MAMBO SABA (7) YA KUZINGATIA ILI MAOMBI YAKO YAJIBIWE
Maombi ni
mazungumzo kati ya Mungu na mwanadamu na huleta ushirika imara na hii
husababisha mahusiano kuimarika.
1. KUKAA NDANI YA KRISTO. (kuwa
mzabibu wa kweli)
Ni ngumu
kuishi nje y mzabibu na kuzaa matunda hivyo ili maombi yako yapate majibu
lazima ukubali kuishi ndani ya wigo na uongozi wa kumkubari Kristo na yeye kuwa
sababu ya matokeo yako unayohitaji kupitia maombi.Kuwa ndani ya wigo
kutakufanya usiwe kinyume nq yale maelekezo anayotoa
Yohana 15:7
7 Ninyi
mkikaa ndani yangu na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni lo lote mtakalo
nanyi mtatendewa.
Kukaa ndani
yake na neno lake kukaa ndani yetu basi ni rahisi kupokea as long kuna
utimilifu wa vitu hivi vyote tunavyojifunza sasa.
2. Imani ni
moja ya mambo saba ambayo ukiwa huna huwezi kupata majibu sawasawa na unacho
omba na wakati mwingine kutindikiwa na imani hufanya maombi kuharibika na
kubaki ukisubiri kitu ambacho imani yako ilishatindika.
Matayo 14:26-28
26 Lakini
wanafunzi wake walipom wona akitembea juu ya maji, waliingiwa na hofu kuu.
Wakasema, “Ni mzimu.” Wakapiga mayowe kwa hofu. 27 Lakini mara moja Yesu
akasema nao, akawaambia, “Jipeni moyo. Ni mimi; msiogope.”
28 Petro
akamjibu, “Bwana, kama ni wewe, niambie nije kwako nikitembea juu ya maji.
Kupunguka
kwa imani ya Peter ndipo kulipoleta ule uzamaji wake ukisoma mistari ya hapo
chini.Hivyo Mungu qnaweza kutoa jibu la maombi yako ila kinachoharibu ni baada
ya wewe kuanza kuwaza yale nilioomba kweli Mungu atafanya?basi unasababisha
malaika aliyekua ametumwa kuleta taarifa zenye tumaini kurudi mbinguni.imani
ikipung7q qu kuweka tashwishwi basi ni moja ya kufanya kile tunachokiomba
kisitoe majibu.
Waebrania 11:6
6 Na pasipo
imani haiwezekani kumpendeza Mungu kwa maana kila mtu anayemjia ni lazima
aamini kuwa yupo na kwamba yeye huwapa tuzo wale wanaomtafuta kwa bidii.
Marko 11:24
Kwa hiyo
nawaambieni, mnaposali na kuomba kitu, aminini kwamba mmekipokea, nanyi
mtapewa.
Ukiweka
shaka basi tayari unachafua na kuharibu maombi yako.
3. OMBA KATIKA ROHO.
Kuomba
kusiko na kikomo huomba kuliko na uendelevu,ukimruhusu roho mtakatifu
akufundishe namna ya kuomba huwezi kuacha kuomba kila muda hata umelala
utashangaa unaomba katika roho,hauchoki na hii inakua constantly,mtumishi mmoja
anasema kuomba Yesu alijua lazima kila mkristo aombe ila kule kunakoleta majibu
ni kudumu kutika kuzungumza na Mungu sababu kila unapomkumbusha nini unahitaji
ni rahisi kupewa kile kilichobora.
Waefeso 6:18
Salini
daima, mkiomba msaada wa Mungu. Salini kila wakati kwa nguvu ya Roho. Kesheni
bila kuchoka mkisali kwa ajili ya watu wote wa Mungu.
Ukiweka
limitations katika kumtafuta Mungu basi nayeye ataweka limitations pia hivyo
hebu kuomba kwetu kunakoleta majibu sio mpk watumishi humu ndani wasema maombi
wakati mwingine ona maisha yangu kama mjori wa Kristo nahitaji kumtafuta
Mungu.kuna vitu haviwi vyetu kama hatujavilazimisha kuwa vyetu kujenga
utarstibu au mazoea ya kuongea na mpenzi Yesu.
Nguvu ya
roho:hii nimeona mara nyingi kwa upande wangu najua hata kwako unaiona umelala
unashituka unakuta ulikua unaomba rohoni na kuna muda unashangaa umeshurutishwa
kuomba sio kwa kuzungumza bali kwa moyo hutoi maneno ila unaomba na unaona
unahitaji kuwa katika hali hio kwa muda mrefu.kikawaida unaweza usielewe ila
Roho Mtakatifu kuna mambo anakuvusha na anakupa ushindi kwa kisemo rahisi wa
goli la mkono bila kutumia nguvu nyingi.
4. KUSIMAMA KATIKA KATIKA NENO.
Maombi yako
ili yapate kujibiwa yanahitaji neno la Mungu,umewekeza nini unachokijua juu
yako mbele za Mungu ukitumie kukidai,je haki zako unazifahamu na unazitumiaje
kuomba.
Zaburi 119:105-106 BHN
Neno lako ni
taa ya kuniongoza, na mwanga katika njia yangu. Nimeapa na kuthibitisha kiapo
changu, kwamba nitashika maagizo yako adili.
Neno
litasimama kukutengeneza au kukuelekezq nini unapashwa kuomba mbele za Bwana
Niliwahi
kusikiliza ushuhuda wa mtu anasema kuna maombi yanahitaji majibu ya papo kwa
papo na kuna yale yanahitaji muda ili kutokea hivyo yale yanayotokea papo kwa
hapo basi yasikufanye unapoomba maombi ya kutokea baada ya miaka 10 yakufanye
usiamini Mungu atajibu,jambo zuri ni kuishi ndani ya neno na kutokutoka kwenye
kile ulichoomba na kuamini utapokea.
5. UWE MTU MWENYE KUSHUKURU.
Kuna mambo
Mungu anatufanyia bila kumuomba basi hata kwa hayo tuwe na neema ya kumshukuru
maana katika yale mambo madogo ayafanyayo basi kutafanya kuyanyunyiza yale
mambo makubwa kutokea.
Mathayo 11:25-26
Wakati huo
Yesu alisema, “Nakushukuru ee Baba, Bwana wa mbingu na dunia, maana umewaficha
wenye hekima na wenye elimu mambo haya, ukawafunulia wadogo. Naam, Baba, ndivyo
ilivyokupendeza.
Kuna mambo
hayafiki sababu hujajua namna ya kumshukuru Mungu hebu mrudishie utukufu kwa
vile alivyofanya kwako na kwa ule umbali aliokutoa ili vile vilivyokua
vimesubiria wewe kushukuru viachiliwe
Kuna watu
sio tu hawajui kumshukuru Mungu hata watu waliofanya vitu kwenye maisha yao
hawajawahi kuwambia asanteh hivyo inawawia ungumu kujua kama huyu mtu
alifurahia vacation niliyompa au extra bonus ya mshahara wake niliyoongeza
hakupenda?ndoa nyingi zinaonekana za kizamani sababu baadhi ya wanandoa
wanasahau asanteh ndio siraha ya kufichua hazina zingine kutoka kwa wenzi wao.
Ilivyo kwa
baba,mama,dada,kaka na watu wengine Mungu mwenyewe anapenda tumshukuru kwa afya
zetu,uhai ambao hatuna uwezo wa kulipia hata kwa saa moja hewa yake hivi vyote
vinaweza kukuangezea usikivu kwa Mungu akupe vile vyenye thamani ambavyo
umeomba.
6. UWE NA KAZI UNAFANYA.
Katika
utekelezaji wowote wa maombi yanahitaji mtu awe na kitu ili kupitia kile
anachoomba kibarikiwe na kifike kule wewe muombaji unaomba.Kuna watu wanaomba
kuwa wafanyabiashara wazuri wakati hata mtaji wa kuuzq karanga hana unampa kazi
Mungu ya kuangalia aanz8e wapi kukubariki,maombi yanahitaji utendaji huwezi
kutaka kuwa mtu fulani bila kuwepo na maandalizi.Anahitaji abariki uimbaji wako
anza kuimba ainue watu watakaokaa upande wako watembee na wewe,unahitaji gari
basi uwe na mradi unaoweza kukupa milioni 10 au zaidi kutokana na kile
unachohitaji,wengi tumebaki kuamini katika miujizq na kusahau kufanya kazi.
2 Wathesalonike 3:6-8
Onyo Kuhusu
Uvivu
6 Ndugu wapendwa,
katika jina la Bwana Yesu Kristo, tuna waagiza mjitenge na kila ndugu ambaye ni
mvivu na ambaye haishi kufuatana na maagizo tuliyowapeni. 7 Maana ninyi wenyewe
mnafa hamu jinsi mnavyopaswa kuiga mfano wetu. Sisi hatukuwa wavivu tulipokuwa
nanyi 8 wala hatukula chakula cha mtu ye yote pasipo kulipa. Bali tulifanya
kazi kwa juhudi usiku na mchana ili tusimlemee mtu ye yote kati yenu.
Katika
maombi mengi tunayoomba yamejaa uhitaji hivyo ili kufullfill uhitaji wetu
lazima tufanye kazi tusiwe wavivu kuwaza miujiza only doing work gives us, our
aspects of living.Hivyo ni vizuri kuwa na jambo unafanya ili kile unachoomba
kisione hata wewe muombaji unaupungufu sehemu.baraka zinatazama nini unacho kwa
ajiri ya kuikamilisha baraka ya kile ulichoomba
7. KUISHI MAISHA YALIYOJAA UPENDO.
Kuna watu
wanaomba masaa ya kutosha lakini kwa habari ya upendo kuwatendea wengine
hawana,na ubaya mkubwa wamejaa kisasi na kutokuachilia.Maombi unayoomba
hayawezi kuleta impact yoyote kama huwezi kuuapply upendo kwa watu.
1 Wakorintho 13
13 Kama
ningekuwa na uwezo wa kusema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina
upendo, nimekuwa kama kelele ya kengele au toazi. 2 Na kama nina uwezo wa
unabii, na kuelewa siri zote na maarifa yote; na hata kama nina imani kiasi cha
kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, mimi si kitu. 3 Kama nikitoa mali
yote niliyo nayo, na kama nikitoa mwili wangu uchomwe moto, kama sina upendo,
hainifaidii kitu.
4 Upendo
huvumilia, upendo hufadhili; upendo hauna wivu au majivuno.
5 Upendo
hauna kiburi na haukosi kuwa na adabu. Upendo hau tafuti kujipendeza nafsi;
haukasiriki upesi, hauweki orodha ya mabaya. 6 Upendo haufurahii mabaya, bali
hufurahia kweli. 7 Upendo huvumilia yote, huamini yote, hutumaini yote, hustahim
ili yote.
8 Upendo
hauna mwisho. Lakini penye unabii, utakoma; zikiwepo lugha zitakoma; yakiwepo
maarifa yatakwisha. Unaweza kuomba na kufanya mambo mengi yaliyo ya haki lakinj
bado ukishindwa kuwa mtu wa upendo bado huwezi kujibiwa unachokiomba,upendo
huambatana na kusamehe ukishindwa kupenda basi hata kusamehe kwako kunakua
shida.
Mt 18:22
Yesu
akamwambia, Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini.
Yesu alijua
wengi kusamehe ni ngumu hivyo alisema kuwa watu wenye kusamehe ili kusababisha
yale yafungwayo kwa kutokusamehe yasiwe kwazo kwetu.
Mungu akubariki sana kwa kufuatilia blog hii
Maombi na Maombezi
piga: +255762756542
whatsap: +255762756542
0 Comments