UKUAJI WA KANISA
Ukuaji wa
kanisa ni harakati za kiinjili za ukristo ambazo zinakusudia kulikuza kanisa
duniani pote.
Harakati
hizi za Ukuaji wa kanisa zilianza kwa shauku kwa Agizo kuu ..Mathayo 28:19-20 na matokeo tunaona
watu wakija kwa kristo, kimsingi Agizo hili lilikuja kwa kinywa cha Kristo
mwenyewe ambae ndie baba wa kanisa.
Lakini pia
tujue kwamba ni mapenz ya Mungu kwamba Wanaume na wanawake wanakuwa wanafunzi
wa Yesu kristo na wanachama wawajibikaji wa kristo. Na Agizo hili limetutaka
tuende ulimwenguni pote kwa watu wa aina yoyote wa rangi zote ili tuwahubili
habari njema.
Na matokeo
ya kufanya hivyo kunalifanya kanisa ulimwenguni kukua kiidadi lkn pia kwa
kanisa la mahali pamoja kukua kiidadi.
BAADHI YA NJIA ZINAZOWEZA KUKUSAIDIA
WEWE MCHUNGAJI, NABII,MTUME KTK UKUAJI WA KANISA NA HUDUMA YAKO KAMA KANISA LA
MAHALI PAMOJA
1=KUMUHUBIRI KRISTO KWA MARAFIKI NA
MAJIRANI
Hapa ni
wachungaji kuwa na mahimizo kwa washirika wao kumuhubiri kristo kwa majirani,
marafiki, wafanyakazi, wafanyabiashara, wenzao kwa njia ya ushuhudiaji mtu kwa
mtu kwa msisitizo na jambo hili kusimamiwa na wewe mwenyewe kama ndio mbeba
maono na baada ya zoez hili kulifanya kwa muda mulio upanga kimkakati utaona
jinsi huduma yako kanisa lako litakavyokua kiidadi.
2=KANISA KUWA NA VIVUTIO
Katika
kanuni hii kanisa ni Lazima liwe na mipango kwa kuwa na vitu vya kijamii kama
vivutio na vishawishi vya watu kuja na kuhamia kanisani pako, kanisa linahitaji
kuwa na program za michezo kufungua shule za awali kuwa na vikundi vizuri vya
uimbaji kama kuwa na kwaya nzuri zenye ufanisi na Ubunifu, waimbaji binafsi
wazuri na kuwa na Idara ya Kusifu na kuabudu yenye nguvu na yenye watu wabunifu
na wenye uwezo, kuandaa makongamano ya uimbaji ya mara kwa mara tukumbuke
kizazi hiki cha sasa kinalivuta sana kanisani kwenye mambo ya kawaida yenye
mivuto lkn kwa vile ambavyo tunaona vinaweza kuleta matokeo mazuri na bado
havituondoi kwenye maadili basi ni vizuri kuvitumia kwa Ukuaji wa makanisa yetu
na huduma zetu tumia Ubunifu wako kulikuza kanisa lako.
3= KUFANYA UMISHENI
Ukuaji wa
kanisa umekaa katika kufanya umisheni tena umisheni wa ndani hii kwa kufikiri
unaweza ukafikiri ni kwaumisheni ni kwa ajili ya kutoka nje ya kanisa lako au
nchi mikoa ni sawa lkn bado munaweza mukawa na programs za umisheni wa ndani
kwa kufanya huduma ya ushuhudiaji sana kuhubiri mitaani mashuleni,
mahospitalini magerezani,, nakuhakiishi kwa kufanya hivyo hao watu ambao
Utakuwa unawahubilia hayo maeneo siku wakitoka huko Lazima watakutafuta na kuja
kuabudu kanisana pako na ndio Ukuaji wa kanisa unyokwenda ktk dhana hii ya
kimisheni.
4=KANISA KUWA NA MIKUTANO NA
MAKONGAMANO
Ni Lazima
kanisa la mahali pamoja kufanya mikutano ya injili makongamano katika eneo
husika jirani na makanisa yenu ili kuliongeza kanisa kiidadi lkn pia kuwaleta
watu kwa bwana kanisa linalokosa mikutano na makongamano hata Ukuaji wake ni
mdogo sana ni Lazima pawepo na vitu kama hivi ili kulikuza huduma na ukuaji wa
kanisa la mahari pamoja,
Mwisho
kukukua kwa kanisa ndio kukua kwa nguvu kazi ya kanisa kanisa kama mapato ya
kanisa kwa hiyo sisi washirika tukishikamana na wachungaji wetu kuvisimamia
vitu hivi basi tutaliona kanisa likikua kawa kasi, ni Lazima tuwe wa mambo ya
Mungu tuhatarishe baadhi ya vitu kwa ajili ya Bwana Ukisoma histolia ya Mitume
utauona jinsi walivyo hatarisha maisha yao kwa injili tu Mungu awabariki.
MUNGU AKUBARIKI SANA KWA KUENDELEA KUJIFUNZA MANENO YA MUNGU .
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
KANISA LA ELIM PENTEKOSTE NCHI YA UKOMBOZI- MUHAWA SINGIDA MJINI.
(NENO, MAOMBI NA MAOMBEZI)
Tuna ununuzi wa vifaa kwa ajili ya Mkutano wa Injili. Unaweza kuchangia kwa ajili ya kuhubiri injili na Mungu atakutana na wewe na kuzungumza na wewe na atatenda mambo makubwa sana kwenye maisha yako kuanzia leo.
TUNAHITAJI KUNUNUA.
1. VITAMBAA VYA MADHABAHU........TSHS, 60000/=
2.MAIKI WIRELESS....4......TSHS, 240,000/=
3. MAIKI ZA WIRE......4.......TSHS, 100,000/=
4. TRUBAI...........4..........TSHS, 60,000/=
5. MABATI 20@ 27,000......JUMLA NI TSHS, 540,000/=
6. DRAMS......1........TSHS, 1,100,000/=
7.SPEAKER FIDEK 3......TSHS, 2,100,000/=
WASILIANA NA MCHUNGAJI ILI MCHUNGAJI AKUOMBEE PAPO HAPO UTAKAPOCHANGIA KIMOJA WAPO KATI YA HIVYO HAPO JUU AU CHOCHOTE ULICHO NACHO TUNAPOKEA.
MUNGU AKUBARIKI SANA, AKUFUNGUE KWENYE HILO UNALOPITIA, MUNGU AKUINUE KATIKA FAMILIA, UCHUMI, KAZI NA MENGINEYO UNAYOHITAJI KATIKA MOYO WAKO.
NAMBA ZINAZOTUMIKA KATIKA MCHANGO NI NAMBA ZA MCHUNGAJI TU.
1. M-PESA 0762756542.....JINA: LAURENT MPOMA
2. AIRTEL MONEY: 0782859946....JINA: LAURENT MPOMA
3: TIGO PESA: 0714890889.....JINA : LAURENT MPOMA
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
KWA MSAADA ZAIDI NA MAOMBEZI:
WASILIANA NA MCHUNGAJI AU
FIKA KANISANI,
KANISA LA ELIM PENTEKOSTE NCHI YA UKOMBOZI
(NENO, MAOMBI NA MAOMBEZI)
AU WASILIANA NASI KUPITIA
FACEBOOK: nchi ya ukombozi ministry
Follow us on YOUTUBE: Upenyo Wa Mungu Tv
TELEPHONE: +255762756542
WHATSAP: +255762756542
BLOGSPOT: NCHI YA UKOMBOZI MINISTRY
http:// nchiyaukomboziministrytz.blogspot.com/
MUNGU AKUBARIKI SANA KWA KUJIFUNZA MANENO YA MUNGU.
0 Comments