YAFUATAYO NI BAADHI YA
MAMBO MUHIMU AMBAYO ROHO WA MUNGU AMENIFUNULIA TUJUE MUNGU ALIVYOKUSUDIA
KWA AJILI YETU WATOTO WAKE:-
1. Ni mwaka wa kuwekeza na kukusanya (kuweka
akiba) Zaidi kwa kuwa kuna mabadiliko ya kiuchumi yanakuja.
Biblia
katika kitabu cha Mwanzo 41:35-36 inasema ‘Na wakusanye chakula chote cha miaka
hii myema ijayo, wakaweke akiba ya nafaka mikononi mwa Farao wakakilinde kuwa
chakula katika miji. Na hicho chakula kitakuwa akiba ya nchi kwa ajili ya miaka
hiyo saba ya njaa, itakayokuwa katika nchi ya Misri, nchi isiharibike kwa
njaa’.
2. Ni mwaka wa kucheka kwa kuwa BWANA anaenda
kuwafurahisha watu wake wale wanaomtegemea.
Ayubu 42:10
‘Kisha BWANA akageuza uteka wa Ayubu, hapo alipowaombea rafiki zake; BWANA naye
akampa Ayubu mara mbili kuliko hayo aliyokuwa nayo kwanza’. Ukisoma kitabu cha Ayubu sura 1-2 utaona
habari za Ayubu na jinsi Shetani alivyoharibu maisha yake kwa ujumla. Kilikuwa
ni kipindi kigumu sana kwa Ayubu, hata hivyo hizo ndio nyakati zilizokuwa zimeruhusiwa
juu yake. Maandiko yanaonyesha kuwa baada ya Ayubu kusimama vizuri na Mungu
wake katika kipindi hicho kigumu, BWANA alimrejeshea Ayubu maradufu kila
kilichokuwa kimeharibiwa na Shetani yaani furaha, afya, watoto na mali zake
zote.
3. Ni mwaka wa amani utakaokupa fursa ya
kujijenga na kutimiza mapenzi ya Mungu kwa mwaka husika.
1 Waflme 5:
3-5, ‘Umemjua Daudi baba yangu jinsi asivyoweza kujenga nyumba kwa jina la
Bwana, Mungu wake, kwa sababu ya vita vilivyomzunguka pande zote, hata Bwana alipowatia
watu chini ya nyayo zake. Ila leo Bwana, Mungu wangu, amenipa amani kila
upande; hakuna adui, wala tukio baya. Nami, tazama, nakusudia kujenga nyumba
kwa jina la Bwana, Mungu wangu, kama Bwana alivyomwambia Daudi baba yangu,
akisema, Mwana wako, nitakayemweka katika kiti chake cha enzi mahali pako,
ndiye atakayeijenga nyumba kwa jina langu’.
Maneno haya
yalisemwa na Sulemani baada ya kutawazwa kuwa mfalme kufuatia kifo cha baba
yake Daudi. Ukisoma Biblia yako vema utagundua kwamba utawala wa Daudi ulikuwa
na vita sana, na kwa sababu ya vita na damu nyingi iliyomwagika katika kipindi
chake BWANA alimzuia Daudi asimjengee Hakalu. Hekalu lilijengwa kipindi cha
mwanawe Sulemani. Naam ili Sulemani
aweze kujenga hekalu vema, BWANA akampa amani pande zote na kazuia baya lolote
lisitokee.
MUNGU AKUBARIKI SANA
0 Comments