Follow us

MAOMBI YA UREJESHO

Tangazo

 

KUHANI: LAURENT MPOMA
KANISA LA ELIM PENTEKOSTE -MUHAWA SINGIDA MJINI
(NCHI YA UKOMBOZI)
NENO, MAOMBI NA MAOMBEZI MASAA 24

MAOMBI YA UREJESHO

UREJESHO KWENYE NDOA NA MAHUSIANO

Malaki 2:13-16. Mungu anachukia kuachana. Mungu hapendi mvurugano kwenye ndoa. Dhumuni la Mungu kuwapa ndoa ni kwamba mumzalie mtoto atakayemcha Yeye. Mwambie Mungu kuhusu ahadi hiyo na kwamba arejeshe ndoa na mahusiano yenu kwa maana yeye mwenyewe hataki kuachana kwa wana ndoa.

UREJESHO KWENYE UCHUMI NA MAISHA YAKO AMBAYO YAMEKUWA DUNI

Ruth 4:15 mwambie Mungu arejeshe uchumi katika maisha yako ambayo unayaona sasa yamekuwa duni. Naomi aliishi maisha duni sana baada ya mume wake na watoto wake kufariki. Mungu aweza kukurejeshea uchumi na maisha bora na kukung’arisha kama Naomi.

Pia angalia ahadi ya Mungu katika Isaya 58:12

UREJESHO KWENYE MAGONJWA

Yeremia. 30:17 “Lakini nitakurudishia afya yako na kuyaponya majeraha yako asema BWANA”.  Omba mwambie Mungu umeahidi kunirudia afya yangu sawa sawa na neno lako. Yesu yule yule aliyeponya maelfu elfu bado anaponya hata leo maana yeye hajabadili Ebrania 13:8

UREJESHO KWENYE MIAKA ILIYOPOTEA

Yoeli 2:25. Mwambie Mungu rejesha miaka yangu yote niliyopoteza. Mungu hurejesha muda wote tulioupoteza kinyume na mapenzi yake tukimrudia.

UREJESHO KATIKA MOYO ULIOJERUHIWA

Zaburi 34:17-19. Mungu hurejesha upya roho za watu waliopita kwenye mateso na kuvunjika moyo sababu ya taabu mbalimbali za dunia. Ikiwa ni katika ndoa, kazini au kwenye jamii. Mungu yuko karibu nawe uliyevunjika moyo na Bwana yuko tayari kukuokoa. Pia Zaburi 51:12.

ENDELEA KUFUATILIA BLOGSPOT HII ITAKUFUNGUA KWA MAANDIKO YALIYOPO NDANI YAKE.

 TUMA MAHITAJI HAPA

+255762756542

WATSAP: +255762756542

Post a Comment

0 Comments