Follow us

ILI UWEZE KUWA HODARI KATIKA MUNGU?

Tangazo

MCHUNGAJI LAURENT MPOMA
NCHI YA UKOMBOZI MINISTRY

ILI UWEZE KUWA HODARI KATIKA MUNGU

1. Vaa silaha za MUNGU.

 Waefeso 6:11 "Vaeni silaha zote za MUNGU, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani."

Baada ya wewe kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako inakupasa sana kufanya mambo ya Kibiblia yanaweza kukufanya uwe hodari katika MUNGU na katika uweza wa nguvu zake.

Silaha za MUNGU zinaweza kukufanya uwe hodari katika MUNGU maana MUNGU hatakuwa kinyume na wewe.

Silaha hizi za MUNGU tunazivaa kwa kuziishi na sio kuzitaja tu.

2. Mpokee ROHO MTAKATIFU.

Yohana 14:26 " Lakini huyo Msaidizi, huyo ROHO MTAKATIFU, ambaye BABA atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia."

Ukimpokea ROHO MTAKATIFU hakika utapokea na yote yaayomhusu.

Utapokea nguvu, utapokea maelekezo ya kukusaidia, utapokea kibali kikuu kwa MUNGU n.k

3. Lifanyie kazi Neno la MUNGU.

 Yakobo 1:22 "Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu."

 

4. Nyenyekea kwa MUNGU katika KRISTO YESU.

1 Petro 5:6 "Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa MUNGU ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake;"

5. Ishi maisha ya kuongozwa na ROHO MTAKATIFU utashinda kila nguvu za kishetani.

 1 Yohana 4:4 "Ninyi, watoto wadogo, mwatokana na MUNGU nanyi mmewashinda, kwa sababu yeye(ROHO MTAKATIFU) aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye(Shetani) aliye katika dunia."

 

6. Zitafute nguvu za MUNGU kwa maombi yanayoambatana na maisha matakatifu.

 Waefeso 6:18 "kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika ROHO, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote;"

Maombi ni njia mojawapo kuu ya kukufanya uwe hodari katika MUNGU maana maombi yatakufanya uwe mshindi daima.

Maombi yapo ya aina mbili yaani maombi ya bila kufunga na kisha kuna maombi ya kufunga(Mathayo 17:21), haya nayo ni ya muhimu sana sana ili uwe mshindi mwenye nguvu daima.

Hivyo tafuta daima nguvu za MUNGU.

1 Nyakati 16:11 "Mtakeni BWANA na nguvu zake; Utafuteni uso wake siku zote."

 

7. Mtumikie Bwana YESU Mwokozi.

 Danieli 11:32b " lakini watu wamjuao MUNGU wao watakuwa hodari, na kutenda mambo makuu."

 Ukimtumikia MUNGU kwa usahihi katika KRISTO YESU lazima uwe hodari.

1 Wakorintho 15:58 "Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya BWANA sikuzote, kwa kuwa mwajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika BWANA."

 Nguvu za MUNGU kubwa sana huwa zinaambatana na Neno la MUNGU, hivyo unavyomtumikia Bwana YESU ujue nguvu za MUNGU lazima ziambatane na wewe.


MUNGU AKUBARIKI SANA

MAOMBI NA MAOMBEZI

PIGA +255714890889

Post a Comment

0 Comments