SOMO: LAANA NI NINI? NA NINI MADHARA YAKE
Laana ni nini?
Laana ni
ukosefu wa radhi za MUNGU katika jambo fulani.
Radhi ni nini?
Radhi ni
msamaha.
Hivyo laana
ni ukosefu wa msamaha wa MUNGU katika jambo fulani.
Hiyo ni
maana ya kwanza ya laana.
Maana ya pili ya laana.
Laana ni nini?
Laana ni
apizo alitoalo mtu kwa mtu mwingine ili afikwe na mabaya?
Wakristo
wengi hujitanganya kwamba hawana laana kwa sababu wamewakombolewa kutoka kwenye
laana ya torati.
Wagalatia 3:13-14 '' KRISTO alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa
alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu
aangikwaye juu ya mti;
ili kwamba
baraka ya Ibrahimu iwafikilie Mataifa katika YESU KRISTO, tupate kupokea ahadi
ya ROHO kwa njia ya imani.''
Hiyo haina
maana kwamba tufanye maovu yanayoleta laana tukijifariji kwamba tumekombelewa
kutoka laana ya torati.
Aliyekuambia
kwamba torati kazi yake ni kulaani ni nani?
Biblia hapo imeweka wazi kwamba
tumekombolewa na laana ya torati ILI BARAKA YA IBRAHIMU AMBAYO MWANZO ILIKUWA
NI YA WAISRAELI PEKEYAO, SASA KWA NJIA YA KRISTO YESU BARAKA HIYO INAHUSU WATU
WOTE WALIOKOMBOLEWA KWA DAMU YA YESU KRISTO.
Jambo la
kujua ni kwamba tumekombolewa kutoka laana ya kutengwa na MUNGU na sasa kwa
njia ya KRISTO tunatambuliwa na MUNGU kama warithi sawasawa na ahadi aliyopewa
Ibrahimu kwa wanaye.
Wagalatia 3:26-29 '' Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa
MUNGU kwa njia ya imani katika KRISTO
YESU . Maana ninyi nyote mliobatizwa katika KRISTO mmemvaa KRISTO. Hapana Myahudi wala Myunani.
Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote
mmekuwa mmoja katika KRISTO. Na kama ninyi ni wa KRISTO, basi, mmekuwa uzao wa
Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi.''
Kumbe kabla
ya Bwana YESU kutuokoa hatukuwa uzao wa Ibrahimu na hiyo ilikuwa ni laana
lakini wana YESU ametufanya sisi kuwa uzao wa Ibrahimu warithi sawasawa na
ahadi aliyoapiwa Ibrahimu na MUNGU.
Laana
ilipofutika tulihesabiwa haki kama Ibrahimu alivyohesabiwa haki kwa kumwamini
MUNGU.
Leo andiko la Wagalatia 3:13 wakristo wengi hulitumia kuonyesha
kwamba hawana laana lakini wakati mwingine maisha yao yana laana.
Kuna laana
ambazo hutolewa na wanadamu kama maapizo, ndio maana ya pili ya laana na laana
hizo zimewakamata wengi kwa sababu hawaombi na hawajui haki zao kwa MUNGU,
Wameteswa sana na laana hizo huku wakijifariji kwamba wamekombolewa kutoka
laana.
Ndugu zangu
ni muhimu kujua kwamba YESU anaweza kukutenga na laana lakini hadi ukiamua wewe
kumwita, usipomwita utabaki na laana yako.
Kuna mambo
umeyaona kwenye ndoto au maono yakionyesha wachawi au wakuu wa giza
wanakulaani, Usipoomba hakika laana hiyo itakupata huku wewe ukibaki kujifariji
kwamba umekombolewa kutoka laana.
YESU
alisemea ''Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala
wasikate tamaa-Luka 18:1''
Kama huombi
hakika laana inaweza kukupata na kukutesa huku ukiendelea kujifariji.
Ndugu mmoja
alilaaniwa kwamba hataolewa, ilipita
miaka mingi hadi alipojua kuombea kufuta laana hiyo ndipo aliolewa.
Watumishi
wengi kwa sababu labda hawajawahi kupitia laana ndio maana hufundisha kwamba
hakuna laana.
Wengine
husema kwamba agano jipya halijazungumzia laana lakini wanasahau kwamba Bwana
YESU alisema kwamba wenye laana ya MUNGU wataenda jehanamu.
Mathayo 25:41 '' Kisha atawaambia na wale walioko
mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa
milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;''
>>>LAANA KUTOKA KWA MUNGU INATENGENEZWA
NA DHAMBI USIZOTUBIA HADI KIFO CHAKO.
Kumb 28:20 '' BWANA atakuletea laana na mashaka, na kukemewa,
katika yote utakayotia mkono wako kuyafanya, hata uangamie na kupotea kwa
upesi; kwa ule uovu wa matendo yako, uliyoniacha kwayo.''
=>> LAANA YA MUNGU PIA UNAWEZA
UKAIPATA KWA SABABU YA KUTOKUTOA FUNGU LA KUMI.
Malaki 3:9
'' Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote.''
Kutokutoa
zaka kamili ni kumwibia MUNGU na jambo hilo hutengeneza laana.
Wengi
hawatoi fungu la kumi wakisingizia kwamba wamekombolewa kutoka laana ya torati
wakati Fungu la kumi lipo kabla ya torati. Akina Ibarahimu walitoa Fungu la
kumi kwa akina Melkizedeki kipindi ambacho hata torati hajapewa Musa.
Akina Yakobo
walitoa Fungu la kumi kabla hata Waisraeli hawajaenda utumwani Misri.
Mathayo 25:41 kwamba waliolaaniwa na MUNGU
watakwenda jehanamu huwa naogopa sana.
Njia ya mbinguni ni nyembamba ndio
maana hata kwa zaka tu watu hupishana na njia hiyo ya uzima.
Laana za wanadamu au majini au wakuu
wa giza haziwezi kumfanya mtu asiende uzima wa milele lakini laana kutoka kwa
MUNGU inaweza kumfanya mtu asiende uzima wa milele.
Laana kutoka kwa wanadamu na mawakala
wa shetani zinaweza kusababisha ukateseka katika maisha ya duniani, hivyo ukihisi
kuna laana inakufuatilia iwe ni kutoka kwa babu au bibi au mama au baba au
mjomba au shangazi au kaka au dada au mtoto wako hakikisha tu unatubu kwa
sababu ya kisababishi cha laana hiyo kisha ifute laana hiyo kwa maombi katika
jina la YESU KRISTO.
Laana ni jambo baya sana.
Hata makosa
ya akina adamu hayakumfanya MUNGU awalaani bali aliilaani ardhi na sio wao.
Je ni lini
uliiombea ardhi yao iliyolaaniwa ili laana iondoke kwa damu ya YESU na ufaidike
na mazao yanayotokana na ardhi yako?
Bwana YESU
analifundisha kanisa lake kupitia Mtume Paulo akisema tusiwe watu wa kulaani
watu wengine, ni heri tuwabariki na sio kuwalaani, kuna madhara makubwa
yanayotokana na laana hivyo ni heri kubariki tu.
Warumi 12:14-17 '' Wabarikini wanaowaudhi; barikini,
wala msilaani. Furahini pamoja nao wafurahio; lieni pamoja nao waliao. Mpatane
nia zenu ninyi kwa ninyi. Msinie yaliyo makuu, lakini mkubali kushughulishwa na
mambo manyonge. Msiwe watu wa kujivunia akili.Msimlipe mtu ovu kwa ovu.
Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote.''
Laana ni kitu kinachokukamata ili
usifanikiwe kwenye jambo fulani maishani mwako.
Hakikisha
laana inaondoka maishani mwako.
Kama ni
laana kutoka kwa MUNGU tubu na acha uovu huo kwa kuanza kutenda mema ayatakayo
MUNGU.
ZINGATIA HIYO ITAKUSAIDIA.
Biblia
inasema mtu akilaani mjini basi hata mashambani yaani kijijini atakuwa
amelaani.
Kama unasumbuliwa na laana unaweza
ukajaribu kufanya biashara mjini lakini hufanikiwi. Baadaea unaweza ukajaribu
kwenda kijijini labda huko utafanikiwa, kwa sababu ya laana iliyo juu yako
hakika hata kijijini hutafanikiwa.
Kuna watu hukimbilia mijini labda
wakidhani huko watafanikiwa lakini kama laana inawasumbua hakika hata waende
wapi hawatafanikiwa.
Kumb. La torati 28:16 ''Utalaaniwa mjini, utalaaniwa na mashambani.''
Dawa ya
kuondoa laana sio kuhama eneo bali ni kutubu na kutengeneza kwa KRISTO YESU
Mfalme wa uzima.
UNATAKA KUJIJUA KAMA UNA LAANA?
Kumb 28
itatujibu.
MTU MWENYE LAANA YUKO HIVI;
1. Hata ahamie eneo jingine lolote
hatafanikiwa.
Kumbukumbu la torati 28:16 ''Utalaaniwa mjini, utalaaniwa na
mashambani. ''
2. Chanzo chake cha kipato hakimpi
faida yeyote.
Kumbukumbu la torati 28:17 '' Litalaaniwa kapu lako na chombo chako cha kukandia.''
3. Uzao wake unakuwa chini ya laana
na pia Biashara au mradi anaoanzisha
hafanikiwi kwa sababu viko chini ya laana
Kumbukumbu la torati 28:18 ''Utalaaniwa uzao wa tumbo lako, na
uzao wa nchi yako, maongeo ya ng'ombe wako, na wadogo wa kondoo zako. ''
4. Kwa kosa la kumkosea MUNGU basi
mtu huyo atakuwa mtu wa kuwa na mashaka mashaka, hukemewa, Kudhalilishwa na
kutishwa bila kosa kwa sababu ya laana aliyonayo.
Kumbukumbu la torati 28:19-20 '' Utalaaniwa uingiapo, utalaaniwa na
utokapo, BWANA atakuletea laana na mashaka, na kukemewa, katika yote utakayotia
mkono wako kuyafanya, hata uangamie na kupotea kwa upesi; kwa ule uovu wa
matendo yako, uliyoniacha kwayo.''
5. Kwa Kumkosea MUNGU basi Laana yake
inaweza kutengeneza magonjwa mabaya.
Kumbukumbu la torati 28:22 ''BWANA atakupiga kwa kifua kikuu, na kwa homa, na kwa
kuwashwa, na kwa hari ya moto, na kwa upanga, na kwa ukaufu, na kwa koga; navyo
vitakufukuza hata uangamie.''
6. Kufungwa kwa baraka kutoka kwa
MUNGU.
Kumb 28:23 ''Na mbingu zako zilizo juu ya kichwa
chako zitakuwa shaba, na nchi iliyo chini yako itakuwa chuma.''
7. Kwa kumkosea MUNGU basi Mazuri
anayoyatarajia yatageuka kuwa mabaya
Kumbukumbu la torati 28:24 '' BWANA atafanya
mvua ya nchi yako iwe vumbi na mchanga; itakujilia juu yako kutoka mbinguni
hata uangamie.''
8. Kwa Kumkosea MUNGU basi Adui
kwenye ulimwengu wa roho watampiga.
Kumbukumbu la torati 28:25 '' BWANA atakufanya upigwe mbele ya adui zako;
utawatokea juu yao kwa njia moja, lakini utakimbia mbele yao kwa njia saba;
nawe utatupwa huko na huko katika falme zote za duniani.''
9. Atakuwa mtu wa kuonewa.
Kumbukumbu la torati 28:29 '' utakwenda kwa
kupapasa-papasa mchana, kama apapasavyo kipofu gizani, wala hufanikiwi katika
njia zako; nawe sikuzote utaonewa na kutekwa nyara, wala hapatakuwa na mtu wa
kukuokoa.''
10.
Kupata Hasara zisizoisha.
Kumbukumbu la torati 28:38-39 '' Mbegu nyingi utazichukua nje shambani, lakini utavuna
haba, kwa kuwa nzige watazila. Utapanda mizabibu na kuitengeza, wala hutakunywa
katika divai yake, wala kuichuma kwani italiwa na mabuu.''
11. Wageni au watu wapya wakija
wanafanikiwa lakini yeye yuko pale pale, Pia atateswa na madeni
Kumbukumbu la torati 28:43-44 '' Mgeni aliye kati yako atazidi kupaa juu yako; nawe
utazidi kushuka chini.Yeye atakukopesha, wala wewe usimkopeshe; yeye atakuwa ni
kichwa, wewe utakuwa mkia. ''
12. Akipata mali au pesa wanatokea
walaji ili asifanye chochote cha kimaendeleo.
Kumbukumbu la torati 28:50-51 ''taifa lenye uso mkali, ambalo haliangalii uso wa
mzee, wala halipendelei kijana; naye atakula uzao wa ng'ombe wako wa mifugo, na
uzao wa nchi yako mpaka utakapokwisha kuangamizwa;''
Hizi ni alama chache tu za mtu
anayesumbuliwa na laana.
Ndugu yangu ni
muhimu kujua kwamba damu ya YESU inaweza kufuta laana zote lakini ni mpaka
uombe na sio kujifariji tu.
Kanuni ya
laana ni kwamba mkubwa anamlaani mdogo hivyo na kuondoka laana kunahitajika
nguvu kubwa kuliko mtoa laana wa kidunia.
Kama laana imetoka kwa MUNGU basi
dawa ni kutubu tu kwa MUNGU na kutengeneza njia zako kwa kuanza kutenda yale
ayatayo MUNGU.
YESU KRISTO
ana uwezo wa kukuweka huru kweli kweli mbali na laana, lakini hadi uamue wewe
kuwekwa huru.
Yohana 8:36 '' Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa
huru kweli kweli.''
Ewe mteule
wa MUNGU nakuomba Mche MUNGU na timiza utakatifu wako kwa kumtii MUNGU hata
katika matoleo.
Pia usitumie
ulimi wako kulaani watu wa MUNGU bali laani shetani na jeshi lake.
Yakobo 3:9-10 ''Kwa huo(Ulimi) twamhimidi MUNGU Baba yetu, na kwa huo twawalaani wanadamu
waliofanywa kwa mfano wa MUNGU.

<<<<<MUNGU AKUBARIKI SANA KWA KUJIFUNZA MANENO YA MUNGU>>>>>>>>>>
SOMA UJUMBE HUU NI MUHIMU SANA KATIKA MAISHA YAKO LEO ILI MUNGU AKUPANDISHE VIWANGO VYA JUU.
2 Mambo ya Nyakati 1:7-12
Usiku ule Mungu akamtokea Sulemani, akamwambia, Omba utakalo nikupe. Sulemani akamwambia Mungu, Umemfanyia baba yangu Daudi fadhili kuu, nawe umenimilikisha mimi badala yake. Basi sasa, Ee BWANA Mungu, na limyakinie baba yangu Daudi neno lako; maana umenitawaza niwe mfalme juu ya watu wengi kama mavumbi ya nchi. Basi sasa nipe hekima na maarifa, nijue kutoka na kuingia mbele ya watu hawa; kwa kuwa ni nani awezaye kuwatawala watu wako hawa walio wengi? Naye Mungu akamwambia Sulemani, Kwa sababu neno hili lilikuwamo moyoni mwako, wala hukujitakia mali, wala utajiri, wala utukufu, wala maisha ya wakuchukiao, wala hukujitakia maisha ya siku nyingi; bali umejitakia hekima na maarifa, upate kuwatawala watu wangu, niliokutawaza juu yao; basi hekima na maarifa umepewa; nami nitakupa mali, na utajiri, na utukufu, kupita walivyokuwa navyo wafalme wote waliokuwa kabla yako, wala baada yako hapatakuwa na mtu atakayekuwa navyo.
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
KANISA LA ELIM PENTEKOSTE NCHI YA UKOMBOZI- MUHAWA SINGIDA MJINI.
(NENO, MAOMBI NA MAOMBEZI)
Tuna ununuzi wa vifaa kwa ajili ya Mkutano wa Injili. Unaweza kuchangia kwa ajili ya kuhubiri injili na Mungu atakutana na wewe na kuzungumza na wewe na atatenda mambo makubwa sana kwenye maisha yako kuanzia leo.
TUNAHITAJI KUNUNUA.
1. VITAMBAA VYA MADHABAHU........TSHS, 60000/=
2.MAIKI WIRELESS....4......TSHS, 240,000/=
3. MAIKI ZA WIRE......4.......TSHS, 100,000/=
4. TRUBAI...........4..........TSHS, 60,000/=
5. MABATI 20@ 27,000......JUMLA NI TSHS, 540,000/=
6. DRAMS......1........TSHS, 1,100,000/=
7.SPEAKER FIDEK 3......TSHS, 2,100,000/=
WASILIANA NA MCHUNGAJI ILI MCHUNGAJI AKUOMBEE PAPO HAPO UTAKAPOCHANGIA KIMOJA WAPO KATI YA HIVYO HAPO JUU AU CHOCHOTE ULICHO NACHO TUNAPOKEA.
MUNGU AKUBARIKI SANA, AKUFUNGUE KWENYE HILO UNALOPITIA, MUNGU AKUINUE KATIKA FAMILIA, UCHUMI, KAZI NA MENGINEYO UNAYOHITAJI KATIKA MOYO WAKO.
NAMBA ZINAZOTUMIKA KATIKA MCHANGO NI NAMBA ZA MCHUNGAJI TU.
1. M-PESA 0762756542.....JINA: LAURENT MPOMA
2. AIRTEL MONEY: 0782859946....JINA: LAURENT MPOMA
3: TIGO PESA: 0714890889.....JINA : LAURENT MPOMA
KABLA YA KUTUMA WASILIANA NA MCHUNGAJI KWA NAMBA HIZO.
MCHUNGAJI ATAFANYA MAOMBI KWA AJILI YAKO.
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
KWA MSAADA ZAIDI NA MAOMBEZI:
WASILIANA NA MCHUNGAJI AU
FIKA KANISANI,
KANISA LA ELIM PENTEKOSTE NCHI YA UKOMBOZI
(NENO, MAOMBI NA MAOMBEZI)
AU WASILIANA NASI KUPITIA
FACEBOOK: nchi ya ukombozi ministry
Follow us on YOUTUBE: Upenyo Wa Mungu Tv
TELEPHONE: +255762756542
WHATSAP: +255762756542
BLOG: NCHI YA UKOMBOZI MINISTRY
http:// nchiyaukomboziministrytz.blogspot.com/
MUNGU AKUBARIKI SANA KWA KUJIFUNZA MANENO YA MUNGU.
0 Comments