Follow us

SOMO: KUVUNJA MAAGANO YA KICHAWI

Tangazo

 

MCHUNGAJI LAURENT MPOMA
(NCHI YA UKOMBOZI MINISTRY)

SOMO: KUVUNJA MAAGANO YA KICHAWI

Maagano:  ni makubaliano au mikataba au mafungamano yanayowekwa kati ya pande kuu mbili au zaid ya mbili ili kupata kitu fulani au kufikia hatua fulani..

Maagano yanaweza kufanyika katika majina, vyakula, sehemu watu wanayoishi, uzao fulani n.k

 mwanzo 17:1-8, mwanzo 15:4-7, mwanzo 21:18.

Koo nyingi ndani ya africa zilikuwa zikitumaini katika miungu kama vile mawe,miti mirefu,nyoka wakubwa,vinyago na aina nyingine nyingi za miungu kutokana na mazingira waliokuwa nayo.lakini ukweli na kwamba hizo zote n njia tofauti tofaut za kumuabudu shetani...akitoa baraka zake kupitia vitu hivo ambavyo waanzilishi wa koo zetu walikuwa wameweka tumaini.

Kila agano la kiimani lina matokeo yake: nayo matokeo hayo yanadumu katika vizazi vinne (kutoka 20:5, yoeli1:3)

MATOKEO YA MAAGANO KATI YA SHETANI NA MWANADAMU:

1). Magonjwa ya kurithi

2). Matukio mabaya ya kurithi kama vile ajali katika mtindo fulani, kupata ukilema,majanga ya kufanana yanayojirudia rudia katika kizazi fulani..n.k

3). Kuishi sehemu/mji mmoja tu ukoo mzma.

4). Kuvunjika kwa ndoa kwa watu wa vizazi vya ukoo husika.

5). Kufanya kazi moja tu hatakama inawafanya kuwa maskini,,,,mfano....kama mwanzilish wa uko alikiri kwa kinywa chake kuwa yeye na uzao wake kazi yao n kilimo cha jembe la mkono tu, au n wapiga debe tu n.k

6). Kutofanikiwa katika ajira, masomo na shughuli zingine( kama mmoja kati ya waanzilishi wa ukoo husika aliudhiwa na kutamka kuwa"na tuone kama watafanikiwa" ambayo n maagano katika maneno.

FAIDA ZA MAAGANO KATI YA MUNGU NA MWANADAMU:

1).Utabarikiwa kama vile mjini, mashambani, utoKapo, Uingiapo n.k

2). Uzao wa tumbo lako utabarikiwa,

3).kapu lako la kukandia (maana nyumba yako haitaon Njaa kamwe.

4).utaheshimishwa n.k

 Yoeli 2:12, torati 28

 SIFA ZA MAAGANO

Maagano lazima yawekwe kwa gharama kubwa na pia hulindwa kwa gharama pia.

Kwa mfano maagano kati ya koo zetu za kiafrika na shetani kupitia mawakala wake kama vile mawe, milima,miti mikubwa,vibuyu na masanamu, yaliweza kuwekwa kwa kutumia sadaka ambazo n kama vile damu ya wanyama, fedha, vyakula, pombe, maneno ya kujifunga n.k

Hapo wakisaidiwa kupata mvua, mavuno mazuri na kuishi salama kumbe huo ulikuwa n ubatili wa shetani na mtego wa kuzinasa koo zetu katika utawala wake

Tofauti kati ya maagano baina ya Mungu na shetani :

1).Agano kati ya shetani na Mwanadamu:

1.      Faida zake hudumu muda mfupi na madhara yake n ya muda mrefu zaidi.

2.      lengo lake n kuzima mafanikio ya mwanadamu kwani anajuwa ukifanikiwa utaweza kufanya mamb ya kumdharirisha kama vile kujenga nyumba za ibada, kusaidia wajane, kutojihusisha na dhamb kama vile dhuluma, wizi ni

2) sifa zaAgano kati ya mwanadamu na Mungu.

1.      Faida zake hudumu milele hata milele.

2.      Hufanywa kwa hiari na uhuru wa kuchagua

3.      Daima hulinda utakatifu wa Mungu.

Kama vile ambavyo nchi haiwez kukaa bila uongozi na hivo hivo ukoo/familia haiwezi kukaa bila uongozi:

Kwahio ni muhimu kujitambua kuwa nyie mupo katika uongozi wa nan ?? N Mungu au shetani?? Kama hamuridhik na uongoz wa roho moja kati ya hizo ndipo harakti za kuvunja mmoja na kujenga mwingine huanza mara moja kisha wahusika waendelee mbele katika maisha yao ya ndoa,kiuchumi,kisiasa na mengine yenye mafanikio na baraka tele.

Bila shaka watu huvunja uongozi wa shetani na kujenga uingozi wa kimungu katika koo/familia zao!

namna ya kuvunja maagano ya kishetani/mizimu.

1). Hatua ya kwanza lazima wahusika wa ukoo huo wawepo na kama sio wote wawepo hata wawakilishi wake wakiume kwa maana urithi upo kwa ukoo wa baba na sio mama (evidenced@ Daniel 9, nehemia1:1...,

2). Kukiri kwa vinywa vyenu kuwa mumetenda uovu mwingi kwa kumtegemea shetani/mizimu na sio Mungu wa mbinguni mukitaja na hayo yaliofanywa kwa wakati huo kama mulisimuliwa au munakumbuka.

3). Kusogeza sadaka toka katika vitu vyenu mulivovipata kiharali kama vile pesa,sehemu ya mazao yenu kama mchele,mahindi mihogo n.k kwani babu zetu walitumia hivyo kuweka maagano na shetani ilaa sisi tunavikusanya leo kwajili ya kuvunja. Pia ipo sadaka kubwa kupita zote nayo n damu ya Yesu. Munatakiwa kuiita kwa imani ili ishuke...hivo itapendeza kama wote au baadhi yenu mutakuwa mumefunga na kujitakasa. Hiyo damu ya yesu itatumika kuvunja na kubomoa ufalme wa mizimu.


>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>

MAOMBI NA MAOMBEZI

WASILIANA NA MCHUNGAJI MPOMA 0762756542

WATSAP 0762756542

TUMA MAHITAJI KWA E-MAIL: mchungajilaurent@gmail.com


fika : NCHI YA UKOMBOZI MINISTRY - MWAJA KITOPE SINGIDA MJINI.

Post a Comment

0 Comments