FAIDA ZA KUMTOLEA BWANA FUNGU LA KUMI
Faida za
Kumtolea Bwana Fungu la Kumi”. Mungu amezungumuzia aina mbalimbali za sadaka. Zifuaatzoni aina ya hizo sadaka:
1. AINA ZA SADAKA KIBIBLIA
(i). SADAKA YA AMANI
KUTOKA
32:6….[Wakaondoka asubuhi na mapema, wakatoa dhabihu, wakaleta sadaka za amani,
watu wakaketi kula na kunywa, wakaondoka wacheze. ]… Hizi ni aina ya sadaka za kusababisha amani ndani ya
nchi,familia. Ikikosekana amani mema hayawezi kukujia.
(ii). SADAKA YA DHAMBI.
Israeli
wakitenda dhambi, sasdaka hii hutolewa. Mnyama (ng’ombe au kondoo) huchinjwa
ili kufanya dhambi za wana Israeli
waachliwe kwenye.
HESABU 6:13-14 …[Na sheria ya Mnadhiri ni hii,
zitakapotimia hizo siku za kujitenga kwake; ataletwa mlangoni pa hema ya
kukutania; 14 naye atasongeza sadaka yake kwa Bwana, mwanakondoo mmoja mume wa
mwaka wa kwanza mkamilifu, kuwa sadaka ya kuteketezwa, na mwanakondoo mmoja mke
wa mwaka wa kwanza mkamilifu, kuwa sadaka ya dhambi, na kondoo mume mmoja
mkamilifu kwa sadaka ya amani,]….
(iii). SADAKA YA HATIA
Mtu anakuwa
ametenda mambo yenye kumtia hatia, hata akataka kujiua. Yuda Iskariote, kwa
mfano, alijisikia ndani mwake hatia kwa kumsaliti Bwana Yesu na mwishowe
akajinyonga. Wana wa Israeli pindi wanapojisika hatia ndani ya mmioyo
yaowalikuwa wanatoa sadaka ya hatia kwa ajili yao. Cha muhimu ni kuziacha njia zako mbaya ili
hatia ndani yako isiwepo. Yapo mapepo kabisa ya kutia hatia ndani yako. Hayo
ndiyo huinon’goneza masikio yako kukuambia kwamba dhambi uliyoifanya ni kubwa na
kwamba haiwezi kusamehewa.
WALAWI 5:6-7 …[naye atalipa kwa ajili ya hilo
alilolikosa katika kitu kile kitakatifu, kisha ataongeza na sehemu ya tano, na
kumpa kuhani; naye kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake kwa huyo kondoo
mume wa sadaka ya hatia, naye atasamehewa.]…. Kwa hiyo aina hii ya sadaka
huleta upatanisho.
(iv). SADAKA YA HIARI
Ni sadaka
itolewayo kwa Bwana kama hiari,ya kumshukuru
Bwana kwa mambo aliyokutendea. Haulazimiki kuitoa, ila ni kuonesha
mapenzi mema kwa Bwana, kwamba unamjali,unapenda aendelee kukuhudumia. Biblia
inasema aheri kutoa kuliko kupokea.
HESABU 29:36….[lakini mtasongeza sadaka ya
kuteketezwa, sadaka ya kusongezwa kwa moto, harufu ya kupendeza kwa Bwana;
ng'ombe mume mmoja, na kondoo mume mmoja, na wanakondoo waume wa mwaka wa
kwanza wakamilifu saba;]…
(v). SADAKA YA KINYWA
KUMBUKUMBU
32:38…[Uliokula shahamu za sadaka zao, Na kunywa divai ya sadaka zao za
kinywaji? Na waondoke na kuwasaidia
ninyi; Na wawe hao himaya yenu.]…. Baadhi ya makabila wana mila zakumwagapombe
ardhini, kama njia mojawapo ya kuwasiliana na mizimu.
2SAMWELI 23:16-17….[Basi hao mashujaa watatu wakapenya
jeshi la Wafilisti, wakateka maji kutoka kile kisima cha Bethlehemu, kilicho
karibu na lango, wakayachukua, wakamletea Daudi; walakini yeye hakukubali
kuyanywa, akayamimina mbele za Bwana. 17
Akasema, Hasha, Bwana, nisifanye hivi; je! Si damu hii ya watu hao
waliohatirisha nafsi zao? Kwa hiyo hakukubali kuyanywa. Hayo ndiyo
waliyoyafanya wale mashujaa watatu.]….
(vi). SADAKA YA KUINULIWA
KUMBUKUMBU
12:11…[ wakati huo itakuwa kwamba mahali pale atakapopachagua Bwana, Mungu
wenu, alikalishe jina lake, hapo ndipo mtakapoleta kila kitu ninachowaamuru;
sadaka zenu za kuteketezwa, na dhabihu zenu, na zaka zenu, na sadaka ya
kuinuliwa ya mikono yenu, na nadhiri zenu zote teule mtakazoweka kwa Bwana.]….
Mashambani yapo yale mazao ya kwanza kabisakuanza kukomaa, na waisraeli
wallikuwa wakito aina hii ya sadaka kwa Bwana (kama Malimbuko) kuwa sadaka ya
kutikiswa kwa Bwana. Maana yake, kila
kitui cha kwanza ni cha Bwana.
(vii). SADAKA YA KUNYWEA
Aina
hii ya sadaka hufanywa na watu, wakati
mwingine akiwa mzima hakuelezi sababu yake, bali pale akienda bar na kunywa
anakuwa na ujasiri wa kuja kwako na kueleza dukuduku zake. Nyakati nyingine anakuwepo mtu amenuna
moyoni mwake kwa sababu yako. Ni vyema
kukaa naye na kuyamaliza kabla ya kutoa sadaka zako mbele za Bwana.
Yeyote
aliyeninywea mahali popopte,nageuza majeshi yamrudie mwenyewe Kwa Jina la Yesu.
EZEKIELI 20:28…[ Kwa maana nilipokuwa nimekwisha
kuwaingiza katika nchi ile, ambayo naliuinua mkono wangu kuwapa, wakati huo
walipoona kila mlima mrefu, na kila mti wenye majani mengi, walitoa matoleo yao
huko, na huko walitoa chukizo la sadaka zao, na huko walifanya nukato la
kupendeza, na huko walimimina sadaka zao za kunywewa.]….
(viii). SADAKA YA KUSONGEZWA
WALAWI 7:30….[ mikono yake mwenyewe itamletea hizo
sadaka za kusongezwa kwa moto; mafuta yake pamoja na kidari atayaleta, ili
kwamba hicho kidari kitikiswe kuwa sadaka ya kutikiswa mbele ya Bwana.]….
(ix). SADAKA YA KUTEKETEZWA
MWANZO 22:1-2…[Ikawa baada ya mambo hayo Mungu
alimjaribu Ibrahimu, akamwambia, Ee Ibrahimu! Naye akasema, Mimi hapa. 2
Akasema, Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, umpendaye, Isaka, ukaende zako
mpaka nchi ya Moria, ukamtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima mmojawapo
nitakaokuambia.]….
MWANZO 8:20….[Nuhu akamjengea Bwana madhabahu; akatwaa katika kila
mnyama aliye safi, na katika kila ndege aliye safi, akavitoa sadaka za
kuteketezwa juu ya madhabahu.]…
Nuhu aliitoa
sadaka ya kutekekzwa juu ya madhabahu.
2WAFALME 3:26-27….[Naye mfalme wa Moabu alipoona ya
kwamba ameshindwa vitani, alitwaa pamoja naye watu mia saba wenye kufuta panga
ili wapenye hata kwa mfalme wa Edomu; wala hawakudiriki. 27 Ndipo akamtwaa
mwanawe wa kwanza, yeye ambaye angetawala mahali pake, akamtoa awe sadaka ya
kuteketezwa juu ya ukuta. Kukawa hasira kuu juu ya Israeli; basi wakatoka
kwake, wakarudi kwenda nchi yao wenyewe.]….
Vita
ilimlemea Mfalme wa Edomu na ndipo ili ashinde vita ilimlazimu kumtoa mwanae
kuwa sadaka ya kuteketezwa. Kuna watu wanatoa sadaka zao ili kuishinda vita.
Hata katika taifahili letu, wapo watu wanaowania uongozi (urais, ubunge,
udiwani n.k) kwa uchaguzi mkuu mwaka huu wakitaka kushinda kwa kutoa aina hii ya
sadaka.
(x). SADAKA YA KUTIKISWA
WALAWI 10:15….[Mguu wa kuinuliwa, na kidari cha
kutikiswa, Watavileta pamoja na dhabihu zisongezwazo kwa njia ya moto, za hayo
mafuta ili kuvitikisa viwe sadaka ya kutikiswa mbele za Bwana; kisha vitakuwa
ni vyako wewe, na vya wanao pamoja nawe, ni haki yenu milele, kama Bwana
alivyoagiza.]…
(xi). SADAKA YA SHUKRANI
Ni kuonesha
shukrani mbele za Mungu.
YEREMIA 17:26…[Nao watatoka miji ya Yuda, na
mahali palipo pande zote za Yerusalemu, na nchi ya Benyamini, na Shefela, a na
milima, na upande wa Negebu, b wakileta sadaka za kuteketezwa, na dhabihu, na
sadaka za unga, na ubani, wakileta pia sadaka za shukrani, nyumbani kwa Bwana]…
(xii). SADAKA YA UNGA
KUTOKA
40:29…[Akaiweka madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa mlangoni pa maskani ya
kukutania, akatoa sadaka ya kuteketezwa juu yake, na sadaka ya unga; kama Bwana
alivyomwamuru Musa.]…
(xiii). SADAKA YA MALIMBUKO
HESABU 15:21 ….[Malimbuko ya unga wenu mtampa Bwana
sadaka ya kuinuliwa, katika vizazi vyenu.]….
(xiv). SADAKA YA FUNGU LA KUMI
Ni sadaka
yenye mkataba/agano na Mungu. Na mungu ametoa maelekezo kwamba endapo mtu
hatatoa aina hii ya sadaka zipo adhabu zitakazofuatia baada ya yake.
MWANZO 14:20…[Ahimidiwe Mungu Aliye juu sana,
aliyewatia adui zako mikononi mwako. Abramu akampa fungu la kumi la vitu
vyote.]…. Hapa aina hii ya sadaka initwa fungu la kumi.
WALAWI 27:30…[ Tena zaka yote ya nchi, kama ni
mbegu ya nchi, au kama ni matunda ya nchi, ni ya Bwana; ni takatifu kwa
Bwana.]… Hapa aina hii ya sadaka inaitwa
‘zaka’. Ni sadaka ambayo mbele za Bwana ni ‘takatifu’, kwa ajili
ya matumizi ya kazi ya Bwana.
MWANZO 28:22…[Na jiwe hili nililolisimamisha kama
nguzo litakuwa nyumba ya Mungu; na katika kila utakalonipa hakika nitakutolea
wewe sehemu ya kumi.]…. Ni sadaka ambayo pia hujjulikna kama fungu la kumi.
Kawaida, mtu
akila vitakatifu vya Bwana hukumbana na adhabu. Vile uvifanyavyo vyaweza kufa,
ikiwemo mifugo, kazi n.k.
2. TARATIBU ZA UTOAJI WA FUNGU LA
KUMI
Ni mpango wa
Mungu wa Kuwabariki watu waliookoka.
MITHALI 15:8…[Sadaka ya mtu mbaya ni chukizo kwa
Bwana; Bali maombi ya mtu mnyofu ni
furaha yake.]…Dhambi ni kikwazo cha kupata majibu kutoka kwa Bwana.
EFESO 2:8-9…[Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa
njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; 9 wala
si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.]… Mtu hapaswi kujisifu kwamba
ameshabarikiwa, kwa sababu ni kwa neema tu. Ndiyo maana baadhi ya
watu shida haziishi miongoni mwa
waliookoka.
YOHANA 3:16…[Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda
ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali
awe na uzima wa milele.]… Hata uzimawa milele tulio nao unatokana na utoaji wa
Mungu kwa ajili yetu.
Ibrahimu alitoa fungu la Kumi (MWANZO 14:17….[Abramu aliporudi kutoka kumpiga
Kedorlaoma na wale wafalme waliokuwa pamoja naye, mfalme wa Sodoma akatoka
amlaki katika bonde la Shawe, nalo ni Bonde la Mfalme. 18 Na Melkizedeki mfalme
wa Salemu akaleta mkate na divai, naye alikuwa kuhani wa Mungu Aliye juu sana.
19 Akambariki, akasema, Abramu na abarikiwe na Mungu Aliye juu sana, Muumba
mbingu na nchi. 20 Ahimidiwe Mungu Aliye juu sana, aliyewatia adui zako
mikononi mwako. Abramu akampa fungu la kumi la vitu vyote.]…. Mungu ana uwezo
wa kuvaa mwili wa kibinadamu. Melkisededki ni mfano wa aina yake katika Biblia.
Tafsiri ya jina la huyu mfalme ndiyo inayotupa uhakika wa kuwa Mungu alijifunua
kwa namna ya kipekee.
EBRANIA 7:1-3...[Kwa maana Melkizedeki huyo, mfalme wa
Salemu, kuhani wa Mungu aliye juu, aliyekutana na Ibrahimu alipokuwa akirudi
katika kuwapiga hao wafalme, akambariki; 2 ambaye Ibrahimu alimgawia sehemu ya
kumi ya vitu vyote; (tafsiri ya jina lake kwanza ni mfalme wa haki, tena,
mfalme wa Salemu, maana yake, mfalme wa amani; 3 hana baba, hana mama, hana
wazazi, hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhai wake, bali amefananishwa
na Mwana wa Mungu); huyo adumu kuhani milele.]…. Kawaida, tafsiri ya jina la
mtu huwa moja, na hayupo mtu wa kawaida
awezaye kuwa na jina lenye maana nyingi
zaidi ya moja.
Hata katika
Agano Jipya, watu walitoa fungu la kumi.
MATHAYO 23:23…[Ole wenu waandishi na Mafarisayo,
wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira, lakini mmeacha
mambo makuu ya sheria, yaani, adili, na rehema, na imani; hayo imewapasa
kuyafanya, wala yale mengine msiyaache.]… Ni mpango wa Mungu kwa watu kutoa
fungu la kumi.
3. KAZI YA FUNGU LA KUMI
Ni
kuhakikisha kuwa nyumbani mwa Mungu pana
chakula.
MALAKI 3:8-9…[Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini
ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu. 9 Ninyi mmelaaniwa
kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote. 10 Leteni zaka kamili
ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama
sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo
nafasi ya kutosha, au la.]… Kwa hiyo mojawapo ya kazi ya fungu la kumi ni kuona
kuwa kipo chakula katika nyumba ya Bwana.
Chakula kwenye nyumba ya Bwana kina
maaba gani?
YOHANA 4:34…[Akawaambia, Mimi ninacho chakula
msichokijua ninyi. 33 Basi wanafunzi wake wakasemezana, Je! Mtu amemletea
chakula? 34 Yesu akawaambia, Chakula changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake
aliyenipeleka, nikaimalize kazi yake.]… Chakula katika nyumba ya Bwana ni
kufanya kanisani pasiwe ukiwa, bali Injili ya Mungu iweze kusonga mbele.
4. FAIDA YA KUTOA FUNGU LA KUMI
Mungu
atakaufunulia madirisha ya mbinguni. MALAKI 3:10….[Leteni zaka kamili ghalani, ili
kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama
sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo
nafasi ya kutosha, au la.]...
Mungu
atamkemea ibilisi alaye biashara zetu,
afya zetu, ndoa yak n.k. (MALAKI 3:11…[ Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye
alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha
matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa
majeshi.])….Ibilisi anakula. Kanuni inasema kuwa, Kama humtolei Bwana fungu la
kumi, basi unamtolea Yule alaye. Ndiyo maana, unamkuta mtu
Mataifa yatakuita heri. MALAKI 3:12…[Na mataifa yote watawaiteni heri;
maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema Bwana wa majeshi.]… Siyo kwamba kwa kutoa fungu la kumi,Mungu
atakupa fedha, bali atakaupa vitu vya
rohoni, mfano akili nzuri, karama, ujuzi n.k ambavyo vitawafanya watu/mataifa
kukuita heri.
5. NANI WA KUTOA FUNGU LA KUMI?
Kila mtu ana wajibu wa kutoa fungu la
kumi. 1WAFALME 17:10-14…[Basi, akaondoka, akaenda Sarepta; hata alipofika langoni pa mji, kumbe!
Mwanamke mjane alikuwako akiokota kuni; akamwita, akamwambia, Niletee,
nakuomba, maji kidogo chomboni nipate kunywa. 11 Alipokuwa akienda kuleta,
akamwita akasema, Niletee, nakuomba, kipande cha mkate mkononi mwako. 12 Naye
akasema, Kama Bwana, Mungu wako, aishivyo, sina mkate, ila konzi ya unga katika
pipa, na mafuta kidogo katika chupa; nami ninaokota kuni mbili ili niingie
nijipikie nafsi yangu na mwanangu, tuule tukafe. 13 Eliya akamwambia, Usiogope;
enenda ukafanye kama ulivyosema; lakini unifanyie kwanza mkate mdogo
ukaniletee; kisha ujifanyie nafsi yako na mwanao. 14 Kwa kuwa Bwana, Mungu wa
Israeli, asema hivi, Lile pipa la unga halitapunguka, wala ile chupa ya mafuta
haitaisha, hata siku ile Bwana atakapoleta mvua juu ya nchi.]… Siri ya kutoa
siyo kwa sababu vipo vingi, bali hata katika vidogo ni muhimu kutoa fungu la
kumi. Baraka zetu zimeambatanishwa na kutoa,
tena hasa kwa watumishi wa Bwana.
6. MSINGI WA UTEKELEZAJI KATIKA KUTOA
FUNGU LA KUMI
Kwa wale
wafanyabiashara, endapo umechukua mkopo wako benki kwa ajili ya bishara,
unapaswa kutoa sehemu ya kumi ya ule mkopo (mfano: mkopo wa sh.100,000 funugu
lake la kumi ni shs. 10,000 na hivyo mtaji wako utakuwa shs. 90,000). Endapo biashara hii itaongezeka kwa kutoa
faida. Mathalani mtaji na faida umefikia sh. 150,000, cha
kufanya hapo ni kuondoa ule mtaji lakini kwenye faida (sh.60,000) unapaswa
kutoa fungu la kumi ambalo ni sh. 6,000. Kawaida mtaji hautolewi fungu la kumi
kama awali ulishatolea fungu la kumi.
Mke asiye na
kazi, hapaswi kuigusa pesa ya matumizi anayoachiwa na mumewe ili iwe fungu la kumi. Kama mumewe ameshalipa
fungu la kumiyatosha. Hata hivyo, mume na mke wakiwa na kazi, kila mmoja
anapaswa kutoa fungu la kumi.
Mwanafunzi
aweza kutoa fungu la kumi la ile
pocket money apewayo na wazazi wake. Hata hivyo haipaswi kutoa fungu la
kumi la fedha ya ADA upewayo ukiwa mwanafunzi kulipa shuleni.
7. MAMBO YA KUZINGATIA
Fungu la
kumi hutolewa nyumbani mwa Bwana (Kanisani) mahali ambapo wewe ni mshirika, unapolelewa. Halitolewi tu kila
mahali, bali pale ambapo Bwana ametuelekeza.
Halitolewi
kwenye mikutano ya Injili, wala kwa wajane wala kwa masikini na wagonjwa
8. LAANA YA KUTOTOA FUNGU LA KUMI
ZEKARIA 5:1-4…[Basi, nikainua macho yangu tena,
nikaona, na tazama, gombo la chuo lirukalo. 2 Akaniuliza, Unaona nini?
Nikajibu, Naona gombo la chuo lirukalo; na urefu wake ni dhiraa ishirini, na
upana wake dhiraa kumi. 3 Ndipo akaniambia, Hii ndiyo laana itokayo kwenda juu
ya uso wa nchi yote; maana kwa hiyo kila aibaye atatolewa kama ilivyo upande
mmoja, na kwa hiyo kila aapaye atatolewa kama ilivyo upande wa pili. 4
Nitaituma itokee, asema Bwana wa majeshi, nayo itaingia katika nyumba ya mwivi,
na katika nyumba yake yeye aapaye kwa uongo kwa jina langu; nayo itakaa
katikati ya nyumba yake, na kuiteketeza, pamoja na boriti zake na mawe yake.]….
Haijalishi wizi unaofanyika ni wa aina gani, lakini kutotoa fungu la kumi ni
wizi kama wizi mwingine. Na adhabu ya mwiiz imeoneshwa hapa katika maandiko ya
Biblia siku ya leo.
UKIRI
Baba Mungu naomba unisamehe, kwa kuwa
nimetenda dhambi ya kutokuwa mwaminifu
kwa kutotoa zaka kamilifu, na laana
imeingia katika nyumba yangu. Leo
ninakuomba Bwana unisamehe, nilijihesabia haki kwa kuwa mimi nilikuwa
sina, lakini kumbe siri na njia ya kuwa
navyo vingi ni kutoa, kwa mfano wa Yule mama mjane aliyekubali kumtengenezea
Nabii Eliya mkate, na kwa kufanya hivyo hakupungukiwa na kitu.
Ninatubu leo dhambi ya kutokuwa
mwaminifu. Nisamehe Bwana. Kuaznia leo nitakuwa natoa zaka kwa ukamilifu wake.
Ponya ndoa yangu, ponya biashara yangu kwa kuwa imeandikwa akusamehe maovu yako
yote na kukuponya magonjwa yako yote. Naomba Bwana Yesu unisamehe katika Jina oa Yesu. Amen
MUNGU AKUBARIKI SANA KWA KUENDELEA KUJIFUNZA MANENO YA MUNGU .
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
KANISA LA ELIM PENTEKOSTE NCHI YA UKOMBOZI- MUHAWA SINGIDA MJINI.
(NENO, MAOMBI NA MAOMBEZI)
Tuna ununuzi wa vifaa kwa ajili ya Mkutano wa Injili. Unaweza kuchangia kwa ajili ya kuhubiri injili na Mungu atakutana na wewe na kuzungumza na wewe na atatenda mambo makubwa sana kwenye maisha yako kuanzia leo.
TUNAHITAJI KUNUNUA.
1. VITAMBAA VYA MADHABAHU........TSHS, 60000/=
2.MAIKI WIRELESS....4......TSHS, 240,000/=
3. MAIKI ZA WIRE......4.......TSHS, 100,000/=
4. TRUBAI...........4..........TSHS, 60,000/=
5. MABATI 20@ 27,000......JUMLA NI TSHS, 540,000/=
6. DRAMS......1........TSHS, 1,100,000/=
7.SPEAKER FIDEK 3......TSHS, 2,100,000/=
WASILIANA NA MCHUNGAJI ILI MCHUNGAJI AKUOMBEE PAPO HAPO UTAKAPOCHANGIA KIMOJA WAPO KATI YA HIVYO HAPO JUU AU CHOCHOTE ULICHO NACHO TUNAPOKEA.
MUNGU AKUBARIKI SANA, AKUFUNGUE KWENYE HILO UNALOPITIA, MUNGU AKUINUE KATIKA FAMILIA, UCHUMI, KAZI NA MENGINEYO UNAYOHITAJI KATIKA MOYO WAKO.
NAMBA ZINAZOTUMIKA KATIKA MCHANGO NI NAMBA ZA MCHUNGAJI TU.
1. M-PESA 0762756542.....JINA: LAURENT MPOMA
2. AIRTEL MONEY: 0782859946....JINA: LAURENT MPOMA
3: TIGO PESA: 0714890889.....JINA : LAURENT MPOMA
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
KWA MSAADA ZAIDI NA MAOMBEZI:
WASILIANA NA MCHUNGAJI AU
FIKA KANISANI,
KANISA LA ELIM PENTEKOSTE NCHI YA UKOMBOZI
(NENO, MAOMBI NA MAOMBEZI)
AU WASILIANA NASI KUPITIA
FACEBOOK: nchi ya ukombozi ministry
Follow us on YOUTUBE: Upenyo Wa Mungu Tv
TELEPHONE: +255762756542
WHATSAP: +255762756542
BLOGSPOT: NCHI YA UKOMBOZI MINISTRY
http:// nchiyaukomboziministrytz.blogspot.com/
MUNGU AKUBARIKI SANA KWA KUJIFUNZA MANENO YA MUNGU.
0 Comments