MAOMBI YA KUFUTA DUA ZA KIPEPO ULIZOHUSISHWA.
Dua ni nini?
Dua ni maneno unayowasiliana na
MUNGU.
Dua ya kishetani ni nini?
Dua ya kishetani ni maneno unayowasiliana na
mashetani.
Shetani ni baba wa uongo, hivyo
wanaomtumainia wako katika njia isiyo sahihi.
Yohana 8:44 ''Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na
tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo;
wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo
uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa
huo.''
Dua hizo za giza zinaamsha majini
kufuatilia watu na kuwatesa sana katika maisha yao, MUNGU anakataza wanadamu
kujihusisha na nguvu za giza ikiwemo dua ya kipepo, mfano dua ya wafu.
Kumb 18:10-13 '' Asionekane kwako mtu ampitishaye
mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu
atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri, wala mtu alogaye
kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye
wafu. Kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa BWANA; kisha ni kwa sababu ya
hayo BWANA, Mungu wako, anawafukuza mbele yako. Uwe mkamilifu kwa BWANA, Mungu
wako.''
KUOMBA WAFU, HIYO NI DUA YA KIPEPO.
Biblia
inasema kwamba Wafu hawajui lolote hata moja.
Mhubiri 9:5 '' kwa sababu walio hai wanajua ya
kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena;
maana kumbukumbu lao limesahauliwa.''
na
wanaowaomba wafu wanajua kabisa kwamba wafu hawajui lolote na hawana msaada
hata mmoja kwa mwanadamu anayeishi duniani, lakini kwa sababu shetani ni baba
wa uongo kuna watu matokeo ya kishetani hutengenezwa na majini kupitia ibada
hizo, na mtu huyo huanza kufuatiliwa na majini katika maisha yake.
Leo kumejaa
dua nyingi za kipepo na hizo zinatesa maisha ya wengi.
Kuna watu
wana matambiko ya ukoo, familia au kabila na hayo hujumuisha dua ambazo ni
mlango wa shetani kuwatesa watu hao. Kuna watu huenda kwa waganga na huko dua
za kipepo husomwa na kufunga maisha ya watu.
Ndugu leo
futa dua zote za kishetani ulizohusishwa.
Jitenge na
maagano ya giza yaliyotokana na dua za kichawi.
Ndugu mmoja
alisoma hadi chuo kikuu huku baadhi ya ndugu zake na majirani wakiwa na hasira
kwa sababu baba yake mzazi alikuwa anawalingishia watu hao kwamba mtoto wake
akimaliza chuo atapata kazi nzuri na kuinua familia hiyo. Baada ya kumaliza
masomo yule kijana, katika hali isiyo ya kawaida vyeti vyake vya masomo
viliibiwa na kupelekwa kusomewa dua kwa mganga ili asipate kazi, kisha
vikarudishwa huku akiambiwa kwamba vimesomewa dua hivyo kuhusu kazi asahau.
Ndugu ilichukua zaidi ya miaka 8 akitafuta kazi bila mafanikio.
Dua za
kipepo ni mbaya sana sana na leo futa dua zote za giza zilizosomwa ukihusishwa
wewe ili usifanikiwe katika jambo fulani maishani mwako.
Inawezekana
hata wewe kikwazo katika maisha yako ni dua ya kipepo uliyosomewa.
Kuna watu
walisomewa dua ili wasifunge ndoa au wasizae, Leo kwa damu ya YESU KRISTO futa
kila dua ya kipepo.
Kuna watu
walisomewa dua ili wawe vichaa, leo futa kila dua ya kichawi, kwa maombi yako
katika jina la YESU KRISTO.
Zamani za
mitume kuna watu waliokoka na kuleta zana zao za kichawi, vitabu vyao vya
kichwai ili vichomwe moto.
Matendo 19:19-20 ''Na watu wengi katika wale
waliotumia mambo ya uganga wakakusanya vitabu vyao, wakavichoma moto mbele ya
watu wote; wakafanya hesabu ya thamani yake, wakaona ya kwamba yapata fedha
hamsini elfu. Hivyo ndivyo neno la BWANA lilivyozidi na kushinda kwa nguvu. ''
Vitabu vya kiganga na kichawi ni
ibada ya shetani na vitabu hivyo hutumika katika dua za giza.
Wasoma dua za kipepo huhusisha vitabu
vya kiganga na kichawi.
Hakikisha
katika maisha yako hushiriki ibada hizi za giza na kama wamekufunga kipepo kwa
dua za giza, leo zifute dua hizo kwa damu ya YESU.
Kumbuka
ulimwengu wa roho unaenda kwa matamsha hivyo inawezekana unateseka kwa sababu
ulitamkiwa mabaya, mabaya hayo ndio dua za giza.
MADHARA YA DUA ZA GIZA.
1.Ni dhambi kwa MUNGU aliye hai.
Isaya 8:19 ''Na wakati watakapokuambia, Tafuta
habari kwa watu wenye pepo na kwa wachawi; waliao kama ndege na kunong'ona; je!
Haiwapasi watu kutafuta habari kwa MUNGU wao? Je! Waende kwa watu waliokufa kwa
ajili ya watu walio hai? ''
2. Ni ibada ya kishetani ambayo Mcha
MUNGU hatakiwi kuhusika.
Walawi 19:31 '' Msiwaendee wenye pepo, wala wachawi;
msiwatafute; ili kutiwa unajisi na wao; Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.''
3. Hutengeneza maagano ya kishetani.
1 Kor 10:20 '' Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo
sadaka wavitoa kwa mashetani, wala si kwa MUNGU; nami sipendi ninyi
kushirikiana na mashetani. Hamwezi kunywea kikombe cha BWANA na kikombe cha
mashetani.''
4. Ni kujiunganisha na shetani ili
awe na uhalali kwako.
1 Kor
10:14-15 '' Kwa ajili ya hayo, wapenzi wangu, ikimbieni ibada ya sanamu. Nasema
kama na watu wenye akili; lifikirini ninyi ninenalo. ''
Inawezekana
wewe umewahi kushiriki dua hizi za giza, tubu kwa ajili ya hilo na jitenge kwa
jina la YESU KRISTO na hiyo dua ya giza.
Inawezekana wewe hujawahi kushiriki
dua hizi za giza lakini wapo watu wasiokutakia mema ambao walifanya dua hizo
ili zikupate, futa dua hizo kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kumbuka hizi
ni zama za mwisho na mafundisho ya mashetani ni mengi kama Neno la MUNGU
linavyosema katika 1 Timotheo 4:1
kwamba ''Basi ROHO anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine
watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya
mashetani; ''
Watu wengi
leo wamewaendea makuhani wa kishetani ambayo husoma dua hizo za giza. Makuhani
wa giza wasoma dua ni waganga wa kienyeji, wachawi, wanajimu, wasihiri na wakuu
wa giza wote.
Leo hata
kanisa la MUNGU linashirikishwa katika ukumbi mmoja au uwanja mmoja na watu
wenye Mungu mwingine ili kuomba maombi fulani, hapo kila imani na MUNGU wao,
ndugub jitenge na dua za giza.
Maombi ya leo.
1. Futa kwa damu ya YESU KRISTO kila
dua ulishiriki au uliyohusishwa.
2. Futa kwa damu ya YESU KRISTO
kilichobebwa na dua za giza ulizohusishwa.
3. Futa maagano ya kishetani
yaliyotokana na madhabahu za giza zilizosoma dua ya giza kukuhusu.
4. Haribu majini wote waliofanyia
kazi dua za kishetani zilizofanyika kwa ajili yako au kwa ajili ya watu
wanaokuhusu.
5. Batilisha kila mipango ya giza
inayotokana na dua za giza.
Natamani niseme mengi mno lakini
naamini mwenye kuelewa ameelewa.
MUNGU akubariki kwa kujifunza somo
hili muhimu.
Hapa chini ni MAOMBI YA KUFUTA DUA ZA
KIPEPO ULIZOHUSISHWA.
Maombi haya
naomba yamsaidie mtu yule ambaye hajui kuomba ili katika kuomba kwa kutumia
hayo basi atakumbuka mahitaji yake na kuyataja katika maombi yake. Haya hapa
chini ni maombi ya kuanzia tu katika maombi yako ili uendelee zaidi kuomba
Kwa waombaji
wazoefu naamini baada tu ya kulisoma somo na kulielewa basi anajua aombee nini
maana alikuwa anaandika points za kuombea.
MAOMBI YA KUFUTA DUA ZA KIPEPO
ULIZOHUSISHWA.
Wewe MUNGU
Baba ni wa tahamni sana na ninakushukuru sana kwa kunilinda na kunipa uzima.
Nikiwa na wewe YAHWEH MUNGU wangu ni
bora kuliko vyote maishani mwangu.
Niko mbele
zako MUNGU wangu ninaomba unisamehe kwa dua ya kipepo yeyote ambayo mimi
binafsi nilishiriki katika dua hiyo, nisamehe MUNGU wangu na ninatubia dhambi hiyo. Damu ya YESU kristo Mwokozi
itakase roho yangu na nafsi yangu na kila dua ya giza iyaachie maisha yangu
sasa, katika jina la YESU KRISTO.
Ninatubu
MUNGU wangu kwa ajili ya dua za kipepo walizoshiriki mababu zangu na wazazi
wangu, mahali popote niliposhikilia na dua hizo za giza naomba kwa Neema yako
Bwana YESU niachiliwe huru leo.
Kila dua
yenye hukumu ndani yake, ninatubu kwa ajili ya dua hiyo na kwa neema yako Bwana
YESU ninaomba hukumu hiyo ifutike na isiyaguse tena maisha yangu.
Nafuta kila
dua ya giza iliyotamkwa na wachawi au na majini kunihusu, naifuta dua hiyo kwa
damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila dua ya
giza iliyotamkwa na wanadamu kunihusu mimi, naifuta dua hiyo kwa damu ya YESU
KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila dua ya
kichawi iliyofanywa na wasionitakia mema, naifuta dua hiyo kwa damu ya YESU KRISTO
na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila dua ya
giza iliyotajwa na wanaotaka nifukuzwe kazi au nifilisike biashara, naifuta dua
hiyo kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila dua ya
kishetani aliyotamkiwa baba yangu au mama yangu ambayo na mimi nahusika kama
sehemu ya uzao wao, naifuta dua hiyo kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la
YESU KRISTO.
Dua za
kunizuia kufunga ndoa, naifuta dua hiyo kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la
YESU KRISTO.
Dua za
kunizuia kuzaa,naifuta dua hiyo kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU
KRISTO.
Dua za
kunizuia kuishi maisha ya amani na furaha katika ndoa, naifuta dua hiyo kwa
damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Dua ya
kunifanya nifuatiliwe na majini, naifuta dua hiyo kwa damu ya YESU KRISTO na
kwa jina la YESU KRISTO.
Kila dua ya
kichawi iliyotamkwa na mchawi, mshirikina, mwanga, mgangaa wa kienyeji au mkuuu
wa giza yeyote, naifuta dua hiyo kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU
KRISTO.
Kila adhabu
iliyobebwa na dua za kichawi dhidi yangu, hiyo adhabu naifuta kwa damu ya YESU
KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila adhabu
iliyo katika dua za giza kunizuia kupata kazi au kufanikiwa, hiyo adhabu
naifuta kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila hukumu
ya kipepo iliyotokana na dua za giza, hiyo adhabu naifuta kwa damu ya YESU
KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila
kilichobebwa katika dua za kishetani ninakiharibu hicho kwa jina la YESU
KRISTO.
Kila agano
la giza lililo katika dua ya kishetani kunihusu, hilo agano nalifuta kwa damu
ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
Kila agano
la kipepo la kunifanya nidharauliwe na kuonewa,hilo agano nalifuta kwa damu ya
YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
Kila agano
la kunizuia kusonga mbele katika biashara na maisha yangu, hilo agano nalifuta
kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
Kila agano
la kunifanya niwe mtumwa wa shetani, hilo agano nalifuta kwa damu ya YESU
KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
Kila agano
la kunifanya niwe wa kuonewa tu kipepo na wachawi kila siku, hilo agano
nalifuta kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
Kila agano la giza lolote
lililotokana na dua za giza,
hilo agano
nalifuta kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
Sasa katika
jina la YESU KRISTO nafanyika silaha ya MUNGU kwa ajili ya kuharibu majini wote
wanaotumika kunifuatilia na kufuatilia maisha yangu na baraka zangu, Kama Neno
linavyosema katika Yeremia 51:20-22
kwamba '' Wewe u rungu langu na silaha zangu za vita; kwa wewe
nitawavunja-vunja mataifa; na kwa wewe nitaharibu falme; na kwa wewe
nitamvunja-vunja farasi, na yeye ampandaye; na kwa wewe nitalivunja-vunja gari
la vita, na yeye achukuliwaye ndani yake; na kwa wewe nitawavunja-vunja
mwanamume na mwanamke; na kwa wewe nitawavunja-vunja mzee na mtoto; na kwa wewe
nitawavunja-vunja kijana mwanamume na kijana mwanamke; ''
Sasa kwa
mamlaka ya jina la YESU KRISTO ninawaadhibu majini wote waliotumwa kipepo
kupitia dua za giza ili wanitese na kutesa fursa zangu, nawapiga kwa moto wa
jina la YESU KRISTO sasa.
Kila jini
aliyejificha katika mwili wangu ili kuleta magonjwa, Nampinga jini huyo na
kumfukuza, kwa jina la YESU KRISTO Mwokozi wangu aliye hai.
Kila jini
aliyejificha katika ndoa yangu ili kuleta migogoro, Nampinga jini huyo na
kumfukuza, kwa jina la YESU KRISTO Mwokozi wangu aliye hai.
Kila jini
aliyejificha katika bishara yangu, Nampinga jini huyo na kumfukuza, kwa jina la
YESU KRISTO Mwokozi wangu aliye hai.
Kila jini
aliyeingia uchumba wangu, Nampinga jini huyo na kumfukuza, kwa jina la YESU
KRISTO Mwokozi wangu aliye hai.
Kila jini
aliyeingilia afya yangu,Nampinga jini huyo na kumfukuza, kwa jina la YESU KRISTO
Mwokozi wangu aliye hai.
Nawapiga kwa
fimbo ya chumba sasa, sawasawa na Zaburi 2:9 Inayonipa mammlaka kwa jina la
YESU KRISTO ikisema '' Utawaponda kwa fimbo ya chuma, Na kuwavunja kama chombo
cha mfinyanzi.''
Sasa
nabatilisha kila mipango ya siri mibaya ya kunidhuru au kuniharibia maisha
yangu, naiharibu kwa jina la YESU KRISTO mipango hiyo.
Sasa mimi ni
mshindi na sitashikwa tena na dua za giza katika maisha yangu.
Asante Bwana
YESU maana umeniokoa leo na kunikomboa na sasa nimeshinda kwa jina la YESU
KRISTO.
Utukufu na
heshimu ni kwa MUNGU BABA wa
MBINGUNI.
Katika jina
la YESU KRISTO nimeomba na kupokea
ushindi.
0 Comments