini kwa kuwa majina Yenu yameandikwa mbinguni.
Kwa hiyo mamlaka hizi zinatupa namna ya kutembea hapa
Duniani na sio kwenda mbinguni. Suala la kwenda mbinguni ni suala jingine
kabisa. Ukiwa na mamlaka iiswe sababu ya wewe kuoandisha mabega na kumsahau
Mungu wako.
Lengo la kukuonesha utofauti wa mamlaka hizi ni kujua namna
ya kwenda nazo maana kila mlango unafunguo zake maana huwezi tumia funguo za
Bedroom ili kufungulia stoo uwe na uhakika hazitafungua.
Yakobo 5:15 Biblia inasema kuomba kwake mwenye haki kwafaa
sana akiomba kwa bidii maana maombi kama hayo yanaweza mfungua mgonjwa na
kumponya magonjwa yake na kusamehewa dhambi zake. Kwa hiyo unaweza kumuombea
Mtu hata kama hana mpango wa kutubu ila kwa sababu wewe umeomb Mungu anamsamehe
kabisa.
Ndio maana Mungu anatumia kuhani na kuwaombea watu au
kufanya upatanisho na namna ya kufanya toba ili Mungu aje na atengeze hapo
mahali ambapo pana dhambi.Unahitaji kujua sana siri hii ya kufanya maombi
ambayo yatashughulika na chanzo cha maradhi au magonjwa mabacho ni dhambi.
6: MAMLAKA JUU YA
MALANGO YA ADUI.
Mwanzo 22:17 Uzao wako utamiliki malango ya adui. Galatia
3:13,14,29 Biblia inasema amelaaniwa yuke angakue juu ya mti, na Yesu
alifanyika laana ili kwa ajili yake ili sisi tupate neema ya kufikiwa na Braka
za Ibrahimu ambazo Mungu alituahidi kwa watu wa Duniani kote.
7: MAMLAKA JUU YA
MIJI.
Luka 19:16-19 Habari za Yule kabaila au kwa lugha ya sasa
tungemwita Mwekezaji na wale watu walipewa yale mafungu ya fedha.
Mafungu 10 alileta faida mara 10 na akapewa mamlaka juu ya
miji kumi.
Mafungu 5 alileta faida mara 5 na akapewa mamlaka juu ya
miji mitano.
fungu 1 alileta Hakuleta faida yoyote bali alirudisha fedha
tu na haikuwa na faida na akinyimwa mamlaka juu ya miji.
Uaminifu juu ya fedha hauleti mamlaka bali uaminifu juu ya
matumizi ya fedha ndio unaleta mamlaka juu ya miji.Mwekezaji anaanza
kuheshimika kwenye jamii au mji aliopo kwa sababu ya kuwa na fedha. Kwa hiyo
hata dini yake nayo inapata sauti kila mtu ataanza kuiheshumu. Usijulize hili
ni swala la ulimwengu wa Roho.
8: MAMLAKA JUU YA
MIFUMO YA KIUTAWALA YA WANADAMU.
Waefeso 2:6. 6Mungu alitufufua pamoja na Kristo na
kutuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho katika Kristo Yesu
Waefeso 1:20-23 20ambayo aliitumia alipomfufua Kristo kutoka
kwa wafu, akamketisha mkono Wake wa kuume katika mbingu, 21juu sana kuliko
falme zote na mamlaka, enzi na milki na juu ya kila jina litajwalo, si katika
ulimwengu huu tu, bali na katika ule ujao pia. 22Naye Mungu ameweka vitu vyote
viwe chini ya miguu Yake na amemfanya Yeye awe kichwa cha vitu vyote kwa ajili
ya Kanisa, 23ambalo ndilo mwili Wake, ukamilifu Wake Yeye aliye yote katika
yote.
Ufalme wa wadamu umetambulishwa kama NGUVU AU USULTANI
lakini vyote ni ufalme wa wanadamu.
Soma Ufunuo 17:1-2
9: MAMLAKA JUU YA
MAENEO MUHIMU YENYE MAKUSNYIKO YA WATU.
Ufunuo 5: 9-12 Wanamiliki juu ya
i) Kabila
ii) Lugha
iii) Jamaa/ukoo
iv) Taifa.
Ufunuo 17:15-
Ndio maanampinga kristo anafuatilia juu ya soko yaani kuuza
na kununua kila sehemu yeye anafuatilia hasi kwenye mitandao. Soma Ufunuo 13.
10: MAMLAKA JUU YA
KILA FIKRA.
2Wakorintho 10:3-5 3Ingawa tunaishi duniani lakini
hatupigani vita kama ulimwengu ufanyavyo. 4Silaha za vita vyetu si za mwili,
Bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome. 5Tukiangusha mawazo na kila
kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu na tukiteka nyara kila
fikira ipate kumtii Kristo
Jiulize swali hili je kuna fikra ngapi ambazo hazimtii
kristo na je sisi tumechukua hatia gani ili kuzifanya zimtii kristo. Chukua
hatua kushughulika na kila fikra isyomtii kristo na iweze kumtii kristo.
11: MAMLAKA JUU YA
ULIMI NA KINYWA CHAKO.
Yakobo 3:1-12 Mtu Yupo kama meli, mtu atakula matunda ya
kinywa chake. Kwa hiyo hata ndoa nyingi huvunjika kwa sababu ya maneno na hadi
hufika hatua ya kusambaratika kabisa.
Ulimi ni Karamu na Roho Mtakatifu ni wino. Kwa hiyo kuwa makini sana na matumizi ya ulimi wako.
0 Comments