Follow us

SOMO: VIFUNGO

Tangazo

 

MCH: LAURENT MPOMA

NCHI YA UKOMBOZI MINISTRY

SOMO: VIFUNGO

Kifungo cha kipepo ni adhabu ya mtu kuwekwa jela kipepo na mawakala wa shetani.

Baadhi ya vifungo hivyo  vimetajwa katika Isaya 42:22 ''Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana asemaye, Rudisha. '' acha nikifafanulie. 

Vifungo hivyo vya giza ni hivi.

    1. Kuibiwa ufahamu kipepo ili ulitumikie kusudi la shetani na sio la MUNGU.

''Lakini watu hawa ni watu walioibiwa ''

Kuna watu wengi fahamu zao zimefunga kipepo kiasi kwamba wanalitumikia kusudi la shetani na sio la MUNGU, Leo kwa njia ya maombi yako katika jina la YESU KRISTO hakikisha unakiharibu kifungo hicho cha giza kilichokufunga ufahamu.

Fikra zako zinatakiwa zimtii KRISTO na sio kutii majini na mizimu.

2 Kor 10:3-5 '' Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili;  (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika MUNGU hata kuangusha ngome;)  tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya MUNGU; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii KRISTO; ''

   2. Kutekwa na nguvu za giza.

 ''Lakini watu hawa ni watu waliotekwa''

Baadhi ya dalili ya mtu aliye katika kifungo cha kutekwa na nguvu za giza ni kuonewa sana na majini au wachawi kwa sababu tu wamekuteka katika ulimwengu wa roho.

Somo linaitwa jinsi ya kutoka kwenye vifungo vya giza, ni muhimu kujua kwamba kila kifungo kina kanuni zake hadi utoke katika kifungo hicho, kuna vifungo vingine huhitaji hata maombi bali unahitaji tu kubadilika tabia na kifungo hicho kinaondoka.

   3.Kunaswa katika mashimo ya giza.

''Lakini watu hawa ni watu  walionaswa katika mashimo''

Inawezekana wewe uko katika kifungo cha mashimo ya giza.

Inawezekana uko katika shimo la dhambi.

Inawezekana wewe uko katika shimo la madeni au kufilisika.

Inawezekana umenaswa katika shimo la magonjwa na hadi kwa sasa unadhani hutapona kabisa kulingana na jinsi unavyouona ugonjwa wako.

Inawezekana uko katika shimo la kifo ili siku chache zijazo upate ajali mbaya waliyoipanga wachawi na wakuu wa giza ili ikupate.

Wakati mwingine kupitia ndoto ambazo unaota unakuwa unajulishwa aina ya kifungo ambacho umefungwa ili ujue jinsi ya kutoka katika kifungo hicho.

Inawezekana wewe huota ndoto kabisa ukiwa ndani ya shimo refu sana na huoni pa kutokea, hapo unaonyeshwa aina ya kifungo kinachokutesa.

Ndugu, leo katika jina la YESU KRISTO nakuomba kimbilia maombezi makanisani na utaombewa na kifungo hicho kukuacha.

   4. Kufichwa katika magereza.

''Lakini watu hawa ni watu waliofichwa katika magereza ''

Kuna kifungo cha giza kinaitwa gereza.

Inawezekana wewe uko katika gereza la magaonjwa, kukataliwa,kudhalauliwa bila sababu, kutengwa n.k

Inawezekana ndoa yako iko gerezani, inawezekana uchumba wako uko gerezani, iinawezekana biashara yako au wito wako viko gerezani

Ndugu leo hakikisha unandoka katika gereza la kipepo ulimofungwa kipepo.

    5. Kuwa Mawindo ya nguvu za giza.

''Lakini watu hawa ni watu ambaob  wamekuwa mawindo, ''

Kuna kifungo kinaitwa mawindo, inawezekana wewe siku zote uko katika mawindo ya majini au wachawi.

Kuna watu huwa hawalali usiku kwa sababu wako katika mawindo ya wachawi na majini.

Mama mmoja kutoka nchi jirani siku moja alinipigia simu ili nimuombee, nilipomuombea kesho yake alituma sadaka kisha akasema hivi ‘’ Mtumishi Mabula huwezi kuamini mimi na mtoto wangu tuna zaidi ya miezi miwili bila kulala usiku, jana uliponiombea ndio nilishangaa maana nilipojaribu kulala nikashtuka nikidhani wachawi sasa wanakuja kumbe ili asubuhi saa mbili yaani nililala salama kwa mara ya kwanza’’

Mathayo 18:18 '' Amin, nawaambieni, yo yote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yo yote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni. ''

 

MUNGU AKUBARIKI SANA.

MAOMBI NA MAOMBEZI WASILIANA NA MCHUNGAJI LAURENT MPOMA

PIGA: 0762756542, 0714890889

WATSAP: 0762756542

JIFUNZE ZAIDI HAPA>>>"shorturl.at/tFKU9"

Post a Comment

0 Comments