Nikusudi la Mungu mwanadamu aishi maisha mazuri na
yakumpendeza yeye,tena Mungu alimuweka mwanadamu kuwa mtawala katika ulimwengu
huu ambao Mungu aliuumba ila tu mwanadamu alipoteza nafasi hiyo baada ya
kufanya dhambi (Yer.5:25)lakini Mungu kwa neema yake na upendo wake alimtuma
Mwanawe wa pekee Yesu Kristo awakomboe wanadamu(Yoh.3:16) nakuwapatanisha na
Mungu na hivyo kuirudisha nafasi ile ambayo Mungu alimuwekea mwanadamu ila
shetani kwa ujanja wake
aliichukua(Mwanz.3:13)
Fuatana nami katika mafundisho
haya,tafakari kwa kina kisha chukua hatua
Ukisoma katika Uf.12:17 utaona kuwa shetani amekasirika
dhidi ya mwanamke na amedhamiria kufanya vita juu ya uzao wa mwanamke lakini
hasira yake ni juu ya wale wazishikao sheria za Mungu na wenye ushuhuda wa Yesu
(Ebra.12:1); nia yake ni atawale kizazi cha mwanamke,wale wasiompinga hana
hasira nao maana wanakuwa chini yake (Ef.2:1-3).
Katika Mwanzo 3 tunaona kuwa Wazazi wetu wa kwanza,adamu na
hawa,walimkabidhi shetani dunia waliyopewa na Mungu (2Kor.4:3-4), hivyo basi
shetani akatumia hila na uongo (Yoh.8:44) ili awafunge waweke patano/mkataba
nao
Shetani ni mwerevu mwenye ngazi ya kimalaika,kumbuka hapo
mwanzo alikuwa malaika mwenye cheo kizuri huko Mbinguni(Isa.14:9-17),anafahamu
tabia za Mungu na mambo yote mazuri ambayo Mungu ameyaweka kwaajili ya mwanadamu
ndio maana alitaka kumpindua Mungu akashindwa na badala yake amekusudia
kumpotosha mwanadamu ili asipate yale ambayo Mungu ameweka kwaajili ya wanadamu
Kumbuka mwanadamu nizaidi ya malaika ndio maana malaika
hakupewa kutawala na Mungu isipokuwa mwanadamu(Mwanz.1:26, 1Kor.6:3).
Shetani naye anatamani kuabudiwa na kuogopwa na mwanadamu
ndio maana anafanya yote haya(Isa.14:13); biblia inasema shetani alipambana na
malaika,hivyo mwanadamu peke yako huwezi kupambana naye isipokuwa ukiwa na Nguvu za Mungu na kwa
kumkubali Yesu katika maisha yako maana yeye ni Jemedari wa vita(Rum.10:9-10).
Shetani anaelewa kwamba Mungu ni wa maagano,na agano linadumu kizazi hata kizazi (Torati 8:18,Zab.102:12) Shetani anafanya mbinu za kuwadanganya wanadamu wapuuze mkataba wao na Mungu halafu anawashawishi kuanzisha mkataba mpya nao(2Tim.2:26)
·
Falme na mamlaka
·
Wakuu wa giza hili
· Jeshi la pepo wabaya
MUNGU AKUBARIKI SANA
M
0 Comments