Follow us

MAMBO 6 YA KUFANYA IKIWA HALI YAKO YA MAOMBI SIO NZURI.

Tangazo



MAMBO 6 YA KUFANYA IKIWA HALI YAKO YA MAOMBI SIO NZURI.

JAMBO LA 1: Omba toba ili Mungu akusamehe! Ndiyo - omba toba ili Mungu akusamehe kwa kushindwa kuomba! Swali unaloweza kuuliza, ni kutaka kujua ikiwa kutokumwomba Mungu ni dhambi.

1Samweli 12:23. Iwe ni kutokuwaombea wengine au kutokujiombea wewe - kutokuomba ni dhambi! Kutokumwomba Mungu si udhaifu bali ni dhambi! Udhaifu katika maombi ni kule kutokujua jinsi ipasavyo! Ndiyo maana imeandikwa.

1Yohana 3:4 dhambi ni uasi au ni kwenda kinyume cha maelekezo ya Mungu. Kuomba ni agizo na mwaliko kutoka kwa Mungu, ili upate kuongea naye. Kutokumwomba ni kukataa mwaliko huo; na ni sawa na kukataa kutii agizo la Mungu. Kwa hiyo kutubu ili usamehewe kwa kutokumwomba ni hatua sasa. Mungu atakusamehe, na kurudisha ndani yako hamu ya kuomba.

 

JAMBO LA 2: Ondoa hali ya kujihukumu moyoni mwako! Kujihukumu moyoni mwako kunakuondolea ujasiri wa kwenda mbele za Mungu na kuomba.

 1Yohana 3:21,22. "Wapenzi, mioyo yetu isipotuhukumu, tuna ujasiri kwa Mungu; na lolote tuombalo, twalipokea kwake....(Huu ni mstari unamhusu yule anayeshindwa kuomba, au kwa sababu anadhani ya kuwa hata baada ya kutubu Mungu hajamsamehe)

JAMBO LA 3 : "Funga katika nafsi yako"! Hebu soma mstari huu: "Nalijitesa nafsi yangu kwa kufunga; maombi yangu yakarejea kifuani mwangu"(Zaburi 35:13).

Daudi aliyasema hayo alipokuwa anatafuta utatuzi wa yeye kushindwa kuomba kama alivyokuwa anaomba huko nyuma! Daudi anasema kufunga katika nafsi yake, kulisaidia kurejesha tena maombi kifuani mwake! Na wewe wewe unaweza ukatumia mbinu kama hii, ili kurudisha tena uwezo wako wa kuomba!

JAMBO LA 4 : “Fanya maamuzi thabiti moyoni mwako kuwa utakuwa mwombaji!”

Fahamu hili ya kuwa: Kufanya maombi ni maamuzi kwanza, kabla hakijawa kitendo! Kufanya maombi ni jambo la moyoni kwanza, kabla halijawa jambo la mdomoni! Ikiwa huna maamuzi thabiti moyoni mwako ya kuwa mwombaji, ina maana na kuomba kwako kutakuwa kwa matatizo.

“Lakini akiiona ahadi ya Mungu hakusita kwa kutokuamini, bali alitiwa nguvu kwa Imani, akimtukuza Mungu; huku akijua ya kuwa Mungu aweza kufanya yale aliyoahidi”. (Warumi 4:20,21).

JAMBO LA 6: Je, umepita au unapita kwenye taabu maishani mwako, kiasi kwamba huwezi kuomba, kwa sababu nafsi yako imakataa kufarijika?

Daudi aliwahi kukumbana na tatizo kama hili maana anatuambia hivi: “Siku ya taabu yangu nalimtafuta Bwana, mkono wangu ulinyoshwa usiku, haukulegea, nafsi yangu ilikataa kufarijika. Nilipotaka kumkumbuka Mungu nalifadhaika, nilipotaka kutafakari roho yangu ilizimia. Ulizishika kope za macho yangu zisifumbike, naliona mashaka nisiweze kunena” (Zaburi 77:2-4). Ni wazi kwamba taabu alizokuwa anapitia Daudi, ziliumiza nafsi yake, na nafsi yake ikakataa kufarijika, na mwisho wake alishindwa kuomba.

MAOMI A MAOMEZI

WASILIANA NA MCHUNGAJI LAURENT MPOMA

SIMU: +255762756542

WATSAP: +255762756542

YOUTUBU : Upenyo wa Mungu Tv

Post a Comment

0 Comments