SOMO: MADHABAHU YA KICHAWI
Mchungaji kiongozi Laurent Mpoma
“Tena mtu
mume au mtu mke aliye na pepo, au aliye mchawi, hakika atauawa; watawapiga kwa
mawe; damu yao itakuwa juu yao.” Walawi
20:27
MAANA YA LAANA
Laana ni
zaidi ya kuwa mgonjwa. Ni pale ambapo maisha ya mtu yanakosa muelekeo; kila
unalolianza hulimalizi, ikiwa asubuhi unatamani iwe mchana na mchana unatamani
iwe usiku. Ukiwa huna watoto unawatamani ukiwapata unatamani usingekuwa nao.
Hayo ndio maisha ya laana. Yaliyojaa misukosuko, kukosa amani na furaha
kutoweka kabisa.
Laana
inaweza kumpata mtu kutoka kwa mchawi au mshirikina ambaye anakuwa na wivu juu
ya maisha yako. Ni vizuri ujue kuwa katika kila familia lazima kunakuwa na mtu
mshirikina au mchawi. Na siku zote kamba za kufungwa na mtu anayekujua
zinatenda kazi vizuri kuliko kamba za mtu asiyekujua.
Lakini laana pia yaweza kumpata mtu
anapoacha kuisikiliza sauti ya Mungu. Biblia inaeleza kwa kirefu namna maisha
ya mtu mwenye laana yalivyo.
“Lakini
itakuwa usipotaka kuisikiza sauti ya Bwana, Mungu wako, usiyaangalie kufanya
maagizo yake yote na amri zake, nikuagizazo hivi leo, ndipo zitakapokujia laana
hizi zote na kukupata. Utalaaniwa mjini,
utalaaniwa na mashambani. Litalaaniwa
kapu lako na chombo chako cha kukandia.
Utalaaniwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, maongeo ya ng'ombe
wako, na wadogo wa kondoo zako.
Utalaaniwa uingiapo, utalaaniwa na utokapo, Bwana atakuletea laana na mashaka, na
kukemewa, katika yote utakayotia mkono wako kuyafanya, hata uangamie na kupotea
kwa upesi; kwa ule uovu wa matendo yako, uliyoniacha kwayo. Bwana atakuambatanisha na tauni, hata
atakapokwisha kukuondoa katika nchi uingiayo kwa kuimiliki. Bwana atakupiga kwa kifua kikuu, na kwa homa,
na kwa kuwashwa, na kwa hari ya moto, na kwa upanga, na kwa ukaufu, na kwa
koga; navyo vitakufukuza hata uangamie.
Na mbingu zako zilizo juu ya kichwa chako zitakuwa shaba, na nchi iliyo
chini yako itakuwa chuma. Bwana atafanya
mvua ya nchi yako iwe vumbi na mchanga; itakujilia juu yako kutoka mbinguni
hata uangamie. Bwana atakufanya upigwe
mbele ya adui zako; utawatokea juu yao kwa njia moja, lakini utakimbia mbele
yao kwa njia saba; nawe utatupwa huko na huko katika falme zote za duniani. Na mzoga wako utakuwa chakula cha ndege wote
wa angani, na wanyama wote wa duniani, pasiwe na mtu wa kuwafukuza. Bwana atakupiga kwa majipu ya Misri, na kwa
bawasiri, na kwa pele, na kwa kujikuna, ambayo hupati kupoa. Bwana atakupiga kwa wazimu, na kwa upofu, na
kwa bumbuazi la moyoni; utakwenda kwa
kupapasa-papasa mchana, kama apapasavyo kipofu gizani, wala hufanikiwi katika
njia zako; nawe sikuzote utaonewa na kutekwa nyara, wala hapatakuwa na mtu wa
kukuokoa. Utaposa mke na mume mwingine
atalala naye; utajenga nyumba usiikae; utapanda mizabibu usitumie matunda
yake. Ng'ombe wako atachinjwa mbele ya
macho yako, usile nyama yake; utanyang'anywa punda wako mbele ya uso wako kwa
jeuri, usirudishiwe; kondoo zako watapewa adui zako, usipate mtu wa kukuokoa. Wanao na binti zako litapewa taifa lingine,
na macho yako yataangalia, na kuzimia kwa kuwatamani mchana kutwa; wala
hapatakuwa na kitu katika uwezo wa mkono wako.
Matunda ya nchi yako, na taabu yako yote, vitaliwa na taifa usilolijua;
utaonewa tu, na kupondwa chini daima;
hata uwe mwenye wazimu kwa yaonwayo na macho yako, utakayoyaona. Bwana atakupiga magoti na miguu kwa jipu
lililo zito, usilopata kupozwa, tokea wayo wa mguu mpaka utosi wa kichwa. Bwana atakupeleka wewe, na mfalme wako
utakayemweka juu yako, kwa taifa usilolijua wewe wala baba zako; nawe huko
utatumikia miungu mingine ya miti na mawe.
Nawe utakuwa ushangao, na mithali, na dharau, kati ya mataifa yote huko
atakakokuongoza Bwana. Mbegu nyingi
utazichukua nje shambani, lakini utavuna haba, kwa kuwa nzige watazila. Utapanda mizabibu na kuitengeza, wala
hutakunywa katika divai yake, wala kuichuma kwani italiwa na mabuu. Utakuwa na mizeituni katika mipaka yako yote
usijipake mafuta yake; kwa kuwa mzeituni wako utapukutika. Utazaa wana na binti, lakini hawatakuwa wako
wewe; kwa sababu watakwenda utumwani.
Miti yako yote, na mazao ya nchi yako, nzige watakuwa nayo. Mgeni aliye kati yako atazidi kupaa juu yako;
nawe utazidi kushuka chini. Yeye
atakukopesha, wala wewe usimkopeshe; yeye atakuwa ni kichwa, wewe utakuwa
mkia. Na laana hizi zote zitakujilia juu
yako, zitakuandama na kukupata, hata uangamizwe, kwa kuwa hukuisikiza sauti ya
Bwana, Mungu wako, kushika maagizo yake na amri zake alizokuagiza; nazo zitakuwa juu yako kwa ishara na ajabu,
na juu ya uzao wako milele; kwa kuwa
hukumtumikia Bwana, Mungu wako, kwa furaha na moyo wa kushukuru, kwa ajili ya
ule wingi wa vitu vyote; kwa hiyo
utawatumikia adui zako atakaowaleta Bwana juu yako, kwa njaa, na kwa kiu, na
kwa uchi, na kwa uhitaji wa vitu vyote; naye atakuvika kongwa la chuma shingoni
mwako, hata atakapokwisha kukuangamiza.
Bwana atakuletea taifa juu yako kutoka mbali, kutoka ncha ya dunia, kama
arukavyo tai; taifa usilolifahamu ulimi wake;
taifa lenye uso mkali, ambalo haliangalii uso wa mzee, wala halipendelei
kijana; naye atakula uzao wa ng'ombe
wako wa mifugo, na uzao wa nchi yako mpaka utakapokwisha kuangamizwa; wala
hatakuachia nafaka, wala divai, wala mafuta, wala maongeo ya ng'ombe wako, wala
wana-kondoo wako, hata atakapokwisha kukuangamiza. Naye atakuhusuru katika malango yako yote,
hata kuta zako ndefu, zenye maboma, ulizokuwa ukiziamini, zishuke, katika nchi
yako yote kila upande; naye atakuhusuru katika malango yako yote kila upande,
katika nchi yako yote aliyokupa Bwana, Mungu wako. Nawe utakula uzao wa tumbo lako mwenyewe,
nyama ya wana wako na binti zako aliokupa Bwana, Mungu wako; katika mazingirwa
na katika mkazo utakaokazwa na adui zako.
Mtu mume kati yenu aliye mwororo na laini sana, jicho lake litakuwa ovu
juu ya nduguye, na juu ya mke wa kifuani mwake, na juu ya masalio ya wanawe
waliosalia naye; hata asitake wao
mmojawapo apewe katika nyama ya wanawe atakaowala, kwa kuwa hana kitu
kilichomsalia kwake; katika mazingirwa na mkazo utakaokazwa na adui yako katika
malango yako yote. Mwanamke kati yenu
aliye mwororo na laini, ambaye hangehatirisha kuweka wayo wa mguu wake nchi kwa
umalidadi na ulaini, jicho lake huyu litakuwa ovu juu ya mume wa kifuani mwake,
na juu ya mwanawe, na juu ya binti yake,
na juu ya mchanga wake atokaye katikati ya miguu yake, na juu ya wanawe
atakaowazaa; kwa kuwa atawala kwa siri, kwa uhitaji wa vitu vyote; katika
mazingirwa na mkazo utakaokazwa na adui yako katika malango yako. Kama hutaki kutunza kufanya maneno yote ya
torati hii yaliyoandikwa katika kitabu hiki, upate kulicha jina hili la fahari
na utisho, Bwana Mungu wako;
ndipo
atakapofanya Bwana mapigo yako yawe ya ajabu, na mapigo ya uzao wako, mapigo
makubwa kwa kweli, ya kudumu sana, na magonjwa mazito ya kudumu sana. Naye atakurejezea maradhi yote ya Misri juu
yako uliyokuwa ukiyaogopa, nayo yataambatana nawe. Tena kila ugonjwa, na kila pigo yasiyoandikwa
katika kitabu cha torati hii, atakutia nayo Bwana juu yako, hata utakapokwisha
kuangamizwa. Nanyi mtasalia wachache kwa
hesabu, ninyi mliokuwa mfano wa nyota za mbinguni kwa wingi; kwa kuwa
hukuisikiza sauti ya Bwana, Mungu wako.
Tena itakuwa, kama vile alivyokuwa akifurahi Bwana juu yenu kwa
kuwatendea mema na kuwafanya kuwa wengi, ndivyo atakavyofurahi Bwana juu yenu
kwa kuwapoteza na kuwaangamiza; nanyi mtanyakuliwa katika hiyo nchi mwingiayo
kuimiliki. Bwana atakutawanya katika
mataifa yote, tokea ncha hii ya dunia hata ncha hii ya dunia; nawe huko
utatumikia miungu mingine usiyoijua wewe wala baba zako, nayo ni miti na mawe. Wala katika mataifa hayo hutapata raha iwayo
yote, wala hutakuwa na kituo cha wayo wa mguu wako; lakini Bwana atakupa huko
moyo wa kutetema, na macho ya kuzimia, na roho ya kudhoofika; na uzima wako utakuwa na wasiwasi mbele yako;
nawe utakuwa na woga usiku na mchana, wala hutaamini kamwe maisha yako; asubuhi utasema, Laiti ingekuwa jioni! Na
jioni utasema, Laiti ingekuwa asubuhi! Kwa kicho cha moyo wako utakavyokucha,
na kuona kwa macho yako utakavyoona.” Kumbukumbu
28: 15-67
Unakuta
unazaa watoto hata uwafundishe vipi hawaelewi, umekuwa mtu wa mashaka na
kuonewa, kila ukianza biashara unakuwa unaishia na madeni na kufilisika. Chanzo
ni laana hiyo, tauni inayoongelewa kwenye biblia ni magonjwa kama kifua,
mgongo, homa zinakuwa haziishi, bumbuazi la moyoi unakuwa umeeduwaa tu; unaposa
mchumba lakini mwingine anakuja kumwoa, unaanza mradi haufanikiwi, ngombe wako
anachinjwa mbele ya macho yako maana yake unapigwa roba au kabari na kuibiwa
huku unajiona,
Shida hizi
zinaweza kuwa zinakupata na hujui kwa nini au nini chanzo chake. Chanzo cha
yote haya chaweza kuwa ni laana ya wachawi.
LAANA YA KICHAWI
(Neno mchawi
limeandikwa mara nane kwenye Biblia tena kwa mkazo; neno wachawi limeandikwa
mara ishirini, uchawi mara kumi na nne, uganga mara kumi na nane, waganga mara
ishirini na moja na mapepo mara mia moja na arobaini na moja. Ni muhimu na
lazima mambo haya yahubiriwe ili watu waweze kuyaelewa na waweze kuwa huru.)
“Kisha wana
wa Israeli wakasafiri na kupanga katika nchi tambarare za Moabu ng'ambo ya pili
ya Yordani karibu ya Yeriko. Na Balaki
mwana wa Sipori akaona mambo yote ambayo Israeli wamewatendea Waamori. Moabu akawaogopa hao watu sana, kwa kuwa
walikuwa wengi; Moabu akafadhaika kwa sababu ya wana wa Israeli. Moabu akawaambia wazee wa Midiani, Sasa jeshi
hili la watu litaramba vitu vyote vinavyotuzunguka, kama vile ng'ombe arambavyo
majani ya mashamba. Na Balaki, mwana wa Sipori, alikuwa mfalme wa Moabu zamani
zile. Basi akatuma wajumbe kwa Balaamu
mwana wa Beori, hata Pethori, ulio kando ya Mto, mpaka nchi ya wana wa watu
wake, kwenda kumwita, akisema, Tazama, kuna watu waliotoka Misri; tazama,
wanaufunika uso wa nchi, tena wanakaa kunikabili mimi. Basi, njoo wewe, nakusihi unilaanie watu
hawa; maana wana nguvu kunishinda mimi. Labda nitawaweza, tupate kuwapiga,
niwafukuze watoke katika nchi yangu, kwa maana najua ya kuwa yeye umbarikiye
hubarikiwa, na yeye umlaaniye hulaaniwa.
Wazee wa Moabu, na wazee wa Midiani, wakaenda, wakichukua ujira wa
uganga mikononi mwao; wakamfikilia Balaamu, wakamwambia maneno ya Balaki. Akawaambia, Kaeni hapa usiku huu, nami
nitawaletea jawabu kama Bwana atakavyoniambia; wakuu wa Moabu wakakaa na
Balaamu. Mungu akamjia Balaamu, akasema,
Ni watu gani hawa ulio nao pamoja nawe?
Balaamu akamwambia Mungu, Balaki mwana wa Sipori, mfalme wa Moabu,
amewatuma kwangu, akisema, Tazama, kuna
watu waliotoka Misri, wanaufunika uso wa nchi; basi njoo unilaanie watu hawa;
labda nitaweza kupigana nao, na kuwafukuza.” Hesabu 22:1-11
Kwenye
ulimwengu wa rohoni kuna viashiria vinavyoonyesha mtu atakuwaje siku zijazo na
watu ambao hawakupendi wanapoona unaelekea kwenye mafanikio wanamkodisha mtu
mchawi ili akulaani. Lakini sisi tuliookolewa kwa damu ya mwanakondoo Yesu
Kristo tuna nguvu ya kuwashinda wao maana wao wanategemea hirizi, na kafara zao
lakini sisi tunamtegemea Bwana wa majeshi.
“Balaamu
akamwambia Balaki, Nijengee hapa madhabahu saba, ukaniandalie hapa ng'ombe
waume saba, na kondoo waume saba. Balaki
akafanya kama Balaamu alivyonena. Balaki na Balaamu wakatoa sadaka, ng'ombe
mume mmoja na kondoo mume mmoja juu ya kila madhabahu. Balaamu akamwambia Balaki, Simama karibu na
sadaka yako, nami nitakwenda, labda Bwana atakuja kuonana nami; na lo lote
atakalonionyesha nitakuambia. Akaenda hata mahali peupe juu ya kilima. Mungu akakutana na Balaamu; naye Balaamu akamwambia,
Nimetengeneza madhabahu saba, nami nimetoa sadaka ng'ombe mume mmoja na kondoo
mume mmoja juu ya kila madhabahu. Bwana
akatia neno katika kinywa chake Balaamu, akasema, Umrudie Balaki; ukaseme
maneno haya. Akarudi kwake, na tazama,
amesimama karibu na sadaka yake ya kuteketezwa, yeye na wakuu wote wa Moabu
pamoja naye. Akatunga mithali yake,
akasema, Balaki amenileta kutoka Aramu, Mfalme wa Moabu kutoka milima ya
mashariki, Njoo! Unilaanie Yakobo, Njoo! Unishutumie Israeli. Nimlaanije, yeye ambaye Mungu hakumlaani?
Nimshutumuje, yeye ambaye Bwana hakumshutumu?” Hesabu 23: 1- 8
Kwa hiyo
yule mtu ambaye hakupendi anamwendea mchawi halafu wanaandaa madhabahu na
kuchinja mnyama ili damu ambayo ni uhai imwagike kwenye madhabahu. Mashetani
huja kwenye ile madhabahu na kunywa ile damu inayomwagika na baadaye huelekezwa
kwako ili waje kukuwekea hiyo laana.
Yapo mambo
makubwa ambayo Mungu ameandaa kwa ajili ya maisha yako. Pale ulipo leo si kitu
kabisa ipo sehemu njema unayoelekea kesho. Mahali ambapo hutatikisika tena na
utasahau taabu yako. Wewe ambaye ni mbilikimo leo kesho utakuwa baunsa. Mungu
tunaye mtumikia ni Mungu anayejua tutokako na tuendako. Ukikubali kumsikiliza
Mungu hakika atasema na Balaam wa maisha yako kama alivyosema kipindi kile cha
wana wa Israeli; kwamba “huweezi kumlaani aliyebarikiwa.” Kama Mungu ndiye aliyekubariki sio mchawi
wala mshirikina atakayeweza kukulaani. Lakini uwe na baraka kutoka kwa Mungu
ambayo hupatikana kwa kuisikiliza sauti yake. Utakapolaaniwa na Mungu pia,
hakuna atakayekubariki ukabarikiwa.
Balaam Alikuwa ni Mchawi si Nabii wa Bwana.
Kwa nini
mchawi huyu Balaam anasikia sauti ya Bwana kama sio nabii wa Bwana? Ni kwa
sababu mtu anapoingia kwenye ulimwengu wa rohoni anakuwa anawaona wote Mungu na
malaika zake pamoja na shetani na mapepo yake. Hivyo Mungu aliingilia
mawasiliano ya Balaam na shetani na kumpa maelekezo yake kwa kuwa alikuwa
anawalinda wana wa Israeli. Balaam yeye atakuwa alidhani kuwa Mungu ni ngazi
fulani ya juu katika utawala wa shetani ambao yeye hajafikia.
Baadaye huyu
mchawi Balaam alikuja kufia mikononi mwa wana wa Israeli.
“Balaamu
naye, huyo mwana wa Beori, huyo mchawi, wana wa Israeli walimwua kwa upanga
kati ya hao wengine waliowaua.” Yoshua 13:22
Madhabahu za
Laana za Kichawi.
Wachawi
hawawezi kuloga bila madhabahu. Ili waweze kuyatuma mashetani yafanyike laana
kwenye maisha yako ni lazima madhabahu ijenge kwanza. Kisha lazima kafara
itolewe juu ya madhabahu hiyo ili ule uhai ambao umo katika damu uyahuishe yale
mashetani ambayo hufanyika laana. Pasipo hiyo madhabahu laana haiwezi kufanyika
kwako. Hivyo ni muhimu kuzishughulikia madhabahu zilizoinuliwa ili wewe
ulaanike. Zinapobomoka zile, wewe unarudi kwenye kusudi la Mungu juu ya maisha
yako.
MAOMBI NA MAOMBEZI
PIGA:+255762756542
WATSAP: +255762756542
MUNGU AKUBARIKI SANA
0 Comments